Mdomo umewaponza kwa kuwashutumu wengine wanatoa kafara ndugu zao

Ophonso

Member
Joined
Feb 2, 2021
Posts
33
Reaction score
122
Hakuna kitu kibaya sana kama ulimi. Usipouchunga ulimi wako utakuletea aibu, madhara kwako na kwa wengine.

Hii familia imekuwa inaropoka sana wengine wakipoteza wapendwa wao tena katika mazingira ya kawaida tu ya kifo kama ajali au magonjwa. Utasikia tu eti Wamemtoa Kafara.

Mtu kafa kwa ukimwi eti Wamemtoa kafara. Mtu kapata ajali kwa kuendesha huku kalewa na hovyohovyo eti Wamemtoa kafara. Mna bibi yenu na babu yenu wana miaka zaidi 90 wamekufa kwa kifo cha kawaida tu cha uzee eti wamewatoa kafara.

Sasa nao wamepoteza mpendwa wao kwenye ajali yani watu tumekomalia kila mahali tena tunasambaza huu uzushi kwa jazba Wamemtoa kafara na inawauma sana.

Sisi Waafrika ni watu wa ajabu sana.
 
Na wewe siku ukipotea humu katika mazingira ya kutatanisha, tutasema Mods wamekutoa kafara. Maana hakuna namna.
 
Hakuna kitu kibaya sana kama ulimi. Usipouchunga ulimi wako utakuletea aibu, madhara kwako na kwa wengine.

Hii familia imekuwa inaropoka sana wengine wakipoteza wapendwa wao tena katika mazingira ya kawaida tu ya kifo kama ajali au magonjwa. Utasikia tu eti Wamemtoa Kafara.

Mtu kafa kwa ukimwi eti Wamemtoa kafara. Mtu kapata ajali kwa kuendesha huku kalewa na hovyohovyo eti Wamemtoa kafara. Mna bibi yenu na babu yenu wana miaka zaidi 90 wamekufa kwa kifo cha kawaida tu cha uzee eti wamewatoa kafara.

Sasa nao wamepoteza mpendwa wao kwenye ajali yani watu tumekomalia kila mahali tena tunasambaza huu uzushi kwa jazba Wamemtoa kafara na inawauma sana.

Sisi Waafrika ni watu wa ajabu sana.
Fanya hiphop taja majina la sivyo huu ni umbea
 
Kwa hiyo unawakingia kifua watoa kafara, au mimi ndo sijakuelewa......hii kitu inaonekana imekukera sana, isije ikawa na wewe ni miongoni mwa hao watoaji kafara.
 
Hapo ni mkuki kwa kitimoto,kwa binadamu mchungu
 
Back
Top Bottom