Duniahadaa
JF-Expert Member
- Oct 16, 2017
- 336
- 677
Mechi hiyo inatazamiwa kuchezwa Oktoba mwaka huu. Ajabu ni kwamba kocha wa mojawapo ya timu mbili hasimu amejitokeza na kuwaambia watazamaji kuwa mchezo utakuwa wa haki tena haki tupu. Maswali yafuatayo yanajitokeza:
- Amejuaje wakati yeye si referee? Je, huyu kocha ni mpiga ramli?
- Je, au yeye ndio huwa referee nyuma ya pazia?
- Kwanini asimwache referee mwenyewe atamke?. Au yeye ndiye humwongoza kuwa mechi hii tenda haki na mechi hii fanya dhuluma?
- Kwanini ameanza kuwapa tuition ma-kocha wa timu za daraja la tatu na kuwakaririsha kawimbo waseme kuwa mechi ya Oktoba refarii lazima atatenda haki. Yaani kila kocha akitoka sebuleni kwake anaongea na waandishi wa habari kuwa “Oktoba haki tupu”. Hii si kuwahadaa mashabiki?
- Huu si uthibitisho kwamba kumbe huyo referee wa mechi hayupo huru bali hufanya kwa matakwa ya huyu kocha?
- TUNATAKA REFEREE WA MECHI AWE HURU.