Mdude Chadema, kama alivyo Tundu Lissu, ni kama kile kizazi kinachotoweka cha wapagani uhuru wa bara hili kutokana na ujasiri walionao

Salary Slip

Platinum Member
Joined
Apr 3, 2012
Posts
49,390
Reaction score
152,301
Mdude CHADEMA, kama alivyo Tundu Lissu, ni miongoni mwa binadamu wachache sana wenye ujasiri na walio tayari kukabiliana na hatari iliyo mbele yao kwa lengo la kupigana kile wanachokimimi ni sahihi kama vile kupigana haki za watu wengine, uhuru wao, n.k hata ikibidi kwa gharama ya maisha yao.

Watu kama kina Mandela na wengineo waliokuwa tayari kwa lolote katika kupigania uhuru na haki za watu weusi, ni kizazi kinachotoweka na sasa tunabakiwa na watu wachache wa aina hiyo akiwemo Tundu Lissu na Mdude Chadema kwa Tanzania ya leo.

Naomba niseme huenda Mdude ni mwanasiasa na mwanaharakati jasiri kuliko wote waliopo nchi hii kwa sasa na anachokikosa ni cheo au wadhifa mkubwa katika jamii ambao ungemfanya awe mtu maarufu na mashuhuru katika kupinga udhalimu, uonevu, ufisadi, matumizi mabaya ya madaraka, n.k.

Kama unabisha, kasome tweets zake za kijasiri anazoziandika kuhusu yanayoendelea huko Ngorongoro huku akimshambulia moja kwa moja Bi. Mkubwa kama alivyokuwa anafanya Tundu Lissu enzi za Mwendazake.

Kwa madhara aliyoyapata Mdude, wengi walitarajia saa hizi angekuwa muoga na mpole kuliko mtu mwingine yoyote ila ukweli ni jasiri na mwenye uthubutu kuliko mtu yoyote kwa sasa na kuweka wazi katika moja ya tweets zake kuwa wakitaka "wamuue".

Mama, kwa Mdude, unalo na usipokuwa na uvumilivu, utafanya yale ya Mwendazake.

Naishia hapo.
 
Kupungukiwa intelligence ni tofauti na ujasiri bwashee. Siyo kila anayesema ovyo ni jasiri. Keep that in mind.
 
Walitakiwa wazaliwe enzi za maji maji, chini ya chifu Songea, Kijengitile, Mkwawa, Miarambo, Fundikira au Kimweri ambao hawakuwa wanaogopa kukosoa na kutenda katika kile wanachokiamini

Nimewaacha Rumanyika wa Kagera na Mangi Sina/Meli wa Kilimanjaro kwa makusudi maana hao waliingia sana mikataba na wajerumani ya kutengeneza matabaka na kujimilikisha mali kama mashamba, vito, wanyama nk bila kutetea wananchi wa jamii yao kwa ujumla ila makundi fulani tu yenye nguvu ya ukwasi
 
Back
Top Bottom