Mdogo wangu Msemaji wa Yanga SC Ally Kamwe naona unaanza vibaya na utapotea mapema

Mdogo wangu Msemaji wa Yanga SC Ally Kamwe naona unaanza vibaya na utapotea mapema

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
60,660
Reaction score
121,325
"Kesho nataka kwenda TFF Kumuombea Msamaha Haji Manara na naamini watanisikiliza na kumsamehe" Ally Kamwe Msemaji wa Yanga SC (Clouds FM Sports Extra).

*Waliyopanga watu wa kwenda kuigiza Filamu ya Royal Tour na Rais Samia walitakiwa wamjumuishe na Mchezaji bora Tanzania nzima tena akitokea Zanzibar atokako Rais Samia aitwae Feisal Salum Fei Toto ili awavutie zaidi Wazungu", Ally Kamwe Msemaji wa Yanga SC (Clouds FM Sports Extra).

Mdogo wangu Ally Shabaan Kamwe najua hivi sasa unahangaika na kujitahidi sana kutaka kulipa fadhila kwa mhamasishaji mkuu wa Yanga SC Haji Manara ambaye ndiyo amekupigia pande (chapuo) kwa watu wa GSM na ukateuliwa wewe na najua hata 20% ya mshahara wako utamgawia kwa makubaliano yenu. Ila kuwa makini kwani utaharibu na unaanza kupotea (kuvapa) mapema sana tu.
 
"Kesho nataka kwenda TFF Kumuombea Msamaha Haji Manara na naamini watanisikiliza na Kumsamehe" Ally Kamwe Msemaji wa Yanga SC ( Clouds FM Sports Extra )

*Waliopanga Watu wa kwenda Kuigiza Filamu ya Royal Tour na Rais Samia walitakiwa wamjumuishe na Mchezaji bora Tanzania nzima tena akitokea Zanzibar atokako Rais Samia aitwae Feisal Salum Fei Toto ili awavutie zaidi Wazungu" Ally Kamwe Msemaji wa Yanga SC ( Clouds FM Sports Extra )

Mdogo wangu Ally Shabaan Kamwe najua hivi sasa Unahangaika na Kujitahidi sana kutaka kulipa Fadhila kwa Mhamasishaji Mkuu wa Yanga SC Haji Manara ambaye ndiyo amekupigia pande ( chapuo ) kwa Watu wa GSM na ukateuliwa Wewe na najua hata 20% ya Mshahara wako utamgawia kwa Makubaliano yenu, ila kuwa makini kwani utaharibu na unaanza Kupotea ( Kuvapa ) mapema sana tu.
Huyu muzeye nae.
 
Tatizo Ally Kamwe kila anachojaribu kufanya anaangalia kama kina contradict policies alizokuja nazo Manara ili isionekane kama anampinga.

Na pale anapogundua kuwa kaenda kinyume basi mchizi ni kama anajiona ana deni na inamshurutisha kusawazisha kosa lake kwa kuongea kitu ambacho Manara kitamfurahisha kwa lengo la kuituliza nafsi.

Juzi kama sikosei alisema anakuja na mfumo mpya wa kipekee wa kufanya Club iwe kubwa kuliko mtu binafsi kama ambavyo wetu wengi wamekuwa wakifanya.

Sasa ukiangalia hizo za kutumia Club kujikuza ni policies za Manara na ndio maana hata katika press zake mara nyingi amekuwa akisema brand yake ameijenga kwa jasho na damu.

Naona sasa Ally baada ya kugundua kauli yake hiyo ni mkuki kwa Manara akaamua aje na hiyo ya kumuombea Manara msamaha TFF ku clear a mess
 
Hata wale WACHAMBUZI WA MCHONGO, wanajitahidi sana KUMCHONGANISHA, na KUMTOA NJE YA MSTARI! Mara, oooo, unaonaje KISPIKA na MALORI! Mara oooooooiii, ajitahidi KUWAZODOA SIMBA!
 
Dogo mzigo unaweza kumwelemea mapema maana huwezi kufanya kazi kwa kuzingatia hisia za mtu/watu wachache wanasemaje.

Bali ni kuzingatia weledi tu, kwa manufaa ya klabu nzima na taifa
 
Ally Kamwe akitaka majukumu yake yamuendee vyema pale Yanga SC, kwanza awe huru, asijione ana mzigo wa kumfurahisha yeyote, pili anatakiwa ku focus na masuala ya timu na menejimenti kwa ujumla, mambo ya mtu binafsi aachane nayo, kwani hakuna mtu mkubwa zaidi ya taasisi anayoiongoza.
 
Hata wale WACHAMBUZI WA MCHONGO, wanajitahidi sana KUMCHONGANISHA, na KUMTOA NJE YA MSTARI! Mara, oooo, unaonaje KISPIKA na MALORI! Mara oooooooiii, ajitahidi KUWAZODOA SIMBA!
Bahati nzuri hicho kispika hata sadio mane anakitumia
 
Attachments

  • IMG_20220929_202227.jpg
    IMG_20220929_202227.jpg
    56 KB · Views: 4
Back
Top Bottom