Wadau mada ni nzuri nataka nitoe mchango wangu ,mimi kutokea kwenye bible navyotambua kutokea kitabu cha ufunuo , kuna mwisho wa ulimwengu huu lazima ufikie na binadamu naye ana mwisho pia wa kuishi hapa dunia ,twende kwenye mwisho wa ulimwengu hapo lazima nielezee kiufupi ili watu waelewe,kuna vitu ambavyo vimeandikwa kwenye biblia lazima vitokee ndipo ulimwengu huu ndo utakuwa unaelekea mwisho mfano kuna jambo linaitwa kukua kwa maarifa kwa binadamu ,ndo kwanza yapata miaka 2000 iliyopita toka yesu kristo azaliwe ,tukisema maarifa ni uwezo wa akili wa binadamu ambao utakua mkubwa sana binadamu atakuwa na uwezo wa kubuni vitu mbalimbali mfano wajukuu zetu na Watoto wetu watakuja kuona magari yanayoendeshwa na kopyuta bila mtu kuwa ndani kwa ajili ya kusafirisha malighafi,kuna mwanasaikolojia mmoja alisema huenda ulimwengu ukafikia miaka bilioni 1.5 ndo itakuwa inafikia ukingoni ,mimi kwa namna flani ninaweza kuamini hebu fikiria wanasayansi wa marekani na china wamefanya utafiti na kupeleka kifaa cha kuchukua sample ya udongo sayari ya mars kujua mama binadamu anaweza kuishi ,inamaana dunia itajaa na sayari mars itajaa ,na hapo tukienda kwenye vitabu vitakatifu kuna mambo yatakuwa yanatokea kama yalivyotabiliwa kuhusu mwisho wa ulimwengu mfano vita ,kwenye vita hapo hizi silaha za maangamizi Yaani nyuklia kipindi hicho litakuwa jambo la kawaida sana kutumiwa pata picha huo ulimwengu utakuaje ,sasa hivi jumuia za kimataifa zinavyopiga kelele kuhusu utengenezaji wa silaha za nyuklia wanajua madhara yake,hivyo hayo ni machache kuhusu mwisho wa ulimwengu huu "hivyo tambua ulimwengu lazima ufikie mwisho "