HOJA MDORORO WA KIBIASHARA POSTA: Kwanini Kata za Kivukoni na Kisutu zimekuwa "kimya" kibiashara tofauti na zamani? Wafanyabiashara wameihama?

HOJA MDORORO WA KIBIASHARA POSTA: Kwanini Kata za Kivukoni na Kisutu zimekuwa "kimya" kibiashara tofauti na zamani? Wafanyabiashara wameihama?

Hoja ya Mdau inayopendekeza maboresho au mabadiliko ndani ya jamii, inayotakiwa kuangakiwa kwa mapana na Mamlaka husika

Mkono Mmoja

JF-Expert Member
Joined
Jan 26, 2019
Posts
4,994
Reaction score
9,625
Wana-JamiiForums,

Leo nimeona niguse mabadiliko makubwa yanayoendelea katikati ya jiji la Dar es Salaam (CBD), hususan katika eneo maarufu la Posta linalojumuisha Kata za Kivukoni (Posta ya Zamani) na Kisutu (Posta Mpya). Hili ni jambo linaloonekana wazi kwa mtu yeyote anayepita au kufanya kazi maeneo haya siku hizi.

Kama tunavyokumbuka, miaka ya nyuma Posta ndio lilikuwa eneo lenye heshima na msisimko mkubwa wa kibiashara. Barabara kama Samora Avenue, India Street, na mitaa inayozunguka Posta Mpya zilikuwa zimefurika maduka ya nguo, vifaa vya kielektroniki, na huduma mbalimbali. Kulikuwa na mzunguko mkubwa wa wananchi wanaoingia madukani kufanya manunuzi, hali iliyofanya eneo hili kuchangamka sana mchana kutwa.

Hata hivyo, miaka ya hivi karibuni, hali imebadilika kwa kiasi kikubwa sana. Eneo la Posta sasa limekuwa kimya sana (low foot traffic) na linaonekana kupoteza mvuto wake wa kibiashara wa zamani. Ukiacha wingi wa watu wanaofuata huduma katika taasisi za Serikali, Bandari na Feri,Soko la samaki feri, na Stesheni ya Reli, shughuli za kibiashara za binafsi zimeshuka kwa kasi, na eneo hili linaonekana kudorora au "kufa kifo cha asili."

Ushahidi wa hili ni uwepo wa mabango mengi yanayotangaza nafasi wazi za ofisi na maduka katika majengo mengi ya ghorofa yaliyopo Kivukoni na Kisutu. Wafanyabiashara wengi hawaipi tena Posta ule uthamani wa zamani; wengi wao wamekimbilia soko la Kariakoo, huku wengine wakifungua biashara zao maeneo ya pembezoni mwa mji kama Sinza, Mbagala, Mbezi n.k
Kutokana na hali hii, ningependa kuleta hoja hizi kwenu kwa ajili ya mjadala wa pamoja:

• Ukosefu wa wateja wa madukani: Nini hasa kimesababisha wananchi wa kawaida wasiingie tena madukani Posta kununua vitu kama ilivyokuwa zamani?

• Kodi na Uendeshaji: Je, kodi kubwa za majengo ya Posta haziendani na hali halisi ya maisha na vipato vya sasa, na hivyo kuwakimbiza wafanyabiashara?

• Changamoto ya maegesho ya magari: Je, ukiukaji na ugumu wa kupata maegesho (parking) unachangia watu kulikimbia eneo hili?

• Ushindani wa Kariakoo: Kwanini soko la Kariakoo limefanikiwa kuimeza Posta kibiashara, licha ya Posta kuwa na miundombinu iliyopangwa vizuri zaidi?

Je, una maoni gani kuhusu mabadiliko haya ya eneo la Posta? Nini kifanyike kurudisha msisimko wa kibiashara katika kata eneo hili la posta, au ndio tushazoea kuwa Posta ni eneo la ofisi za serikali na wasafiri tu?
 
Uwepo wa office spaces nyingi nadhani ni kila jengo ndio imesababisha kuwe na low traffic na biashara kudorora.Na kuongezea posta imekuwa zaidi kama administrative na corporate CBD na hivyo msongamano kuwa mdogo sana hasa wakati wa usiku..Pia kurise CBD nyingine ambazo hasa ni commercial hub na Makazi kama Kariakoo kunafanya ubora wa posta wa zamani udorore,hili suala si Tanzania tu,nchi nyingi ambazo zinaendelea hukumbana na hii changamoto
 
Ajabu sana K/koo unakuta watu wanagombea fremu zenye kilemba cha milioni 100 ila posta unakuta jengo tupu
 
Back
Top Bottom