Wakuu,
Kumekuwa na hiki kipande cha video huku ikielezwa kuwa hakuna kinachowashinda Bodaboda kubeba. Kwa kutumia ujuzi wako wa kubaini iwapo maudhui ni halisi au lah! Tuambie dosari zinazoonekana katika video hii
Kumekuwa na hiki kipande cha video huku ikielezwa kuwa hakuna kinachowashinda Bodaboda kubeba. Kwa kutumia ujuzi wako wa kubaini iwapo maudhui ni halisi au lah! Tuambie dosari zinazoonekana katika video hii
- Tunachokijua
- Kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii kumekuwa na video mbalimbali zikiwaonesha waendesha pikipiki za abiria (bodaboda) wakiwa wamepakia vitu mbalimbali ambavyo vinakuwa vinazua gumzo kwa watu mbalimbali kuhusu mwenendo wao kubeba vitu hivyo.
Hivi karibuni ilisambaa video ikionesha pikipiki ikiwa imebeba kinachoonekana kuwa ni nyumba juu ya vichwa vyao na juu ya paa la nyumba hiyo watu wengine wakiwa wameketi.
JamiiCheck iliwashirikisha wadau wake kuthibitisha video hiyo ili kupata mtazamo wao juu ya uelewa wa kutambua maudhui halisi dhidi ya yaliyotengenezwa kwa teknolojia ya Akili Unde. Wadau wengi walibainisha kuwa maudhui hayo si halisi na badala yake yametengenezwa kwa Teknolojia ya Akili Unde (AI).
Ufuatiliaji wa JamiiCheck kupitia nyenzo za kidigitali pia ilijiridhisha kuwa video hiyo imetengenezwa kwa AI na hivyo si halisi.
Video hiyo pia ina mijongeo isiyo ya kawaida matahalani gari linaonekana kurudi kinyumenyume badala ya kwenda mbele, kamba zinazoonekana kusika jengo hilo hazionekani ziliposhijishikiza, watu waliopo nyuma juu ya nyumba hawana baadhi ya viungo huku abiria aliyebebwa chini akionekana kuwa hana mviungo kamili nk.
Aidha jambo hilo kifizikia pia haliwezekani ukilinganisha na ukubwa wa kilichobebwa na ukubwa wa pikipiki namna kilivyofungwa na watu waliokaa juu.