Mdogo wa mke wangu (binti) amenidharau na kunitukana mbele ya mke wangu

Mdogo wa mke wangu (binti) amenidharau na kunitukana mbele ya mke wangu

Kwaza hao wakurya gani kwetu ukuryani baba mkemwe huwa hatakiwi kuishi kwa binti yake labda kwa kijana wake wa kiume ,Na kama ikitoke iwe kwa sababu maalumu labda ugonjwa ili awe karibu na huduma za hospitali.Ushauri wangu timua binti na dada mtu akizingua mrudishe kwao kwa muda akajifunze .
Ata mimi nimeshangaa Mzee wa kikurya akakae kwa mtoto wake wakike na Wazee wakikurya hawana njaa njaa sanaa kufikia kwenda kuishi kwa mtoto wake wakike.
 
Ondoka mwachie nyumba akae na Baba yake. Siku akiondoka Baba yake rudi nyumbani. Huyo mwanamke anza kuishi naye kitaalamu.
 
Wakuu naomba ushauri.

Mimi ni mkazi wa Morogoro ninaishi kwenye nyumba yangu niliyotafuta pamoja na mke wangu. Baada ya wahitimu kumaliza chuo mwaka huu mke wangu aliniomba mdogo wake aje kuishi nasi pamoja.

Sasa baada ya kipindi kupita mke wangu ameonesha ukaribu sana na mdogo wake ikafika mpaka kumueleza mengi juu ya maisha yetu ndani.

Kisa
Jana nilienda dukan kwetu na mke wangu (duka la vipodozi), lengo kumfuata shemeji na kupiga hesabu na kufunga duka. Dakika chache mke wangu alipokea simu kutoka kwa baba yake mazazi akimuomba aje aishi nyumbani kwangu.

Walikubaliana wao yeye na baba yake mzazi akiwa na mdogo wake na hata akaamua kumtumia nauli bila ya mimi kuhusishwa chochote. Ikumbukwe yote haya yanafanyika dukani tukiwa wote watatu namaanisha mimi, mke wangu na shemeji. Baada ya hili zoezi kuisha ndipo mke wangu ananieleza kuwa "Baba atakuja kesho na nimeshamtumia na nauli"

Mi nikamjibu kwa njia ya ujumbe wa simu, "Unaniambia ama unanipa taarifa?" Baada ya hii kauli alinuna na kukasirika sana na kuamua kuongea Kikurya yeye na mdogo wake (mimi mchaga). Mimi hapo sielewi kitu ila nyuso zao ni kama wamefura kwa hasira.

Dada mtu aliamua kurudi nyumbani kwa pikipiki, mdogo mtu (shemeji) alibaki dukani na kufunga hesabu. Baada ya muda kidogo niliwasha gari na kuelekea nyumbani. Nilipofika nyumbani sasa nikamuuliza mke wangu kwanini umekasirika kwa ujumbe kama ule angali sijaandika tusi?

Ailinijibu we niache kwanza, ushamzika baba yako hivyo huna cha kupoteza. Mimi nikamwambia taswira kama hiyo unanijengea picha mbaya kwa mdogo wako, maana yanayoongeleka ni mengi sana hasa juu ya mimi na wewe.

Maana unayomueleza nduguyo huwaeleza hata watu wa karibu. Dah, baada ya kusema hivyo akampigia simu mdogo wake na kumwambia shemeji yako anasema wewe huwa una muongelea vibaya hapo dukani kwa watu wake wakaribu.

Alifunga duka na akarudi nyumbani spidi ya jeti na kunikuta sebulen nimekaa naperuzi JF. Kwanza alipofika tuu nyumbani aligonga mlango kwa nguvu sana kana kwamba kuna mtu ana tuvamia. Alipotimba sebulen akaanza kwa kusema ilikuwaje mkanizungumzia mimi na hao marafiki (majirani wa dukani) zako?

"Halafu shemeji unajua wewe ni mnafiki sana? Unadhani matendo yako kwa dada siyaoni humu ndani? Ujue shemeji wewe una roho mbaya sana, naishi na wewe kwa kukuvumilia sana?Nlisha kudharau sana.

He he..he! Nlibaki nashangaa sana, kwanza ni mtoto mdogo sana kwangu, ni wa mwaka 98. Mwisho akasema bhana eeh kama vipi andika talaka kwa mkeo mgawane mlivyo chuma kila mtu asepe zake (shemeji huyo)! Hata dada yake hakuwahi kutamka maneno kama haya asee.

Wakuu, mimi nimeamua asepe kwao ifikapo Jumatatu ya tarehe 17, October. Japo mke anakuwa kama anajiuliza sana haya maamuzi yangu.

Pia msaada tafadhali maana nina mawazo sana kuhusu huyu dogo mwenye Degree ya Biashara, halafu pia ndugu lakini sina namna.

Nawasilisha.
Pole sana mkuu. Nimekusoma mstari kwa mstari lakini nadhani kuna kitu unaficha baina yako na huyo shemeji yako. Hujawahi kuwa karibu naye kiasi cha kutatanisha au kumu approach? Ktk hali ya kawaida, shemeji yako (tena mwenye umri mdogo) hawezi akaanza kukubwatukia namna hii bila sababu yoyote. Naomba ufuguke vizuri ili nikushauri.
 
Pole sana mkuu. Nimekusoma mstari kwa mstari lakini nadhani kuna kitu unaficha baina yako na huyo shemeji yako. Hujawahi kuwa karibu naye kiasi cha kutatanisha au kumu approach? Ktk hali ya kawaida, shemeji yako (tena mwenye umri mdogo) hawezi akaanza kukubwatukia namna hii bila sababu yoyote. Naomba ufuguke vizuri ili nikushauri.
Ni kweli haiwezekani ghafla tu shemeji yake amtukane, inawezekana na yeye anatabia za uchuyo maana wachaga wanatabia za Uchoyo uchoyo
 
Mwanamke huyo itakuwa ndo master mind wako TOFAUTI na hapo unabidi umpe divorce 3 na mkongoto mkalia ili atembelee magoti
 
Mkuu,kwanza pole sana. Pili, jitahidi kuwa MWANAUME, sijui unanielewa? Yani chukua hatua/uamuzi wa kiume katika situations kama hizo.

Tatu,hayo alosema huyo binti ndio haswaa mipango waipangayo na dada yake. Jambo la kufanya ,kaa nao kwa makini sana, wanaweza hata kukupoteza kwa namna yoyote ile kwasababu inaonesha MALI wamaeiweka mbele. Na hii ni kupitia kauli za huyo shemeji yako.

Kama ni mimi ningetimua wote siku hiyo hiyo, hao washaingia virus,mpango wao si mzuri kwako.
 
Familia nzima kuanzia baba mkwe, mke na huyo shemeji wape likizo kwa muda alafu itisha kikao cha familia alafu ongea kama mwanaume na uweke terms zako za uendeshaji wa nyumba na biashara.

Fanya hivo lasihiyo tutakupoteza mwamba
 
Piga makofi hao akina bhoke , hao lugha wanayoielewa ni violence Tu
 
Wewe mwenyewe shida
Shemeji zako shida
Mke wako shida
Na hata wazazi wa mke wako shida
Sasa hatujui kwa upande wa kwenu kukojo


Naweza kusema wewe ni shida tu zimekuzunguka
 
Pia, huenda hata wewe una tatizo mahala mpaka inafikia hatua mtoto wa 1998 anakudharau. Huo ujasiri wa kumdharau mtu aliemzidi umri tena mume wa Dada yake, ambae wakati huo yuko kwake(kwako) ,anakula chakula cheke(chako),n.k.

Tueleze mkuu,shida yako ni ipi? Au ulimtaka? Au mkeo kamwambia kwamba una nyumba ndogo na michepuko kibao?

Kama hakuna tatizo ila anakuletea tu jeuri nakushauri ufanye uwezalo ili wote wajikute wako MOI.
 
1. Hakikisha unaifilisi hiyo biashara iishe
2. Toa talaka mgawane mali uanze upya. Maana mke bado hajawa na akili ya kuolewa bado ana akili ya kuishi kwa baba na mama
 
Back
Top Bottom