Mdude Nyagali: Polisi walikosea kuwaua walioteka watoto Mwanza

Mdude Nyagali: Polisi walikosea kuwaua walioteka watoto Mwanza

comte

JF-Expert Member
Joined
Dec 11, 2011
Posts
9,019
Reaction score
6,825
"Watekaji wawili walikuwa wanajihami kwa mapanga lakini askari polisi zaidi ya 20 walishindwa kuwadhibiti wahalifu hao wawili wenye mapanga na kulazimika kuwapiga risasi.

Yani askari zaidi ya 20 wanashindwa kuwadhibiti wahalifu wawili wenye mapanga na kulazimika kuwaua kwa mbali kwa kuwapiga risasi?

Ndio maana nasema hili jeshi letu la polisi ni bovu limepoteza weledi na ufundi kama lilivyokuwa miaka ya nyuma. Kwa sasa jeshi letu la polisi linatumia nguvu nyingi akili kisoda.

Ndio maana tunataka serikali mpya itakayolifanyia ukarabati jeshi hili. Hii ni aibu." Ameandika mdude kupitia ukurasa wake wa X
Image
 
Wangewathibiti wale wawili wenye mapanga wangelisaidia sana Jeshi la Police kuuelewa na kuufumua kabisa mfumo wote wa utekaji watoto.
 
Alikua kwenye tukio? Kama mhalifu anakaidi kujisalimisha mbele ya mtutu unajua anajiamini na nini je vyumba vingine kama wangekua wengine wenye silaha nzito je?
 
Hapo baadae tena tutakuja hapa na kusema tena hapo zamani jeshi letu lilikua na weledi tofauti na sasa.
Hii ndivyo wanadamu tulivyo
 
Kuna vitu sio vya kutetea kabisa
Wanajiita wanaharakati wapenda haki..

Hayo mapanga wangechinja hao watoto Police wangeficha wapi sura zao na matusi haijulikani...

Au police wangeuwawa sijui ingekuwaje...

Ila Mdude sishangai... He knows nothing, i mean he doesnt know anything..

Wafuasi wa Maria Sarungi wengi ni vichwa maji.
 
Acha wauawe tu ili kusudi iwe fundisho kwa wengine.
Lakini wangekuwa na sniper awavunje miguu, ili kusudi waseme mtandao wao wote.
 
Asuburie watoto wake watekwe ndipo aje kuropoka hivyo.
Angekuwa amezaa asingeropoka hivyo
 
Kwa mujibu wa sheria za Polisi, mshukiwa wa ujambazi akiwa na silaha yoyote na amekataa kujisalimisha kwa kuitupa na kuinua mikono juu, kinachofuata ni kumshuti maana hujui nini kinampa kiburi...
 
Pole mdude wenzako wameliwa kichwa. Unaambiwa weka panga chini jisalimishe . Hutaki lazima uliwe kichwa tu
 
Naunga mkono hoja


Duuh Kumbe walikuwepo askari 20? Kazi kweli kweli
 
@mdudenyagali


"Watekaji wawili walikuwa wanajihami kwa mapanga lakini askari polisi zaidi ya 20 walishindwa kuwadhibiti wahalifu hao wawili wenye mapanga na kulazimika kuwapiga risasi. Yani askari zaidi ya 20 wanashindwa kuwadhibiti wahalifu wawili wenye mapanga na kulazimika kuwaua kwa mbali kwa kuwapiga risasi? Ndio maana nasema hili jeshi letu la polisi
@tanpol
ni bovu limepoteza weledi na ufundi kama lilivyokuwa miaka ya nyuma. Kwa sasa jeshi letu la polisi linatumia nguvu nyingi akili kisoda. Ndio maana tunataka serikali mpya itakayolifanyia ukarabati jeshi hili. Hii ni aibu." Ameandika mdude kupitia ukurasa wake wa X
Image
Hivi kesi ya Mdude_Nyagali na polisi, hakimu ni nani? Naona haiishi tu.
 
Back
Top Bottom