Mdogo wangu Ibrahim Ajib ' Mido ' kama hii taarifa ni ya kweli basi japo ni mwana Simba SC mwenzio ila ' umeniangusha ' sana na mno

Mdogo wangu Ibrahim Ajib ' Mido ' kama hii taarifa ni ya kweli basi japo ni mwana Simba SC mwenzio ila ' umeniangusha ' sana na mno

Bandiko zuri ila kabla ya kuandika haya uliuona mkataba wa ajib aliopewa na mazembe????
Unakuja Simba SC mdogo wangu hapo utapata Namba ya nani? Kwanini hupendi kusikia Mawazo ya Kaka zako ambao tunakupenda Ibra? Hivi kweli kwa Mfumo wa Kocha Aussems Wewe utapata Namba kweli ndani ya Kikosi cha Simba hii ya sasa Ibra? Ni kwanini Maisha ya hapa Dar es Salaama yanakulevya na yanakuridhisha hivi Mdogo wangu Ibra? Najua kuwa umeshawishiwa na Rafiki zako wakubwa akina Mkude, Ndemla na Tshabalala ila nawe pia ulipaswa ujitathmini Kwanza kabla ya Kuamua ulichoamua Ibra.

Mimi GENTAMYCINE ni Kaka yako, Rafiki yako mzuri tu tena tokea ukiwa Boom FC na wakati ukicheza pia pale Uwanja wa Shule ya Msimbazi achilia mbali Uwanja wa Barafu, ule wa Tanganyika Packers Kawe na hata pale Biafra ukiwa na ' Washikaji ' zako akina Mkude na Sure Boy wa Azam na unajua fika kuwa Mimi ni mwana Simba SC lia lia ila nilikushauri kuwa usije Simba SC na kukupa Sababu zangu nyingi ila kuna Mtu wako wa karibu yupo TRA Makao Makuu ' amenitonya ' kuwa jana ulikuwa na Viongozi wa Simba na huenda ndani ya Saa 48 au 72 kutoka sasa ukasaini rasmi Simba SC.

Nilikushauri vizuri sana Mdogo wangu Ibra kuwa kwa Mafanikio yako makubwa ya Kimpira ni vyema ukaondoka kabisa Tanzania hii ili ' ukatengenezwe ' zaidi na Makocha wakubwa wa Timu zingine na nakumbuka ulipopata ' Offer ' ya TP Mazembe nilifurahi mno na kujua kuwa usingeiacha hiyo bahati na kwa masikitiko makubwa sana nikaja kuambiwa kuwa ' umewachomolea ' kwakuwa tu Simba SC wanakuhitaji na Wewe umekubali kabisa kuingia ' Mtegoni ' na unaelekea Kusaini nao.

Ibra Mdogo wako kutoka Ilala Bungoni najua kuwa umeangalia Pesa na Maisha mazuri ya hapa Jijin Dar es Salaam hasa ukizingatia kuwa unapenda sana Starehe ila ipo Siku utakuja Kunikumbuka Mimi Kaka yako GENTAMYCINE na naamini hata Rafiki yako mkubwa SaluRaka ambaye sasa yupo nchini Ujerumani ( baada ya Kujilipua / Kuchukua Uraia wa huko kama Mkimbizi ) nae akisikia kuwa umekataa kwenda TP Mazembe atakushangaa achilia mbali Kaka yake Hemed wa TRA ambaye ndiyo Mshauri wako Mkuu najua nae pia atakuwa amesikitika mno tu.

Hivi Ibra ungevumilia tu uende zako TP Mazembe ukapikwe na ukatengenezwe hata kwa miaka yako miwili na ukomae vyema unataka kuniambia na Wewe Vilabu vikubwa vya Ulaya visingekuona na Kukusajili? Ibra ni mara ngapi Mwenzako Mbwana Samatta amekuwa akikuambia Wewe na Rafiki yako Mkude kuwa mnachelewa hapa Tanzania na kwamba nyie ni wa Ulaya tu? Hivi hamuoni Mafanikio yake huko KRC Genk?

Najua mida ya baadae tunaweza Kukutana maeneo ya Morocco Hotel katika Duka za Mke wa Mchezaji mwenzako wa Yanga Beki Gadiel Michael ambako huwa unapenda kuwa hapo ukiwa na Wachezaji wenzako bila Kumsahau Beki Mtukutu na Kaka yako Kelvin Yondan ila nimelazimika Kuja na hii ' Kitu ' hapa ili kuwa ' Funzo ' kwa Wachezaji wengine kuwa achaneni na mawazo ' Finyu ' kuwa Maendeleo ya Mchezaji basi ni lazima tu achezee Klabu za Simba na Yanga wakati kumbe ukweli siyo huo.

Nina uhakika kuwa kwa hili Bandiko langu kuna wana Simba SC Wenzangu watanikasirikia kama siyo kuninunia kwakuwa sijapendelea Ibra kuja Simba SC yetu ila ' Kiufundi ' kabisa na ninavyomjua Ibrahim Ajibu alivyo na Kocha wetu wa Simba SC hatoweza kupata Nafasi ya Kudumu Kikosini na atasubiri mno kwa akina Chama, Niyonzima, Muzamiri na hata Ndemla ila kwa Maendeleo yake ya Kimpira angeenda Azam FC angepata Namba tena ya Kudumu ila angeenda huko TP Mazembe au hata Ulaya angefanya vyema zaidi.

Nimefurahi tu Kusikia kwamba Simba SC inamrudisha Beki wetu wa Vijana William Lucien ' Gallas ' ili aje acheze Namba yake ya Kiasili Beki Namba Mbili kwani si uwongo sikufurahishwa na Usajili wa Beki wa ' hovyo hovyo ' ambaye Kiwango chake Kimeshuka kama si Kupotea ghafla Zana Coulibaly na nasikia kuwa anaachwa rasmi ili Nafasi hiyo ya Beki Namba Mbili ibaki tu kwa Nicolas Gyan, William Lucien na Majeruhi Shomary Kapombe.

Mdogo wangu Ibrahim Ajib umeniangusha sana Kaka yako Mimi GENTAMYCINE ila nayaheshimu pia Maamuzi yako.

Nawasilisha.
 
Kama anapewa elf 20 aende tu kisa tp mazembe wakati unyamani anakula za kutosha nyie vipi
 
Wewe tumia misamiati yote ya kwenu shamba huko ila utawababaisha mambwisi wenzio mliokuja mjini Stand ikiwa Ubungo,unapewa story za vijiwen na wewe unakuja kujifanya unajua watu humu,Wewe Mshamba tu hata ujitutumue vipi humu watoto wa mjini wanajulikana character zao,Shukuru mjomba wako kukuleta mjini hapa ulishe ng'ombe wake

Umeshamaliza ' Kunyabeziwa ' kwa Siku ya leo au bado ' unaliendeleza ' tu hapo ulipo sasa na ' Wanyabezi ' wa Kutukuka?
 
Mkuu huyo magagafu atakuwa ni miongoni mwa wale Wagonjwa wa Akili waliotoroka Wodini Hospitalini Mirembe na wanasakwa hadi hivi sasa.
Pamoja na ushabiki wa hizi timu zetu za Kkoo,ila mchezaji wa kibongo akipata fursa nje huwa naona ni bora akaenda huko kuliko hapa home maana miyeyusho mingi
 
Huyo ajibu ni another type ya mrisho ngassa.
And haruna misho

Akili zao mgando sana wanadhani soka LA bongo litawatoa .

Wanapata chance za kutusua wanambwelambwela wataishia kusukuma brevis na crown wakati wenzako akina samatta wana sukuma mi range rover mijumba ya ukweli title kubwa na soon watua EPL wapige mpunga was maana .

Ajibu anawaza akienda mazembe yule mwajuma wa pale mtaani si atachapiwa .

Stupid Tanzanian player kanisikitisha sana

Samatta na ulimwengu wakati wanaenda mazembe sidhani kama walipewa dau nono sana ila anangalia saivi wako wapi ?

Mpira malengo
 
Huyo ajibu ni another type ya mrisho ngassa.
And haruna misho

Akili zao mgando sana wanadhani soka LA bongo litawatoa .

Wanapata chance za kutusua wanambwelambwela wataishia kusukuma brevis na crown wakati wenzako akina samatta wana sukuma mi range rover mijumba ya ukweli title kubwa na soon watua EPL wapige mpunga was maana .

Ajibu anawaza akienda mazembe yule mwajuma wa pale mtaani si atachapiwa .

Stupid Tanzanian player kanisikitisha sana

Samatta na ulimwengu wakati wanaenda mazembe sidhani kama walipewa dau nono sana ila anangalia saivi wako wapi ?

Mpira malengo

Nasikia wanaogopa kwenda nje ya Tanzania kucheza Soka na Kuwaacha ' Mademu ' zao huku Bongo halafu Bingwa wa Kupita na Wake za Wachezaji wa Kitanzania Mtoto wa Kitanga na ' Handsome boy ' Mchezaji Humud Gaucho atakuwa anapita nao ( anawatindua ) kama ambavyo imekuwa ndiyo kawaida yake.
 
Ajibu atakapokosa namba ya kudumu simba ndio atakapojuta

Tokea nikujue hapa JamiiForums sikuwahi kuona ukichangia jambo ' very constructive ' kama hivi. Mungu mkubwa kwa haya mabadiliko makubwa ninayoanza Kuyaona Kwako na bila shaka sasa tararibu nawe utaingia katika Kikosi cha ' Great Thinkers ' hapa Jamvini. Ila sijajua ni kwanini ' umeposti ' kitu hicho hicho mara Tano.
 
Back
Top Bottom