Mdude Nyangali amfananisha Mbowe na Nabii Musa, Lisu na Nabii Joshua

Mdude Nyangali amfananisha Mbowe na Nabii Musa, Lisu na Nabii Joshua

Mdude anapotosha biblia kwa maslahi yake. Mwenyezi Mungu hakumwambia Musa ampishe Joshua, bali alimuadhibu Musa asiingie nchi ya Kaanan kwa kosa,lile la kule kwenye issue ya kuwapa maji wana wa israel katika mwamba , hivyo alimuagiza amkabidhi Joshua mikoba kisha yeye akapanda hadi kilele cha mlima Nebu akafa huko na akazikwa na malaika wala hakuna anayejua kaburi lake.

Lissu wao ameingizwa chaka na wapiga kelele za mtandaoni hana option bali kukabili sanduku la kura. Mtasema hadi siku ya uchaguzi lakini hapishwi mtu.
Hahaha ni ajabu sana hawataki uchaguzi, wanataka mgombea apite bila kupingwa, APEWE, APISHWE, hawataki demokrasia.

Viumbe waajabu sana, eti wapigania haki.
 
Kasome biblia haruni ndo alikua nabii wa Musa
Mungu alimchagua Musa kuwatoa Wana wa Israel utumwani Misri Musa akamuambia Mungu yeye hajui kuongea anakigugumizi ndio Mungu akamwambia Musa ndugu yako Haruni ataongea baadala yako yaani Musa atakuwa anapokea maagizo toka kwa Mungu kisha anampa maagizo hayo Haruni akamwambie Farao (Firani)

Hivyo Mungu akamuambia Musa yeye atakuwa kama ndiye Mungu anatoa maagiza kwa Haruni na Haruni atakuwa kama nabii anapokea maagizo ya Musa

Hivyo Haruni hakuna nabii alikuwa kama speaker la Musa siku hizi watoto wa mjini wangesema alikuwa chawa wa Musa
 
Mbowe anaheshimika sana, lkn wanachadema hawamtaki kwa sasa.
Lakini inasemekana wasiomtaka wengi ni wanaharakati wa mtandaoni wengi wao ni wale wanaoshi nje ya nchi na ambao ndio waliomshawishi Lisu kugombea
 
Msimamo wake yeye anaenda na nani kati ya Lisu na Mbowe?

..Mdude amesema huu ni wakati wa Chadema kwenda na Tundu Lissu.

..huo mfano wa Biblia ameutumia kuupongeza mchango wa Freeman Mbowe kwa Chadema, na kubainisha kwamba Tundu Lissu ndiye kiongozi anayefaa kuongoza chama kutokana na mazingira na mahitaji ya sasa.
 
Back
Top Bottom