Nilikuwa nakuheshimu sana, ila kwa sasa nakudharau kama JiweWanabodi,
Kuhusu Uchaguzi Mkuu wetu na ushindi wa kishindo wa JPM na CCM, huko nyuma niliwahi kutoa angalizo hili muhimu la kiusalama
Security alert kwa Serikali yetu, tuwe makini sana na Marekani: Kuna kitu kinapangwa halafu wajifanye walionya kabla. Je, wanapanga Kutu-Libya?
Kabla ya hapo, mara kadhaa vyombo vya habari vya kimataifa vya mabeberu, vimekuwa vikiandika makala za uongo na uzushi kuhusu Tanzania zikiwemo kumsema vibaya rais wetu Magufuli ikiwemo kumsingizia kuwa ni dikiteta na anaiendesha Tanzania kidikiteta, na mara zote, uzushi huu huwa haukanushwi, hivyo unaendelea kurudiwa na kurudiwa tena na tena.
Udikiteta: Uongo Ukisemwa Sana na Kuachwa Bila Kukanushwa Hugeuka Ukweli!. Dawa ya Uongo ni Ukweli.
Uongo unaosemwa kumhusu Rais wetu Magufuli na nchi yetu Tanzania, usipuuzwe! Ukanushwe na ukweli usemwe!
Serikali yetu Kuitwa "Sinister" na "Authoritarian": Je, ni kweli? Kama si kweli, Tusiukubali Uongo huu, Tuukanushe!
Leo nimekutana na makala hii katika mtandao wa kibeberu wa WPR, ambayo iliandikwa October 8 na mwandishi Sofia Naimam, ikizungumzia uchaguzi Mkuu wa Tanzania, Mabeberu hawa, kati ya wagombea wote 16 wa urais wa Tanzania, wao wakaamua kumhoji mgombea mmoja tuu, Tundu Lissu, na akawaambia anakwenda kushinda urais wa Tanzania, na wao wakaamini, hivyo sasa wanaandika makala za kututisha kuwa Tundu Lissu asipotangazwa mshindi, Tanzania hapatakalika!.
Watu wengine waliohojiwa kwenye makala hii ni Zitto Kabwe, Robert Amsterdam, Fatma Karume, Balozi wa Marekani,
Thabit Jacob,
Ili mwandishi kubalance story yake, akaandika kuwa ameitafuta Ikulu yetu na Tume ya Uchaguzi NEC, wote wamegoma kutoa ushirikiano, swali la kujiuliza ni kwanini mabeberu hawa, wazushe kuhusu Tanzania halafu waitafute Ikulu yetu na NEC, wakati the right mtu wa kutafutwa ni Msemaji Mkuu wa Serikali, Dr. Hassan Abbas?!.
Kwavile mimi ni mwandishi wa habari, na mchambuzi wa habari, news analysis, nitawachambulia makala hii kwa kueleza ukweli ni wapi mwandishi kasema kweli, wapi kasema uongo na wapi kaandika uzushi kwenye makala hii katika mtandao huu wa vyombo vya habari vya kibeberu.
Haiwezekani kila siku mabeberu hawa kutuzushia mambo ya uongo na uzushi kuhusu Tanzania na rais wetu, na sisi tunanyamaza tuu na kuunyamazia uongo na uzushi huu, huku tunao waandishi Watanzania wazalendo wenye uwezo wa kuukanusha, tunakuwa hatulitendei haki taifa letu, hatuwatendei haki, Watanzania. Tena ningewaomba Dr. Abbas na timu yake, kuwa more proactive kuzungumza mazuri ya nchi yetu na sio kusubiri watu watunge uongo na uzushi kisha ndio sisi tuje kujibu kwa kuwa reactive, kama ule uzushi wa juzi kati wa BBC Swahili kuhusu madini yetu. Uongo na Upotoshaji huu wa BBC London kuhusu Tanzania kipindi hiki cha kampeni una maana gani? Sio mbinu za mabeberu? Wapi weledi wa ki-BBC?
Makala yenyewe ya uzushi ni hii, na chini ina wasifu wa jmwandishi, ila pia, mimi kama mwandishi, naomba pia nimtendee haki mwandishi wa makala hii, kwa kukiri, katika media zetu hapa Tanzania, tuna waandishi wachache sana wa kiwango hiki cha uandishi, na sina uhakika sana kama kwenye wasaidizi wa Dr. Abbas, anao watu wenye uwezo wa kupangua uzushi kama huu, japo namfahamu Dr.Abbasi yeye kama yeye anaweza, ila watu wake.
Kwa wale wenzangu na mimi, wa lugha yetu hii ya madafu, tuishie hapa, maana...
![]()
President John Magufuli hands in his nomination form to the chairman of the National Electoral Commission, in Dodoma, Tanzania, Aug. 25, 2020 (AP photo).Tanzania’s Opposition Fears Election Violence Because, Lissu Says, ‘We Are Winning’
Sophie Neiman Thursday, Oct. 8, 2020
Uchambuzi wangu, unafuatia, ili twende pamoja, nitaichambua para moja moja kwa kuonyesha ipi ni kweli, upi ni uongo na upi ni uzushi.
Karibuni
Paskali
Sent from my Infinix X680 using JamiiForums mobile app