Bezecky
JF-Expert Member
- Apr 28, 2024
- 494
- 897
๐๐ฎ๐ง๐๐ฎ ๐๐ข๐ฌ๐ฌ๐ฎ, ๐๐จ๐ก๐ง ๐๐๐๐ก๐ ๐ง๐ ๐๐๐ฆ๐ ๐ง๐ข ๐ฐ๐๐ฉ๐ข๐ ๐๐ง๐ข๐ ๐ก๐๐ค๐ข ๐ฐ๐ ๐ฎ๐ค๐ฐ๐๐ฅ๐ข ๐ญ๐ฎ๐ฐ๐๐ฎ๐ง๐ ๐ ๐ฆ๐ค๐จ๐ง๐จ.
Lissu, Heche na Lema hawa ni rafiki na ndugu wa haki. Kujitoa kwao kupigania haki za mtu & watu wowote kwao ni jambo la kawaida. Binafsi kwangu kila mmoja amehusika kunisaidia kupigania haki zangu tangu mwaka 2016.
Heche na Lema walifanya mchakato wa kunitorosha nchini mwaka 2018 wakati wa jaribio la utekaji dhidi yangu katika ziara ya makamu Rais mkoa wa Songwe na Mbeya.
Kwa mujibu wa mmoja wa watekaji aliyeamua kutoa taarifa za kunisaidia alisema watekaji waliokuwa kwenye ziara ya makamu wa Rais walikuwa na kazi mbili, moja ilikuwa ni kunipoteza na kazi ya pili ilikuwa kufanya uchunguzi wa tuhuma za RC wa Songwe wakati huo alikuwa akiitwa Chiku Galawa.
Nilimpigia Simu heche muda huo huo na kumsimulia, akachukua hatua kumpigia simu Haonga aliyekuwa mbunge wa Mbozi kwamba afanye awesavyo anitoroshe Vwawa mkoani Songwe mpaka Mbeya kwa wakili wangu Mwabukusi wakati yeye na Lema wanafanya utaratibu wa kunitafutia sehemu salama.
Ni kweli nilifanikiwa kutolokea Arusha kwa gari ya wakili wangu Mwabukusi kabla ya mimi kughaili mpango wa kukimbilia Kenya ambako Lema na Heche waliandaa mazingira. Nikiwa uhamishoni Arusha baada tu ya ziara ya makamu wa Rais kutamatika, ikulu ilitoa press statement ambayo ndani yake moja ya taarifa zilikuwa ni kutumbuliwa kwa yule RC wa Songwe ambaye watekaji walisema wamekuja kufanya uchunguzi dhidi yake na kunipoteza mimi. Hapo niliamini kweli nilikuwa kwenye target. Wakati wote niko Arusha Lema ananichukua na kunipeleka lunch na dinner wakati wote huku akinitia moyo.
Lissu kaka yangu mpendwa alifika Oysterbay baada ya kutekwa na kuteswa na polisi kisha kusafirishwa mpaka Dar mwaka 2016. Baada ya kufikishwa Dar nilichukuliwa na vikosi vya task force mpaka mikocheni kwenye moja ya nyumba zao za mateso nikaanza kuteswa huku nikiwa nimevuliwa nguo zote. Niliteswa kutwa nzima kabla ya kurudishwa Oysterbay na baadaye kupelekwa hospital ya Mwananyamala kutokana na hali yangu kuwa mbaya.
Baada ya matibabu nilirudishwa Oysterbay. Lissu alifika na nilisikia mahabusu waliokuwa wakichungulia dirishani wakiimba Lissu ! Lissu! Huku wakisisitiza kwamba Mdude hapa umetoka kuna siku Lissu alikuja hapa usiku wa saa sita na aliwatoa watu. Kwanza nilikuwa nashindwa kusimama kutokana na maumivu ya kipigo ila nilivyosikia Lissu yuko nje anaingia pale kituoni nilisimama kwa furaha na ujasiri.
Kwanza Lissu alipiga mkwala kwa RPC wa Kinondoni kutaka nipelekwe mahakamani au nipewe dhamana. Mimi ndio mtu wa kwanza kumsimulia Lissu uwepo wa nyumba za mateso kwa raia wakiwemo wapinzani wa serikali. Lissu akaniahidi kwamba anaenda kufanya press kwa lugha ya kiswahili na kingereza ili dunia ijue wapinzani wanavyoteswa na serikali.
Lissu huyu hakuishia hapo akaenda bungeni kuzungumza kuhusu mateso yangu na nyumba za mateso kwa ajili ya wakosoaji ya serikali.
Hivi katika mazingira haya ni nani unaweza kuja ukaniambia hawa watu ni vibaraka wa serikali nikakuelewa? Watu wanaojitoa kutetea haki namna hii tangu wakawa vibaraka wa serikali? Kwamba hawa wakaa kimya tukitekwa, tukiumizwa ndio wapinzani wa kweli halafu akina Lissu ndio vibaraka? Labda mgonjwa wa akili ndio ataamini.
Watanzania wenzangu tuwaunge mkono wapigania haki hawa katika nafasi zozote wanazogombea iwe ndani ya chama au serikali.
Mdude Nyagali 7 x 70 Sumu ya Nyigu.