Mdau, nashauri msipomsikiliza Lema CHADEMA mmekwisha

Yeye ni mjumbe wa kamati kuu,alishawahi kuyasema hayo kwenye vikao halali vya Chama?
Why now?Katumwa na nani?
Lema kanunia one way ticket to his grave!Asahau kunyanyuka tena kisiasa kupitia upinzani!
Labda ahamie CCM rasmi na azawadiwe chochote!
 
Mkuu mbona kama amekatia tamaa siasa safi za kidemokrasia zinazofuta haki na rule of law

Leo IGP wa Kenya amesimamishwa mahakamani Kwa ishu Tena za raia wa kigeni mtanzania mwenzetu

Nchi yetu inahitaji mabadiliko makubwa ya kimfumo

Tukimpoteza Lisu itatuchukua miaka mingi sana Mungu kutupa mtu wa aina hiyo
 

..Kwenye suala la Maridhiano John Heche, na Tundu Lissu, wanakubaliana kimtazamo.

..Kama unabisha tuletee taarifa aliyotoa Wakili Kisabo ni nitadhibitisha kuwa msimamo wa Chadema, na Heche, ndio msimamo wa Tundu Lissu.

..Na Godbless Lema hajapingana na msimamo wa Chadema kuhusu maridhiano.

..Tundu Lissu kupitia Wakili Kisabo alisema yuko tayari kufanya maridhiano ikiwa huru, na chama kikiwa huru.

..Pia amesema anataka UCHUNGUZI HURU wa matukio ya OCT 29.

..Sharti lingine ambalo Tundu Lissu amelitaja ni hatua za UWAJIBIKAJI kwa waliohusika ikiwemo Msajili, Tume ya Uchaguzi, Polisi, ...

..Chadema wao hawakutaka Paul Kisabo atoe taarifa kubwa kama hiyo bila kukishirikisha CHAMA.

..Na walipothibitisha kwamba Mwenyekiti wao ametoa maelezo hayo huo ndio umekuwa msimamo wa chama.

..Sasa baada ya Tundu Lissu na Chadema kuweka mapendekezo yao mezani, Ccm na serikali walipaswa kuweka counter proposal, badala ya hizi kampeni za kumchafua John Heche.

Cc Nguruvi3
 
Unazunguka tu, ifike wakati tukubaliane na ukweli ccm kwa sasa haiko tayari na wala huwezi kuishinda kwa style ya winner takes all.

Kuna kitu tujifunze kwa Wazanzibar wale hatuwawezi na hatujawahi kufikia kuwa radical kama wao lakini imefika wakati wa kugawana nusu mkate mnaingia serikalini kwenye mifumo mnaweka mizizi ndio mnawatowa ccm huku wakiwa na uhakika wa nusu mkate.

Mama na Lisu picha zilikuwa zinaenda sana huyu ndiye alikuwa mtu wa kwenda naye kwa kupuliza kabka alijarudi shetani lingine kama Magufuli halitakagi suluhu.

Tunachokikosa kwa sasa ni chama kikuu cha upinzani kushindwa kuusoma mchezo, siasa za nginja nginha ccm ndio wanazipenda mtakumbana na Polisi huku wao wanaendelea kula na Polisi na wanajeshi.

Nadhani wote mmeona msiba wa Baba wa IGP ulikuwa Masaki, hivi ndivyo ccm inavyokula na watu muhimu kuendwlea kulindwa madarakani.
 

..kwa hapa tulipofika ni CCM ndio wanaopaswa kutia akili.

..jinsi wanavyoendelea kutumia Polisi kujisimika madarakani ndivyo wanavyozidi kujiharibia.

..wasipojifunza kwa makosa waliyoyafanya OCT 29 hawatajifunza kwa lolote na wataelekea shimoni.

..CCM wanapaswa kutambua hatari iliyoko mbele yao na kufanya maamuzi kwa busara kubwa.

..Kwa hapa nchi ilipo Chadema ndio wako kati ya wananchi na CCM.

..Wakiifuta Chadema wawe tayari kukabiliana moja kwa moja na wananchi hawa wa kizazi kipya.

..CCM wasijifariji kwamba kwasababu waliidhibiti Zanzibar basi wataweza kuidhibiti na Tanganyika.

..Tanganyika ni eneo kubwa sana. Zanzibar ni sawa na wilaya za Tanganyika.
 
Soft politics=Kulambishwa asali 🤣
 
Sisi ni nyumbu wala hatujali
chadema ikifa, tutasubiri nyumbu mkuu mwingine ajitokeze tumfuate
hakuna kupoa
 
Wananchi wepi unaowazungumzia hawa wanaompokea shujaa wao Jihan Airport?

Au mapambano yanayoongozwa na mademu Mange, Maria, Hilda wakiwa chumbani?
 
Sifa kubwa ya sauti ya shetani ni VITISHO..! this s the devil huhitaji maombi kufahamu
 
uzuri chadema yote password zipo na Jj mnyika akizingua mnyika chadema itaparanganyika sio dalali lema
 
Wananchi wepi unaowazungumzia hawa wanaompokea shujaa wao Jihan Airport?

Au mapambano yanayoongozwa na mademu Mange, Maria, Hilda wakiwa chumbani?

..watu wanaoweza kuongozwa na mademu kama Mange, na Maria, mimi nawaona ni hatari.

..fikiria Rais wa nchi ameshindwa ushawishi na Kina dada kama Mange mpaka akalazimika kuuwa wananchi wake kwa maelfu.
 
..watu wanaoweza kuongozwa na mademu kama Mange, na Maria, mimi nawaona ni hatari.

..fikiria Rais wa nchi ameshindwa ushawishi na Kina dada kama Mange mpaka akalazimika kuuwa wananchi wake kwa maelfu.
Na zaidi ya hapo imeshatokea! Oct 29. Nchi ikivimba inahitaji pa kutokea! ndicho kilichotokea kwa mabinti kuwaweka CCM mtu kati hadi leo wanahaha hawajui mwelekeo wa nchi
 
I.Mwenyekiti Tundu Lissu anataka maridhiano lakini Makamu wake Heche hataki maridhiano.Lema leo kaweka kila kitu wazi.

Mbona hili hitimisho lako ni kinyume na kauli za Lissu kwamba hakuna suala la maridhiano, anataka mahakama iamue kama ni KUNYONGWA au kuwa HURU
 
Lema rasmi matèka wa ccm
 
Pamoja na longo longo kuwa ni sehemu ya siasa, lakini hakuna kitu kizuri kama kuukubali ukweli wa hali halisi ya siasa zetu. Nilikuwa US, nikaona jinsi Trump alivyo mnock down Camala, nikawashauri Chadema

Pre GE2025 - Hata Kusipofanyika Reforms, 2025 CHADEMA Ina Fursa!, Ila They Are Just Too Blind to See!, Hawajitambui! No Election ni Utopia!. Wake Up!​

Sikuishia kuandika tuu humu jf, nikamkabili TL, nikamshauri
View: https://youtube.com/shorts/iv7asnge8Qo?si=obMHaDpCfE9Ous7k
P
 
CCM ndio wanaopaswa kutia akili.Ile press conference ya Lema imethibitisha kuwa ni kweli Lema ni Pandikizi.Lema ametumia “doublespeak/talk”kuongea ukweli kuwa yeye ni Pandikizi kwa wakati huo huo akijifanya Anakanusha.Ametumia hiyo style yake ya “doublespeak” kufanya kazi ya CCM kuisambaratisha Chadema na kutoa Siri za hata jinsi CCM wanavyomtumia kwenye Balozi mbali mbali wakati huo huo yeye align himself na CCM.Anamalizia kazi ya kumsbaratosha Heche ambaye CCM tayari wamefanya hiyo Kazi kuanzia kwenye ile public show trial Heche alipopanda Kizimbani wakaja na zile ambush na evidence zao,yeye Ana cement kwa kusema Heche is not all that,Mimi ndio nilisaidia,Mara Mimi nilitakiwa yada yada nyingi,bila kuchelewa CCM wakiongozwa na Kitila pamoja Media za CCM wanaumgana na Lema kumalizia kazi kuwa CCM ndio chama pekee,Chadema iko weak mara haina uhuru.Lema ni Pandikizi na yuko na wenzake,k Chadema ichukue hatua na kujipanga vizuri,ikitokea Heche anafungwa na Lisu kufungwa,lazima Chadema ijipange kisawasawa.CCM imeshindwa ku erode trust ya Public kwa baadhi ya Wanaharakati hasa Mange.Maria na Hilda wakinadilika na kuwa makini na habari wanazotumiwa,kuacha kuendekeza umbea wanaoletewa mfano issue sijui Jk anaumwa au Samia anaumwa na Mapandikizi ya CCM ambayo yanajifanya ni watu wao wa karibu ili kutaka kuwaaminisha Umma kuwa wao ni waongo na Wazushi Basi hawa Mabinti watazidi kuitia karaha CCM.Agenda ya Wanaharakati ni Agenda ya CHadema ya Lisu na Heche,mabadiliko ya Mfumo Binafsi sioni tatizo Lao.Tatizo la Chadema ya Lisu na Heche ni watu wanaopingana na agenda za Chama..
 
Wananchi wepi unaowazungumzia hawa wanaompokea shujaa wao Jihan Airport?

Au mapambano yanayoongozwa na mademu Mange, Maria, Hilda wakiwa chumbani?
Hao hao ndo walifanya 29 Oct mfumo wa siasa ubadirike and why issue ya jihan na mange au wakina maria ndo iwe kipimo cha siasa hata nchi ikibadirika vp hawawez wananchi wote kuongea lugha moja lipo wazi ila kundi kubwa na muhimu likijua wajibu wao ni ushindi tosha kwa nchii kama hukuwa field 29 Oct kuona mitazamo ya vijana au kufanya research yakinifu huwezi kuelewa nin ccm inajipalilia makaa sijawahi shiriki jambo lolote chadema na asili yangu ni ccm ila tulipo tunapaswa tujisahihishe hali ni mbaya narudia tena hali ni mbaya huko juu huenda wanajua ukweli halisi au wanadanganywa
 
Mh. Lisu aliweka misimamo wake waziwazi.
Anachofanya Lema walifanya akina Tip tip wakishirikiana na machifu kuwauza waafrika wenzao.

Wazee walidhani vijana wakisoma watalikomboa taifa, matokeo yake wameliuza kuliko hata akina Nangungo wa Msovero.

Ni laana taifa kuzaa watoto wanaoliuza mchana kweupe.
Dalali Lema si wa kwanza, walimtangulia Lyatonga Mrema, Ibrahim Lipumba, Zitto Kabwe, James Mbatia, .....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…