Mdogo wangu Ibrahim Ajib ' Mido ' kama hii taarifa ni ya kweli basi japo ni mwana Simba SC mwenzio ila ' umeniangusha ' sana na mno

Mdogo wangu Ibrahim Ajib ' Mido ' kama hii taarifa ni ya kweli basi japo ni mwana Simba SC mwenzio ila ' umeniangusha ' sana na mno

Mpaka umekuja hivi nina uhakika kuwa tayari ' Dozi ' ya Awali niliyokupa ' imeshapenya ' kabisa. Pole sana na Siku zingine uache ' Kukurupuka ' Swine Mkubwa Wewe.
Hakuna dozi wala nini. Wewe ni mbuzi tu huna issue....mammae we.
 
Kwenye hii ishu Ajib anaweza akawa sahihi... Maana kwa usajiri wa bongo mchezaji akiwa huru anapewa na hela ya usajiri ili akachezee timu flani ambapo icho kitu akipo kwa nchi zengine au soka la ulaya Sasa itakua Mazembe walivyoona mchezaji huru wakataka wajadiliane maslahi binafsi tuu,bila kumlipa hela ya usajiri ambapo kibongo bongo tumezoea kutoa na hiyo pesa
 
GENTAMYCINE ni zaidi ya Umjuavyo Mkuu. Mama yao akina Hemed na SaluRaka ndiyo alimlea mno Ibrahim Ajib wakati akiwa Mdogo na anahangaika na Maisha Magumu ( huku Kaka zake wote wakiwa ni Mateja watupu Ilala ) hasa baada ya Baba yake Ibra na Mama yake Kuachana na Mama yake Ibrahim akaamua Kutokomoea zake Uarabuni Kufanya Kazi huko ambako sasa ni mwaka wa 20 yupo huko Kimakazi.

Wakati Wewe ukidhani kuwa Ibrahim Ajib anajua mno Mpira basi unaambiwa hakuna Mtu aliyekuwa ana Kipaji cha Mpira kama huyo SaluRaka na Simba SC kupitia KD ( Kassim Dewji ) walihagaika sana Kumsajili achezee Simba SC ila alikataa kwakuwa Yeye Mpira hachezei Shida kwani anatoka Familia hiyo ya akina Hemed inayojiweza kiasi Kiuchumi na sasa yupo zake huko nchini Ujerumani ambapo amejilipua ( namaanisha amechukua Uraia rasmi wa huko )

Naomba nisiendelee zaidi ya hapa tafadhali.
Kweli mkuu. Mama yao kina saluraka alikuaga teacher. Na hawa jamaa kina saluraka wapo vizuri kimaisha. Sis tulishangaa sana saluraka alivyong'ang'ania kwenda ulaya wakati hapa kwao mambo safi. Mpaka ule usiku ambao kesho yake ndio anasafiri tulikuwa nae maskani mkuu huyu jamaa.
 
Genter...ukuje huku
tapatalk_1558467247081.jpeg
 
Manara ndio mshauri mkuu wa Ajibu mnategemea nini zaidi ya kumjaza upuuzi tu.
 
Unakuja Simba SC mdogo wangu hapo utapata Namba ya nani? Kwanini hupendi kusikia Mawazo ya Kaka zako ambao tunakupenda Ibra? Hivi kweli kwa Mfumo wa Kocha Aussems Wewe utapata Namba kweli ndani ya Kikosi cha Simba hii ya sasa Ibra? Ni kwanini Maisha ya hapa Dar es Salaama yanakulevya na yanakuridhisha hivi Mdogo wangu Ibra? Najua kuwa umeshawishiwa na Rafiki zako wakubwa akina Mkude, Ndemla na Tshabalala ila nawe pia ulipashwa ujitathmini Kwanza kabla ya Kuamua ulichoamua Ibra.

Mimi GENTAMYCINE ni Kaka yako, Rafiki yako mzuri tu tena tokea ukiwa Boom FC na wakati ukicheza pia pale Uwanja wa Shule ya Msimbazi achilia mbali Uwanja wa Barafu, ule wa Tanganyika Packers na hata pale Biafra ukiwa na ' Washikaji ' zako akina Mkude na Sure Boy wa Azam na unajua fika kuwa Mimi ni mwana Simba SC lia lia ila nilikushauri kuwa usije Simba SC na kukupa Sababu zangu nyingi ila kuna Mtu wako wa karibu yupo TRA Makao Makuu ' amenitonya ' kuwa jana ulikuwa na Viongozi wa Simba na huenda ndani ya Saa 48 au 72 kutoka sasa ukasaini rasmi Simba SC.

Nilikushauri vizuri sana Mdogo wangu Ibra kuwa kwa Mafanikio yako makubwa ya Kimpira ni vyema ukaondoka kabisa Tanzania hii ili ' ukatengenezwe ' zaidi na Makocha wakubwa wa Timu zingine na nakumbuka ulipopata ' Offer ' ya TP Mazembe nilifurahi mno na kujua kuwa usingeiacha hiyo bahati na kwa masikitiko makubwa sana nikaja kuambiwa kuwa ' umewachomolea ' kwakuwa tu Simba SC wanakuhitaji na Wewe umekubali kabisa kuingia ' Mtegoni ' na unaelekea Kusaini nao.

Ibra Mdogo wako kutoka Ilala Bungoni najua kuwa umeangalia Pesa na Maisha mazuri ya hapa Jijin Dar es Salaam hasa ukizingatia kuwa unapenda sana Starehe ila ipo Siku utakuja Kunikumbuka Mimi Kaka yako GENTAMYCINE na naamini hata Rafiki yako mkubwa SaluRaka ambaye sasa yupo nchini Ujerumani ( baada ya Kujilipua / Kuchukua Uraia wa huko kama Mkimbizi ) nae akisikia kuwa umekataa kwenda TP Mazembe atakushangaa achilia mbali Kaka yake Hemed wa TRA ambaye ndiyo Mshauri wako Mkuu najua nae pia atakuwa amesikitika mno tu.

Hivi Ibra ungevumilia tu uende zako TP Mazembe ukapikwe na ukatengenezwe hata kwa miaka yako miwili na ukomae vyema unataka kuniambia na Wewe Vilabu vikubwa vya Ulaya visingekuona na Kukusajili? Ibra ni mara ngapi Mwenzako Mbwana Samatta amekuwa akikuambia Wewe na Rafiki yako Mkude kuwa mnachelewa hapa Tanzania na kwamba nyie ni wa Ulaya tu? Hivi hamuoni Mafanikio yake huko KRC Genk?

Najua mida ya baadae tunaweza Kukutana maeneo ya Morocco Hotel katika Duka za Mke wa Mchezaji mwenzako wa Yanga Beki Gadiel Michael ambako huwa unapenda kuwa hapo ukiwa na Wachezaji wenzako bila Kumsahau Beki Mtukutu na Kaka yako Kelvin Yondan ila nimelazimika Kuja na hii ' Kitu ' hapa ili kuwa ' Funzo ' kwa Wachezaji wengine kuwa achaneni na mawazo ' Finyu ' kuwa Maendeleo ya Mchezaji basi ni lazima tu achezee Klabu za Simba na Yanga wakati kumbe ukweli siyo huo.

Nina uhakika kuwa kwa hili Bandiko langu kuna wana Simba SC Wenzangu watanikasirikia kama siyo kuninunia kwakuwa sijapendelea Ibra kuja Simba SC yetu ila ' Kiufundi ' kabisa na ninavyomjua Ibrahim Ajibu alivyo na Kocha wetu wa Simba SC hatoweza kupata Nafasi ya Kudumu Kikosini na atasubiri mno kwa akina Chama, Niyonzima, Muzamiri na hata Ndemla ila kwa Maendeleo yake ya Kimpira angeenda Azam FC angepata Namba tena ya Kudumu ila angeenda huko TP Mazembe au hata Ulaya angefanya vyema zaidi.

Nimefurahi tu Kusikia kwamba Simba SC inamrudisha Beki wetu wa Vijana William Lucien ' Gallas ' ili aje acheze Namba yake ya Kiasili Beki Namba Mbili kwani si uwongo sikufurahishwa na Usajili wa Beki wa ' hovyo hovyo ' ambaye Kiwango chake Kimeshuka kama si Kupotea ghafla Zana Coulibaly na nasikia kuwa anaachwa rasmi ili Nafasi hiyo ya Beki Namba Mbili ibaki tu kwa Nicolas Gyan, William Lucien na Majeruhi Shomary Kapombe.

Mdogo wangu Ibrahim Ajib umeniangusha sana Kaka yako Mimi GENTAMYCINE ila nayaheshimu pia Maamuzi yako.

Nawasilisha.
Agib mtoto wa ilala huyo
 
Mimi ninahisi (sina uhakika sana) kwamba Simba ilimpa mkataba wa awali kijana Ajibu, na kisha baadaye TP Mazembe wakatuma barua Yanga kuomba wamruhusu Ajibu aende akaingie mkataba wa awali nao. Sasa kama ni kweli ameonekana kwa viongozi wa Simba, basi itakuwa anataka EITHER aondoe makubaliano hayo ya awali na Simba AU anataka kuinufaisha Simba iwe kama inamuuza TP Mazembe. Hilo la kuitosa TP Mazembe sababu ya Simba sidhani kama lipo
 
Kweli mkuu. Mama yao kina saluraka alikuaga teacher. Na hawa jamaa kina saluraka wapo vizuri kimaisha. Sis tulishangaa sana saluraka alivyong'ang'ania kwenda ulaya wakati hapa kwao mambo safi. Mpaka ule usiku ambao kesho yake ndio anasafiri tulikuwa nae maskani mkuu huyu jamaa.

Uko sahihi sana / mno Mkuu kwani hata Mimi huyo Mama yao ' Mwalimu ' alinifundisha japo Yeye alikuwa ni Mwalimu hapo Uhuru Mchanganyiko. Familia yao ni ' Family Friend ' na Familia yetu na Mimi hapo Kwao Ilala Bungoni Kituoni kabisa ni kama vile Nyumbani tu kwani naenda muda wowote ule na hata nikiamua Kulala pia nalala vile vile. Hao ' Wapare ' wako njema na hawana shida Kimaisha.

Tukirudi kwa ' Dogo ' Ajib kiukweli ' amenizingua ' mno kwani huku Simba SC kama ni kweli anakuja basi anakuja Kukimaliza kabisa ' Kipaji ' chake. Mkuu kwa Kipaji chake na Uwezo wake mkubwa Uwanjani Ibrahim Ajib sasa hivi siyo Mchezaji wa kuendelea Kubaki Kucheza Timu zetu hizi Kubwa mbili za Simba na Yanga bali anatakiwa sasa awe zake huko mbele ili nae tuwe tunamuona na Kujivunia nae kama ilivyo kwa Mbwana Samatta ' Popa ' a.k.a Samagoal.
 
Ajib tatizo anapenda sifa. Huku ilala huwaga anasumbua sana na kigari chake kile akipita mziki mkubwa japo anakaa tabata. Sasa zile sifa anazopewa ilala bungoni pale na boom fc ndio anaona kamaliza. Ila naskia kuna yule dogo ndugu yake 'teja' alikuwa na kipaji kuliko hata ajibu. Huyu dogo aliendaga uarabuni lakini naona ameshindwa kukaa akaamua kurudi bongo
 
Ilala na Kariako zinalemaza
 
Mkuu sidhani kama kuwa na Gari hapa Tanzania ni tatizo japo Mimi sina mpaka leo. Nadhani tatizo la Ajib siyo huko Kuringa Kwake na hayo Majivuno yake ya sasa bali anza Kwanza kuangalia Makuzi yake. Huyo Mtoto ( Dogo ) amekulia Maisha ya taabu na dhiki mno na kama siyo huyo Mwalimu Mama yao akina Hemed na SaluRaka kumchukua na kuamua Kumlea hapo hapo Kwake Ilala Bungoni basi huenda hata leo hii Ajib angekuwa ni Bonge la ama Teja kama Kaka zake wote au Bonge la Kibaka kama siyo Jambazi pia.

Anachohitaji sasa hivi Ibrahim Ajib ni Kushauriwa tu mambo mema na Watu wenye Mapenzi mema nae ila tukianza Kumsema / Kumnanga kuwa sijui Siku hizi anaringa kwakuwa ana Hela na ni Mtu Maarufu wala haitotusaidia mno sana sana tutaonekana tunamuonea tu Wivu. Mbona Mimi pamoja na kwamba nimemzidi Elimu na mambo mengi tu lakini katika Suala la Hela na Maendeleo yake ameniacha mbali mno na wala siwezi nikampata au nikamfikia leo wala Kesho ila Simchukii au Simuonei Wivu na sana sana kila nikionana nae huwa namshauri mambo mengi na vitu vingi?

Kinachoniumiza zaidi Kwake ni kwamba huyu ' Dogo ' ana Kipaji cha Ajabu sana ambacho kama angeenda huko TP Mazembe basi wangempika zaidi, angecheza Mechi nyingi Kubwa na za Kimataifa ambazo nina uhakika kwa aina ya Uchezaji wake basi ama Vilabu vikubwa vya Uarabuni au Ulaya vingemuona na Kumchukua kwa Pesa / Hela ndefu mno kuliko hiyo Tsh Milioni 80 na Gari mpya aliyoahidiwa hapo Simba SC kwa Mkataba wa miaka miwili ambayo nimedokezwa kuwa ndiyo aliyowekewa Mezani tokea Siku nyingi tu.

Tumtie Moyo, tumshauri na kamwe tusimuonee Wivu / Kijicho kwakuwa tu ametuzidi wengi Wetu Maendeleo na Kimaisha.
 
Back
Top Bottom