Meatballs and spaghetti

farkhina

Platinum Member
Joined
Mar 14, 2012
Posts
14,568
Reaction score
16,917
Mahitaji

Nyama ya kusaga nusu

Kitunguu maji 1

Kitunguu saumu 2 teaspoon

Tangawizi 1 teaspoon

Kotmir (giligilani) 1 teaspoon

Bizar ya pilau 1/2 teaspoon

Mdalasini 1/2 teaspoon

Bread crumbs

Chumvi kiasi

Ndimu/limau 1

Pilipili manga 1 teaspoon

Pilipili ya kuwasha

nyanya. 2 kubwa

Nyanya ya kopo

Mayai 2-3 inategemea na ukubwa

Mafuta ya kupikia

Spaghetti


#1 meatballs


Namna ya kutaarisha

Weka nyama kwenye bakuli safi then tia pilipili manga,chumvi kiasi,tangawizi,saumu changanya vizuri

Mimina bread crumb then changanya

Katika bakuli lengine dogo vunja mayai na koroga then mimina katika nyama halafu changanya

Tengeneza viduara ukubwa kiasi then weka pembeni

Weka pan na mafuta kiasi hakikisha mafuta yanapata moto vziur then kaanga meatballs hadi ziwive na kuwa dark brown


Toa then weka zijichuje mafuta


....#2 sauce


Weka mafuta kidogo katika sufuria

Kaanga kitunguu maji then weka saumu na kotmir kaanga vizuri

Mimina nyanya uliosaga na nyanya ya kopo

Weka chumvi,limau na pililipi wacha ichemke

Weka meatballs zako ndani ya sauce baada ya 5 minute epua


....#3 spaghetti


Chemsha maji hadi yapate moto

Mimina spaghetti na wacha ziwive then chuja maji


Weka katika sahani na weka meatballs juu yake

Enjoy

Sent from my BlackBerry 9320 using JamiiForums
 
Thank u maa but naweza kupunguza viungo kama sitaki vingiii coz vinaboa kwa mtu mwenye kiungulia au mtu akicheua

Thank u in advance,kaz kwangu jikon
 
Thank u maa but naweza kupunguza viungo kama sitaki vingiii coz vinaboa kwa mtu mwenye kiungulia au mtu akicheua

Thank u in advance,kaz kwangu jikon

Karibu shosti

Sent from my BlackBerry 9320 using JamiiForums
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…