Mdau, unatumia muda gani kwenye matumizi ya AI kwa siku?

New Designer

JF-Expert Member
Joined
Aug 8, 2025
Posts
551
Reaction score
879
Mdau, unatumia muda gani kwenye matumizi ya AI kwa siku?

Kutokana na ukuaji mkubwa wa teknolojia, mitandao imekuwa sehemu muhimu ya kupata ushauri, habari, elimu, burudani pamoja na kujifunza mambo mbalimbali kwa haraka zaidi kuliko zamani. Leo watu wengi wanategemea teknolojia katika kazi, biashara, mawasiliano na hata kufanya maamuzi ya kila siku.

Mbali na hayo, teknolojia ya AI imeendelea kuwavutia watu wengi kutokana na uwezo wake wa kutatua matatizo mbalimbali kwenye jamii. AI inasaidia katika uthibitishaji wa taarifa, kutafuta habari kwa haraka mtandaoni, kusaidia masomo na tafiti, kutengeneza maudhui, kuboresha huduma za biashara pamoja na kurahisisha kazi zinazochukua muda mrefu kufanywa na binadamu.

Kadri matumizi yake yanavyozidi kuongezeka, AI imekuwa sehemu ya maisha ya kila siku kwa watu wengi duniani.

Je mdau, wewe unatumia teknolojia ya AI kwa muda gani au asilimia ngapi kwa siku?
Na mara nyingi unaitumia kufanya nini?
 
35%

Nje ya mada AI ya jf imepotelea wapi ?

na hivi kwa nini jf imekuwa na mtindo wa kuleta kitu kwa muda mfupi na kukipoteza kabisa ?
 
AI ni nzuri lakini ni muhimu na wewe ukatumia akili Yako ya ziada kuchambua kile ilichokupatia kwa sababu nayo inafanya makosa mengi tu.
 
AI ni nzuri lakini ni muhimu na wewe ukatumia akili Yako ya ziada kuchambua kile ilichokupatia kwa sababu nayo inafanya makosa mengi tu.
Thanks mkuu AI ipo kurahisisha mambo but akili yako ni muhimu
 
10 _15 %, inategemea siku hio umekuwa mtandaoni kwa muda gani na ulikuwa unafanya nini
 
Natumia mara nyingi,hata Sasa hivi nimetumia lakini ndo kama hivo Hadi wewe uiongoze
Aah hizo picha na video ni kwaajili ya biashara, elimu, au uandishi wa habari au kwaajili ya kupost tu
 
Hongera sana mkuu wangu mara ya mwisho ku Generate picha and video ilikuwa lini na ulikuwa unatumia kwenye issue gani
Kwenye picha ilikua jana , hii picha niipiga jua likizama (machweo) nilitaka itoke bila background ya miti , ndio ikawa hivyo.
 
Iko vizuri Lakini Ina udhaifu asili ya muafrika haisemi ukweli ime base kwa mapebali
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…