Mbigirikavu
Senior Member
- Aug 19, 2022
- 101
- 118
Hakuna anayependa kufa lakini kuna baadhi ya wagonjwa wanafikia kusema "Heri nife kuliko mateso haya", ndivyo ilivyo kwa wanayanga.
Wako tayari kwa matokeo yoyote ilimradi ichezwe, ipite, wawaze mengine, kutokana na fukuto la kuingia makundi kuanzia CAF Champions mpaka Shirikisho. Yanaga wanateseka kila uchao, hawana raha na maisha.
Presha mfululizo, maneno kuntu kutoka kwa wana Simba, hawalali, hapakaliki, damu haizunguki vizuri, pua zinabana, uchovu mwingi, jasho, miili inafukuta, vinyweleo vinachomachoma.
Imefika wakati wanaona bora liende wafunge au wafungwe, yote sawa tu.