Meatu: Madiwani wamtaka Waziri TAMISEMI afanye ukaguzi maalumu wa fedha za Halmashauri, wanusa harufu ya ubadhirifu mkubwa

Meatu: Madiwani wamtaka Waziri TAMISEMI afanye ukaguzi maalumu wa fedha za Halmashauri, wanusa harufu ya ubadhirifu mkubwa

SULEIMAN ABEID

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2013
Posts
390
Reaction score
385
BAADHI ya Madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Meatu wamemwandikia barua waziri mwenye dhamana na Serikali za Mitaa hapa nchini (TAMISEMI) Angela Kairuki ili atume timu maalumu ya ukaguzi iweze kufanya ukaguzi maalum katika Halmashauri hiyo ya wilaya kukagua matumizi ya fedha ambazo zilipangwa kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo.

Madiwani hao wamesema wamepatwa na wasiwasi baada ya kubaini Menejimenti ya Halmashauri hiyo ya wilaya imekuwa ikibadili matumizi ya fedha za miradi kwa kuelekeza fedha kwenye miradi ambayo haikupitishwa na Baraza kwenye Bajeti la 2022/2023 huku miradi wakiondoa fedha kwenye miradi iliyopangwa na Baraza la Madiwani.

Madiwani hao wameambatanisha baadhi ya hoja zao kama zilivyo katika kiambatanisho hiki, Fungua hapa;
 

Attachments

Back
Top Bottom