Mdee na wenzake wakiomba msamaha nashauri wasamehewe

Mdee na wenzake wakiomba msamaha nashauri wasamehewe

Na wakawe wabunge wa huko huko... huku chadema, wameishamaliza kulea kukuza.... waende sasa wakaolewe huko waendapo..

Maendeleo haya chama
Sio kweli mkuu, hakuna mbunge aliyejiunga tayari na CCM mpaka muda huu😀😀😀
 
Unajua au unatakiwa uwelewe ,watu hawasikitiki kwa kuondoka kwa yeyote yule,umeona eei, kinachowafanya watu ni kumuonea au kuwaonea huruma ,wale ambao walijijenga tena kwa muda mrefu na kufikia hatua ya juu kuaminiwa na wao bila ya shaka yeyote ile hilo wanalijua,ingawa hawakulitazama kwa kina.

Kama CCM iliwatongoza na kuwapa chochote au kuwaahidi na ndivyo inavyoonekana dili limetimia, si kwa kuwa inawapenda sana au inawaheshimu sana na kuwaona wana watu nyuma yao au tuseme wanayo sapoti kwa wananchi,

CCM inataka kuwaharibia tu,wangapi walivutwa na kuhadaiwa na CCM leo wapo wapi na hawa wanataka kugeuzwa magombe tu,watachungwa chungwa na mwisho wake muda wa kuonekana sasa hata wakirudi watakuwa hawana tena mvuto na mambo mengi yatakuwa yamewageuka na vigumu kukubalika.

Hapo na CCM wataanza kuwaepuka kwani imani zao ni za kinafiki,CCM hawawezi kuamini viruka njia hata siku moja.
 
Huongei lolote kuhusu "ubunge wao" as if nothing has happened. Habari yote inayofanya watu wawazungumze hawa watu ni kuhusiana na issue ya ubunge. Chama chao kimeweka msimamo juu ya kutotambua matokeo ya uchaguzi mkuu na hivyo kutokua tayari kupeleka majina, sasa huoni unapoleta mapendekezo ya msamaha unatakiwa pia kuongelea hatima ya huu ubunge??

Weka wazi kwenye ushauri wako kama, waombe msamaha na kuruhusiwa kuendelea na ubunge wao au waombe msamaha na kuukana ubunge wao na waendelee na maisha ndani ya chama kama kawaida. Ili watoa maoni wapime uzito wa msamaha katika mktadha huo, siyo tu kuleta hoja ya msamaha na watu watoe maoni bila kukujua unapenda msamaha upi.
 
Nashukuru mkuu, tayari chama kilitangaza hakitambui matokeo ya uchaguzi, hivyo suala la ubunge halipo automatically kwa muktadha huo.
 
Hakuna kitu Kama hichi, nyepesinyepesi zinasema halima kashauriwa na ndugu zake atulie kwanza na ikiwezekana akaombe msamaha chadema.ni za mtaani
Kumbe hata ndugu zake wameona kwamba amekosea? Akiomba msamaha ajitoe na ubunge maana ndicho kinachosababisha ashauriwe kuomba msamaha. Amewatumbukiza wenzake shimoni, sasa sijui kama katika hilo atafanikiwa kuwatoa wenzake kama yeye akisamehewa.

Ingawa nafasi ya kusamehewa kurudi ni ndogo kwa sababu ya kiapo cha Ubunge ambapo CCM watalazimisha ubunge uendelee. CHADEMA wawe makini maana CCM wanaweza kuwatuma wakaombe huo msamaha halafu wao kupitia Ndugai wakang'ang'ana ubunge haufutwi.
 
Back
Top Bottom