Mdau: Bilioni 151 zilizozidi kwenye ujenzi wa Uwanja wa Arusha zingeweza kujenga Barabara ya lami Kilometa 151

Mdau: Bilioni 151 zilizozidi kwenye ujenzi wa Uwanja wa Arusha zingeweza kujenga Barabara ya lami Kilometa 151

Hawa wasomi wetu majanga. Kukadiriwa sio sawa na kukusudiwa. Kabla ya mradi kuanza wataalam wanakadiria gharama za ujenzi. Gharama ya awali ya mradi inajulikana baada ya kuingia mkataba na Mkandarasi. Gharama kamili ya mradi inajulikana baada ya mradi kufungwa baada ya muda wa matazamio kukamilika. Hii maana yake ni kuwa hata hiyo gharama aliyotaja CAG inaweza kuongezeka au kupungua. Ongezeko linaweza kusababishwa na malipo ya Mkandarasi kucheleweshwa, kutokabidhiwa eneo tupu katika wakati muafaka, ucheleweshaji wa maamuzi, mazingira ya ujenzi, matakwa ya mwenye mradi kuongezeka, kuwa tofauti na ilivyo katika mkataba n.k. Zinaweza kupungua kama mwenye mwenye mradi atapunguza baadhi ya kazi zilizomo katika mkataba, mkandarasi akichelewesha kazi bila sababu za kuridhisha n.k.

Amandla...
Engeener makonyola,,,kwenye moja na mbili.
 
Unataka kuniambia ndio mradi mkubwa wa kwanza tumefanya. Nchii hii haina wataalamu wa kufanya feasibility study, hakuna hata consultants?
Niambie mradi gani wa serikali ambao umefanyiwa feasibility study? Sisi hata miradi ya ujenzi wa matundu ya vyoo inatusumbua sembuse Stadium?
Tumefanya miradi mikubwa kama Mkapa Stadium, Daraja Kigbamboni, Busisi_Kigongo, BRT n.k leo hii uje kusema hatuna wataalam? Mkuu tukubali hapa kwamba wizi upo tusilete janja janja
Mkapa Stadium ulifadhiliwa, ulibumiww na ulijengwa na Wachina. Daraja la Kigamboni lilibuniwa na kujengwa na wachina.

Aidha, kumbuka kila aina ya ujenzi una utaalam wake. Aliyesimamia ujenzi wa Bwawa la Nyerere anaweza kushindwa kujua changamoto za ujenzi wa Stadium.

Ukweli ni kuwa hatuna wataalam wenye uwezo wa kutayarisha michoro na kufanya makisio ya uwanja wa michezo wa kisasa serikalini.

Aidha, hapo zamani miradi kama hii ilikuwa inasimamiwa na wizara ya ujenzi ambako ndiko panatakiwa kuwa na hazina ya wataalam waliobobea wa masuala haya. Sasa hivi kila wizara inajijengea inavyotaka. Haya ndio matokeo yake.

Mwisho, ujenzi wa stadium ya kisasa unahitaji utaalam wa kipekee. Ndio maana Stadium ya Beijing ya Olympics ilibuniwa na mtaalam kutoka nje. Tofauti ya wachina na sisi ni kuwa walitumia nafasi ile kujifunza na sasa hivi wana wataalam wa kutosha. Sijui wataalam wetu wangapi walijifunza kutokana na mradi wa ujenzi wa Stadium ya Mkapa!

Wizi unawezekana kuwa upo, hilo siwezi kubisha. Lakini sio kubwa hizi gharama zilizotajwa ni kubwa mno.

Amandla...
 
Subirini u turn mkatayopigiwa kuhusu ripoti ya uwanja huo 😄

Ova
 
Niambie mradi gani wa serikali ambao umefanyiwa feasibility study? Sisi hata miradi ya ujenzi wa matundu ya vyoo inatumbua sembuse Stadium?

Mkapa Stadium ulifadhiliwa, ulibumiww na ulijengwa na Wachina. Daraja la Kigamboni lilibuniwa na kujengwa na wachina. Aidha, kumbuka kila aina ya ujenzi una utaalam wake. Aliyesimamia ujenzi wa Bwawa la Nyerere anaweza kushindwa kujua changamoto za ujenzi wa Stadium.
Ukweli ni kuwa hatuna wataalam wenye uwezo wa kutayarisha michoro na kufanya makisio ya uwanja wa michezo wa kisasa serikalini.
Aidha, hapo zamani miradi kama hii ilikuwa inasimamiwa na wizara ya ujenzi ambako ndiko panatakiwa kuwa na hazina ya wataalam waliobobea wa masuala haya. Sasa hivi kila wizara inajijengea inavyotaka. Haya ndio matokeo yake.

Mwisho, ujenzi wa stadium ya kisasa unahitaji utaalam wa kipekee. Ndio maana Stadium ya Beijing ya Olympics ilibuniwa na mtaalam kutoka nje. Tofauti ya wachina na sisi ni kuwa walitumia nafasi ile kujifunza na sasa hivi wana wataalam wa kutosha. Sijui wataalam wetu wangapi walijifunza kutokana na mradi wa ujenzi wa Stadium ya Mkapa!

Wizi unawezekana kuwa upo, hilo siwezi kubisha. Lakini sio kubwa hizi gharama zilizotajwa ni kubwa mno.

Amandla...
Wanaokula hela za huo uwanja mna maneno mengi sana. Najua hamtafanywa kitu, haya peleka majibu kwa mkaguzi
 
Ndio maana kuna muda nawaza hata kujiua kukwepa aibu ya nchi hii
Siku Ambayo Utaamua Kujing'atisha Mbao,,Usisahau Nishtua Tuje Tuzikunje Sanka/Maweed Haswaa,,Ili Uweze Kwenda Kwa Amani Na Muumba Akujalie Pumziko Lililo Jema....
 
kwa hiyo wewe ndio unajiona una akili
hii nchi inavituko vingi🤣🤣🤣

Bila hata kukariri huoni kwamba makonda alitangulizwa ili mzigo utumwe? Makonda hata akiwa afisa mtendaji acha kuwa RC ana pawa na ni facilitator makini sana wa deals za wakubwa na ni kijana asiyeogopa chochote wala yeyote na ana guts za kusema lolote kwa yeyote anayegusa maslahi yake au ya anayemtumia! So utajua mzigo unaelekea wapi ile ni conduit tu
 
Anayekadiria bajeti ni mwenye mradi na anapaswa kufanya hivyo kabla hajaanza kutafuta mkandarasi. Mkandarasi anaweza kuona changamoto akakaa kimya ili akupige wakati wa utekelezaji wa mradi.
Makadirio ndo Bajeti, wametupeleka mbali sana na makadirio aisee.

hivyo vitu CUF wamesema viongezwe ilitakiwa vije as extra cost .. ila ni double cost na change inabaki.

Mkuu sina utaalamu na mambo ya tenda lkn apa naona wazi wazi kabisa tumepigwa.
 
Ndiyo maana haitaki kuambiwa ukweli ,inapiga mipesa mingi sana ,ukienda Mbweni unajiuliza hii mijengo ya hawa viongozi yenye thamani hadi ya bilioni 5 ni mshahara na mikopo kweli? Mbona ukipiga hesabu ya mishahara yake yote kwa miaka 20 haifiki hizo Bilioni 5?
 
Back
Top Bottom