Mdogo wangu Ibrahim Ajib ' Mido ' kama hii taarifa ni ya kweli basi japo ni mwana Simba SC mwenzio ila ' umeniangusha ' sana na mno

Mpaka umekuja hivi nina uhakika kuwa tayari ' Dozi ' ya Awali niliyokupa ' imeshapenya ' kabisa. Pole sana na Siku zingine uache ' Kukurupuka ' Swine Mkubwa Wewe.
Hakuna dozi wala nini. Wewe ni mbuzi tu huna issue....mammae we.
 
Kwenye hii ishu Ajib anaweza akawa sahihi... Maana kwa usajiri wa bongo mchezaji akiwa huru anapewa na hela ya usajiri ili akachezee timu flani ambapo icho kitu akipo kwa nchi zengine au soka la ulaya Sasa itakua Mazembe walivyoona mchezaji huru wakataka wajadiliane maslahi binafsi tuu,bila kumlipa hela ya usajiri ambapo kibongo bongo tumezoea kutoa na hiyo pesa
 
Kweli mkuu. Mama yao kina saluraka alikuaga teacher. Na hawa jamaa kina saluraka wapo vizuri kimaisha. Sis tulishangaa sana saluraka alivyong'ang'ania kwenda ulaya wakati hapa kwao mambo safi. Mpaka ule usiku ambao kesho yake ndio anasafiri tulikuwa nae maskani mkuu huyu jamaa.
 
Manara ndio mshauri mkuu wa Ajibu mnategemea nini zaidi ya kumjaza upuuzi tu.
 
Agib mtoto wa ilala huyo
 
Mimi ninahisi (sina uhakika sana) kwamba Simba ilimpa mkataba wa awali kijana Ajibu, na kisha baadaye TP Mazembe wakatuma barua Yanga kuomba wamruhusu Ajibu aende akaingie mkataba wa awali nao. Sasa kama ni kweli ameonekana kwa viongozi wa Simba, basi itakuwa anataka EITHER aondoe makubaliano hayo ya awali na Simba AU anataka kuinufaisha Simba iwe kama inamuuza TP Mazembe. Hilo la kuitosa TP Mazembe sababu ya Simba sidhani kama lipo
 

Uko sahihi sana / mno Mkuu kwani hata Mimi huyo Mama yao ' Mwalimu ' alinifundisha japo Yeye alikuwa ni Mwalimu hapo Uhuru Mchanganyiko. Familia yao ni ' Family Friend ' na Familia yetu na Mimi hapo Kwao Ilala Bungoni Kituoni kabisa ni kama vile Nyumbani tu kwani naenda muda wowote ule na hata nikiamua Kulala pia nalala vile vile. Hao ' Wapare ' wako njema na hawana shida Kimaisha.

Tukirudi kwa ' Dogo ' Ajib kiukweli ' amenizingua ' mno kwani huku Simba SC kama ni kweli anakuja basi anakuja Kukimaliza kabisa ' Kipaji ' chake. Mkuu kwa Kipaji chake na Uwezo wake mkubwa Uwanjani Ibrahim Ajib sasa hivi siyo Mchezaji wa kuendelea Kubaki Kucheza Timu zetu hizi Kubwa mbili za Simba na Yanga bali anatakiwa sasa awe zake huko mbele ili nae tuwe tunamuona na Kujivunia nae kama ilivyo kwa Mbwana Samatta ' Popa ' a.k.a Samagoal.
 
Ajib tatizo anapenda sifa. Huku ilala huwaga anasumbua sana na kigari chake kile akipita mziki mkubwa japo anakaa tabata. Sasa zile sifa anazopewa ilala bungoni pale na boom fc ndio anaona kamaliza. Ila naskia kuna yule dogo ndugu yake 'teja' alikuwa na kipaji kuliko hata ajibu. Huyu dogo aliendaga uarabuni lakini naona ameshindwa kukaa akaamua kurudi bongo
 
Ilala na Kariako zinalemaza
 

Mkuu sidhani kama kuwa na Gari hapa Tanzania ni tatizo japo Mimi sina mpaka leo. Nadhani tatizo la Ajib siyo huko Kuringa Kwake na hayo Majivuno yake ya sasa bali anza Kwanza kuangalia Makuzi yake. Huyo Mtoto ( Dogo ) amekulia Maisha ya taabu na dhiki mno na kama siyo huyo Mwalimu Mama yao akina Hemed na SaluRaka kumchukua na kuamua Kumlea hapo hapo Kwake Ilala Bungoni basi huenda hata leo hii Ajib angekuwa ni Bonge la ama Teja kama Kaka zake wote au Bonge la Kibaka kama siyo Jambazi pia.

Anachohitaji sasa hivi Ibrahim Ajib ni Kushauriwa tu mambo mema na Watu wenye Mapenzi mema nae ila tukianza Kumsema / Kumnanga kuwa sijui Siku hizi anaringa kwakuwa ana Hela na ni Mtu Maarufu wala haitotusaidia mno sana sana tutaonekana tunamuonea tu Wivu. Mbona Mimi pamoja na kwamba nimemzidi Elimu na mambo mengi tu lakini katika Suala la Hela na Maendeleo yake ameniacha mbali mno na wala siwezi nikampata au nikamfikia leo wala Kesho ila Simchukii au Simuonei Wivu na sana sana kila nikionana nae huwa namshauri mambo mengi na vitu vingi?

Kinachoniumiza zaidi Kwake ni kwamba huyu ' Dogo ' ana Kipaji cha Ajabu sana ambacho kama angeenda huko TP Mazembe basi wangempika zaidi, angecheza Mechi nyingi Kubwa na za Kimataifa ambazo nina uhakika kwa aina ya Uchezaji wake basi ama Vilabu vikubwa vya Uarabuni au Ulaya vingemuona na Kumchukua kwa Pesa / Hela ndefu mno kuliko hiyo Tsh Milioni 80 na Gari mpya aliyoahidiwa hapo Simba SC kwa Mkataba wa miaka miwili ambayo nimedokezwa kuwa ndiyo aliyowekewa Mezani tokea Siku nyingi tu.

Tumtie Moyo, tumshauri na kamwe tusimuonee Wivu / Kijicho kwakuwa tu ametuzidi wengi Wetu Maendeleo na Kimaisha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…