Mdau Huwa unasalimia mtu unayekaa naye siti moja kwenye daladala au unakaushaga

Mdau Huwa unasalimia mtu unayekaa naye siti moja kwenye daladala au unakaushaga

New Designer

JF-Expert Member
Joined
Aug 8, 2025
Posts
551
Reaction score
879
Habari wakuu

Binafsi mimi huwa na mikausho mikali sana ili kutojipa stress maana wengi kwenye dala dala wanakuwa kama wamevurugwa hivi, unaweza kusalimia mtu halafu akakunyamzia.

Vipi Wewe unatabia gani kwenye daladala ?

#Oktoba_tunatoka
 
Unajinyima fursa sana ,hapo ulipo hukupaswa kuwa kiuchumi (fanyia kazi )
 
Inategemeana na unamuonaje huyo abiria, kama ni mchangamfu unamsalimia kama kanuna unapiga kimya tu. Kuna wengine ukiingia tu garini unawasalimia wote habari zenu abiria hamjambo? hawaitikii hata mmoja, basi unaanza kujuta kwa nini nimesalimia hawajaitikia. Bora kunyamaza tu
 
Hiyo ni tisa, kumi ni pale unaposafiri na abiria ambaye hana stori na wewe, yuko kimya tu. Mara ananua chakula anaanza kula hata bila kukukaribisha. Hawa mi huwapenda sana kwani nami huwa huru kula vyakula vyangu bila kumkaribisha, sisemi karibu chakula wala simpi. Kuna wengine ukiwakaribisha wanakujibu asante, unaweza kujisikia vibaya kwa nini hakutaka kula. Wengine wanakaribisha ule, kama huna aibu na una njaa huna hela za chakula unakula tu bila aibu
 
Kwenye kitendo Cha salamu huwa Nampa tu mtu haijalishi aikubali au asiikubali ila me kwangu fresh tu siwazi
 
Habari wakuu

Binafsi mimi huwa na mikausho mikali sana ili kutojipa stress maana wengi kwenye dala dala wanakuwa kama wamevurugwa hivi, unaweza kusalimia mtu halafu akakunyamzia.

Vipi Wewe unatabia gani kwenye daladala ?

#Oktoba_tunatoka
Ila ukimkuta pisi unamsalmia Au sio
 
Mi uwa nasalimia. Ila baada ya hapo natia earphones. Hamna haja ya story nyingi.
 
Inategemeana na unamuonaje huyo abiria, kama ni mchangamfu unamsalimia kama kanuna unapiga kimya tu. Kuna wengine ukiingia tu garini unawasalimia wote habari zenu abiria hamjambo? hawaitikii hata mmoja, basi unaanza kujuta kwa nini nimesalimia hawajaitikia. Bora kunyamaza tu
Unaingia kwenye Daladala unasalimia watu usiowajua ??
 
Miaka ya nyuma sana sikua mtu wa kusalimia sana watu. Kuna kipindi fulani niliishi Songea kijiji cha madaba kama miezi 8 hivi. Kule kusalimia ni utamaduni wa watu. Kila unaepishana nae lazima akusalimie na mimi nikazoea hivyo hivyo. Mpaka leo nikikutana/nikipishana na mtu yoyote sehemu yoyote lazima nimsalimie
 
Binafsi kila ninayokutana na mtu hasa mpya hukomaa kuhakikisha naitumia hiyo fursa kupata kitu kuanzia utafiti wa mazingira yake , uhusiano tu wakibinaadamu au wakibiashara .

Na mara nyingi kama nikwenye daladala hizi za nauli zisizozidi buku akijichanganya atajikuta nishamlipia nauli.

Huwa naamini kila mtu yupo na kitu ambacho ni aweza kuja kunufaika nacho kwa siku za mbele ,na ni lazima nije kunufaika nacho kweli (kwa wadada huwa suwatongozi kabisa japo huwa nimwepesi sana wakumwaga sifa za urembo kwao) finally nimejikuta nimetengeneza uwezo wa kufungua milango mingi migumu kwa gharama ndogo.

Kimsingi mtu mpya yeyote kwangu humtazama kwa jicho la fursa na nimenufaika sana kupitia hilo
 
Back
Top Bottom