LGE2024 Mdude atolewa Songwe na kupelekwa Mbeya kwa mahojiano zaidi

LGE2024 Mdude atolewa Songwe na kupelekwa Mbeya kwa mahojiano zaidi

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
128,308
Reaction score
245,426
Angalieni wenyewe namna Polisi wanavyohangaika na mtu ambaye wala hana silaha yoyote

Screenshot_2024-11-25-17-14-04-1.png

Halafu rudisheni kumbukumbu ya namna walishughulikia ajali ya ghorofa Kariakoo.
---
Wakati Jeshi la Polisi mkoani Songwe likimaliza mahojiano na kada wa Chadema, Mdude Nyagali, mwanaharakati huyo anapelekwa mkoani Mbeya kwa mahojiano mengine na jeshi hilo kujibu tuhuma zinazomkabili.

Nyagali alikamatwa Novemba 22, 2024 mkoani Songwe akiwa na makada wengine wa Chadema akiwamo Mwenyekiti wake Taifa, Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Kanda ya Nyansa, Joseph Mbilinyi 'Sugu' kwa madai ya kukiuka taratibu za kampeni.

Kupata taarifa na matukio yote kuhusu uchaguzi wa serikali za mitaa ingia hapa: LGE2024 - Special Thread: Orodha ya Mijadala ya Mikoa yote Tanzania Bara inayoshiriki katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Hata hivyo, makada wengine waliachiwa na Polisi kueleza kuwa inamshikilia Mdude kwa mahojiano zaidi.

Akizungumza na Mwananchi leo Novemba 25, 2024 Kamanda wa Polisi mkoani Songwe, Agustino Senga amesema tayari wamemaliza mahojiano na mwanaharakati huyo, na tayari ameelekea Mbeya kujibu tuhuma nyingine zinazomkabili.
 
Hahhaa.....kuna Mapajero yanafanya operation kuanzia Dar hadi Mbeya......RPC akiulizwa vipi kuhusu hawa na wewe upo anasema anashangaa na yeye hajui.

Hiki chama jamaa wanakifaidi sana. Wanakisaidia lakini na wao wanapiga sana mapene

..sitashangaa baada ya Polisi wa Mbeya, wa Njombe nao watasema wana mashtaka na Mdude.
 
Imeelezwa Kiongozi wa Chadema Mdude Nyagali amemaliza mahojiano mkoani Songwe na sasa Polisi wanampeleka Mbeya Kwa mahojiano zaidi

Source Mwananchi
polisi lazima wadeal na kaidi kulingana na ukaidi wake,

hakunaga mbambamba kumdhibiti mtu wa mshari with low IQ like nyumbu :pulpTRAVOLTA:
 
Back
Top Bottom