Melki Wamatukio
JF-Expert Member
- May 3, 2022
- 6,156
- 10,974
Napitia kipindi kigumu ndugu zanguni katika kipindi hiki kigumu cha wanaume wazee wa vilainishi Daslamu. Mtaani naanza kuishi kwa mashaka sana
Hivi karibuni imeibuka hali ya kuzubaa ambayo inaukumbuka uso wangu. Kuna muda nikitizama kitu najikuta naganda, mwisho wa masaa najisahau kabisa, kuja kuganduka najikuta niko mdomo wazi, kanakwamba nashangaa hicho kitu kwa kukiona cha ajabu sana
Hali hii ilianza kunisikitisha kwa kuwa siku hizi ninapoganda, ile kuganduka najikuta namtizama mwanamke kwa kumtumbulia macho kwa makodo makubwa sana huku mdomo wangu ukiwa wazi, ishara ya kama namshangaa, ama kanivutia, ama kanikosha, ama kanishangaza, baada ya hapo udelele hutoka kwa kiasi fulani na kudumbukia kwa mfuko wa shati kama hiyo siku nitakuwa nimevaa shati langu la chichiemu, kisha maisha yataendelea kama kawaida, siku hadi siku
Kinachonishangaza, kila mwanamke ambaye amekumbwa na hali yangu hii, huishia kunitizama tizama kila muda, wengine huvalia vizuri wanapopita mbele yangu, na wengine hujinyunyizia unyunyu, wengine hufika mbele yangu na kuanza kunishangaa, muda huo wengine wakionesha tabasamu na wengine kuonesha kushangaa
Cha ajabu naskia za chinichini kuwa nina mazoea na baadhi ya wanawake ilihali hata salamu nao sina zaidi ya kuoneshana tabasamu tu, tena ni pale tu ninapoanzwa
Hali hii itakuja kunisababishia madhara makubwa sana. Nifanyeje?