Mdau: Bilioni 151 zilizozidi kwenye ujenzi wa Uwanja wa Arusha zingeweza kujenga Barabara ya lami Kilometa 151

Mdau: Bilioni 151 zilizozidi kwenye ujenzi wa Uwanja wa Arusha zingeweza kujenga Barabara ya lami Kilometa 151

Hawa wasomi wetu majanga. Kukadiriwa sio sawa na kukusudiwa.

Kabla ya mradi kuanza wataalam wanakadiria gharama za ujenzi. Gharama ya awali ya mradi inajulikana baada ya kuingia mkataba na Mkandarasi. Gharama kamili ya mradi inajulikana baada ya mradi kufungwa baada ya muda wa matazamio kukamilika.

Hii maana yake ni kuwa hata hiyo gharama aliyotaja CAG inaweza kuongezeka au kupungua. Ongezeko linaweza kusababishwa na malipo ya Mkandarasi kucheleweshwa, kutokabidhiwa eneo tupu katika wakati muafaka, ucheleweshaji wa maamuzi, mazingira ya ujenzi, matakwa ya mwenye mradi kuongezeka, kuwa tofauti na ilivyo katika mkataba n.k.

Zinaweza kupungua kama mwenye mwenye mradi atapunguza baadhi ya kazi zilizomo katika mkataba, mkandarasi akichelewesha kazi bila sababu za kuridhisha n.k.

Amandla...
 
Hawa wasomi wetu majanga. Kukadiriwa sio sawa na kukusudiwa. Kabla ya mradi kuanza wataalam wanakadiria gharama za ujenzi. Gharama ya awali ya mradi inajulikana baada ya kuingia mkataba na Mkandarasi. Gharama kamili ya mradi inajulikana baada ya mradi kufungwa baada ya muda wa matazamio kukamilika.
Hio variation sio torelable mzee project ata uki-estimate 25% as a miscellaneous still haitafika hio stated figure pana shida hapo
 
Hawa wasomi wetu majanga. Kukadiriwa sio sawa na kukusudiwa. Kabla ya mradi kuanza wataalam wanakadiria gharama za ujenzi. Gharama ya awali ya mradi inajulikana baada ya kuingia mkataba na Mkandarasi. Gharama kamili ya mradi inajulikana baada ya mradi kufungwa baada ya muda wa matazamio kukamilika. Hii maana yake ni kuwa hata hiyo gharama aliyotaja CAG inaweza kuongezeka au kupungua. Ongezeko linaweza kusababishwa na malipo ya Mkandarasi kucheleweshwa, kutokabidhiwa eneo tupu katika wakati muafaka, ucheleweshaji wa maamuzi, mazingira ya ujenzi, matakwa ya mwenye mradi kuongezeka, kuwa tofauti na ilivyo katika mkataba n.k. Zinaweza kupungua kama mwenye mwenye mradi atapunguza baadhi ya kazi zilizomo katika mkataba, mkandarasi akichelewesha kazi bila sababu za kuridhisha n.k.

Amandla...

Umesoma vizuri fundi mchundo? Wamesema mkataba uliosainiwa sio hizo sababu ulizozisema, hizi sio costs overrun wakati wa execution!

Ni mkataba ulipoenda kwa wenye maamuzi wakainflate kuweka mafungu yao!

Hii sio rocket science kuelewa
 
Hawa wasomi wetu majanga. Kukadiriwa sio sawa na kukusudiwa. Kabla ya mradi kuanza wataalam wanakadiria gharama za ujenzi. Gharama ya awali ya mradi inajulikana baada ya kuingia mkataba na Mkandarasi. Gharama kamili ya mradi inajulikana baada ya mradi kufungwa baada ya muda wa matazamio kukamilika. Hii maana yake ni kuwa hata hiyo gharama aliyotaja CAG inaweza kuongezeka au kupungua. Ongezeko linaweza kusababishwa na malipo ya Mkandarasi kucheleweshwa, kutokabidhiwa eneo tupu katika wakati muafaka, ucheleweshaji wa maamuzi, mazingira ya ujenzi, matakwa ya mwenye mradi kuongezeka, kuwa tofauti na ilivyo katika mkataba n.k. Zinaweza kupungua kama mwenye mwenye mradi atapunguza baadhi ya kazi zilizomo katika mkataba, mkandarasi akichelewesha kazi bila sababu za kuridhisha n.k.

Amandla...
Una hoja ya unatakiwa usikilizwe lakini pamoja na hayo,wadau lazima waongeze cha juu tu
 
Hio variation sio torelable mzee project ata uki estimate 25% as a miscellaneous still haitafika hio stated figure panashida apo
Variation haiwi based kwenye estimate. Kama inaonekana quotation ya Mkandarasi imezidi mno estimate, njia pekee ni kukataa kuingia kwenye mkataba nae.

Lakini kwa vile huu mradi ulikuwa ni wa single source ni lazima palifanyika majadiliano ambayo yalimconvince mwenye mradi kuwa makisio yake hayakuwa sahihi.

Na hilo linawezekana sana kama makisio yalifanyika bila kuwa na michoro au BoQ. Hatujaambiwa kama mradi ulikuwa wa kawaida ( mshitiri, mshauri na mkandarasi) au Design and Build.

Nadhani ulikuwa Design and Build maana mshauri hatajwi hata sehemu moja. Ndio matatizo ya Design and Build.

Amandla...
 
Hawa wasomi wetu majanga. Kukadiriwa sio sawa na kukusudiwa. Kabla ya mradi kuanza wataalam wanakadiria gharama za ujenzi. Gharama ya awali ya mradi inajulikana baada ya kuingia mkataba na Mkandarasi. Gharama kamili ya mradi inajulikana baada ya mradi kufungwa baada ya muda wa matazamio kukamilika. Hii maana yake ni kuwa hata hiyo gharama aliyotaja CAG inaweza kuongezeka au kupungua. Ongezeko linaweza kusababishwa na malipo ya Mkandarasi kucheleweshwa, kutokabidhiwa eneo tupu katika wakati muafaka, ucheleweshaji wa maamuzi, mazingira ya ujenzi, matakwa ya mwenye mradi kuongezeka, kuwa tofauti na ilivyo katika mkataba n.k. Zinaweza kupungua kama mwenye mwenye mradi atapunguza baadhi ya kazi zilizomo katika mkataba, mkandarasi akichelewesha kazi bila sababu za kuridhisha n.k.

Amandla...
Mmmh!kwani hayo yote si hua yanafanyika kwenye upembuzi yakinifu?

Na tenda si hua zinatangazwa watu wanashindania inakuaje mtu akabidhiwe eneo la mradi ambalo ni chafu chafu litakalo ongeza gharama Tena kwani yeye si anakua kapaona mwanzo kafanya tathimini zake au?

Inakuaje wataalam wanakadilia kabla hata mkandarasi hajafanya feasibility study ili na yeye aje na makadilio yake kulingana na alivyoliona eneo na bado hao wataalam wanapeleka kupitisha Moja kwa Moja?

Kwanini baada ya mkandarasi kuona eneo na changamoto zake wasirudi mezani kwenye mazungumzo kabla ya kupitisha bajeti waliyo ikadilia peke Yao.
 
Hizo km 151 tayari zingeunganisha Arusha na Mara au Simiyu na kuvuta mashabiki kadhaa tokea mikoa hiyo jirani huku mawasiliano baina ya mikoa hiyo ikiimarika.
 
Huo ni wizi wa wazi.

Kwa mradi mkubwa kama ule usingeweza kuwa single source.

Ukisikiliza maelezo ya Msigwa ndio utajua kabisa wizi umefanywa.

Msigwa anasema walitumia single source sabaabu mradi ulikuwa wa dharula lakini hapohapo anasema baada ya Tanzania kuteuliwa kuwa mwenyeji wa mashindano ya CAF waliona inabidi wajenge uwanja unaokidhi vigezo vya CAF.

Maelezo yake yanaonyesha huu mradi haukuwa wa dharula sababu ulianza kaabla ya Tanzania kuteuliwa kuwa mwenyeji wa AFCON.

Kwa miradi mikubwa kama hii lazima kuwe na BOQ na kama BOQ ingekuwepo hata CAG asingehoji.
 
Cha ajabu Msigwa anapingana hata na taratibu za manunuzi zilizowekwa na PPRA
 
Hawa wasomi wetu majanga. Kukadiriwa sio sawa na kukusudiwa. Kabla ya mradi kuanza wataalam wanakadiria gharama za ujenzi. Gharama ya awali ya mradi inajulikana baada ya kuingia mkataba na Mkandarasi. Gharama kamili ya mradi inajulikana baada ya mradi kufungwa baada ya muda wa matazamio kukamilika. Hii maana yake ni kuwa hata hiyo gharama aliyotaja CAG inaweza kuongezeka au kupungua. Ongezeko linaweza kusababishwa na malipo ya Mkandarasi kucheleweshwa, kutokabidhiwa eneo tupu katika wakati muafaka, ucheleweshaji wa maamuzi, mazingira ya ujenzi, matakwa ya mwenye mradi kuongezeka, kuwa tofauti na ilivyo katika mkataba n.k. Zinaweza kupungua kama mwenye mwenye mradi atapunguza baadhi ya kazi zilizomo katika mkataba, mkandarasi akichelewesha kazi bila sababu za kuridhisha n.k.

Amandla...
Upo sawa lakini makadirio ya gharama yaje ku double hapo kuna walakini mkuu. Yanii gharama za mradi zizidi makadirio kwa aslimia 80+??
 
Mmmh!kwani hayo yote si hua yanafanyika kwenye upembuzi yakinifu? Na tenda si hua zinatangazwa watu wanashindania inakuaje mtu akabidhiwe eneo la mradi ambalo ni chafu chafu litakalo ongeza gharama Tena kwani yeye si anakua kapaona mwanzo kafanya tathimini zake au?
Sio lazima. Miradi yetu mingi haifanyiwi feasibility study.

Kuna tenda za aina nyingi. Za kawaida ni hizo za kukaribisha makandarasi washindane. Na kuna kama hii ambayo Mkandarasi mmoja ndie anakaribishwa kuleta maombi. Zote zinaruhusiwa.

Hali ya eneo sio wajibu wa Mkandarasi. Ila kama ni Design and Build bila shaka ataingiza gharama za kusafisha katika hesabu zake.

Mara nyingi ucheleweshaji unatokana na eneo kuwa na watu wanaolitumia. Ni wajibu wa Mwenye Mradi kuhakikisha kuwa hawapo kabla ya kuingia katika mkataba. Akiingia katika mkataba kabla ya kuwaondoa, Mkandarasi ataongeza gharama za kusubiri eneo liwe wazi ili aweze kuanza kazi.
Inakuaje wataalam wanakadilia kabla hata mkandarasi hajafanya feasibility study ili na yeye aje na makadilio yake kulingana na alivyoliona eneo na bado hao wataalam wanapeleka kupitisha Moja kwa Moja?
Mkandarasi hawezi kufanya feasibility study. Sio wajibu wake.

Katika miradi ya kawaida, mshauri ndiye anatayarisha makabrasha yote yanayohusiana na mradi ( michoro, specifications, boq n.k.) ambayo Mwenye Mradi anakabidhi kwa Mkandarasi ili ajaze bei yake ya kuzifanya hizo kazi.

Kama ni mkataba wa aina ya Kubuni na Kujenga, Mkandarasi ndie anayetayarisha makabrasha ya mradi na kuweka bei yake ya kuifanya hiyo kazi. Majadiliano yanakuwa katika bei na pengine na aina na ubora wa vitu vitakavyowekwa.
kwanini baada ya mkandarasi kuona eneo na changamoto zake wasirudi mezani kwenye mazungumzo kabla ya kupitisha bajeti waliyo ikadilia peke Yao.
Mkandarasi anachoweza kufanya ni kuainisha tu changamoto anazoziona lakini halazimiki kufanya hivyo. Mkandarasi hakadirii bajeti.

Anayekadiria bajeti ni mwenye mradi na anapaswa kufanya hivyo kabla hajaanza kutafuta mkandarasi. Mkandarasi anaweza kuona changamoto akakaa kimya ili akupige wakati wa utekelezaji wa mradi.

Ndio maana ni wajibu wa mwenye mradi kuhakikisha hapati nafasi hiyo.

Mkandarasi ni mfanyabiashara na ni wajibu wake kuhakikisha kuwa anapata faida kubwa inavyowezekana katika mradi.

Amandla....
 
Upo sawa lakini makadirio ya gharama yaje ku double hapo kuna walakini mkuu. Yanii gharama za mradi zizidi makadirio kwa aslimia 80+??
Inawezekana kama Mkadiriaji hana experience na mradi wa aina ile. Ukweli ni kuwa wataalam wetu wengi serikalini hawana hiyo experience.

Amandla...
 
Anaandika Mh God Godbless J Lema.

Au tutengeneze !!!

TAAKUTA.
Taasisi ya Aibu na Kusuta Tanzania

Kaulimbiu:
Aibu Kwanza, Uwajibikaji Baadaye

Dhamira:
Kuwataja hadharani wale wote wanaosababisha hasara ya fedha za umma ili waone aibu ya taifa.

Majukumu Makuu:
•Kushirikiana na Public Procurement Regulatory Authority na Prevention and Combating of Corruption Bureau kupata orodha ya wahusika
•Kutangaza majina ya “Wasutwe” kila mwaka
•Kuendesha kampeni za VIBE ya AIBU kwenye mitandao ya kijamii

Huduma Maalum:
•Aibu Index: Kipimo cha kitaifa cha nani kaaibisha zaidi
•Wall of Shame: Orodha ya wazi ya waliotajwa
•Badge ya Aibu: Cheti rasmi cha kusutwa kinachoweza kusambazwa online .

Hitimisho:
Kwa sababu wakati mwingine sheria zipo kimya…TAAKUTA inasema kwa sauti kubwa, INATOSHA.
@
 
Hizo km 151 tayari zingeunganisha Arusha na Mara au Simiyu na kuvuta mashabiki kadhaa tokea mikoa hiyo jirani huku mawasiliano baina ya mikoa hiyo ikiimarika.
Hata hii barabara ya Morogoro (Morogoro road); kutoka Kibaha mpaka Morogoro ingekuwa imekwisha.
 
Inawezekana kama Mkadiriaji hana experience na mradi wa aina ile. Ukweli ni kuwa wataalam wetu wengi serikalini hawana hiyo experience.

Amandla...
Unataka kuniambia ndio mradi mkubwa wa kwanza tumefanya. Nchii hii haina wataalamu wa kufanya feasibility study, hakuna hata consultants?

Tumefanya miradi mikubwa kama Mkapa Stadium, Daraja Kigbamboni, Busisi_Kigongo, BRT n.k leo hii uje kusema hatuna wataalam? Mkuu tukubali hapa kwamba wizi upo tusilete janja janja
 
Back
Top Bottom