Mkalukungone Mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 3,141
- 7,205
Mdau wa siasa na mkazi wa Dar es Salaam, Ramadhan Mashauri, amesema idadi kubwa ya watu wanaojitokeza kuchukua fomu za kugombea nafasi za uongozi, ikiwemo ubunge, inatokana na viongozi wengi wanaomaliza muda wao kushindwa kuzitendea haki nafasi zao wakati wa utumishi wao.
Ameeleza kuwa hali hiyo imeibua hamasa kwa wananchi wengi kutaka kuwania nafasi hizo ili kutafuta suluhisho la changamoto ambazo hazikutatuliwa na wabunge waliopo madarakani au waliomaliza muda wao.
Ramadhan ametoa maoni hayo leo, Julai 10, 2025, katika kipindi cha Mada Kuu kinachorushwa na TBC1, ambacho kilijadili mada inayohoji: “Kunani Bungeni!”