Mechi ya Azam FC Vs Kitayosce imemalizwa kabla ya muda baada ya Kitayosce kubakiza wachezaji pungufu uwanjani

Mechi ya Azam FC Vs Kitayosce imemalizwa kabla ya muda baada ya Kitayosce kubakiza wachezaji pungufu uwanjani

option

JF-Expert Member
Joined
Jan 15, 2013
Posts
2,028
Reaction score
1,496
Mpaka muda hii Kitayose hawajatokea uwanjani kupasha misuli. Bado dkk 18 mpira uanze.
---
Kitayosce FC ilianza mechi dhidi ya Azam ikiwa na wachezaji nane [8], Bodi ya Ligi tulipokea uthibitisho kutoka TFF kuwa wachezaji nane [8] tu wa Kitayosce ndio wanastahili kucheza mechi ya Ligi.

Kikanuni inaruhusiwa timu kucheza ikiwa na wacheza nane [8]. Kanuni inaeleza timu itaruhusiwa kucheza ikiwa na wachezaji wasiozidi 11 na wasiopungua saba [7].

Kanuni hizohizo pia zinaeleza, endapo itakapotokea wale wachezaji wasiopungua saba mmoja wapo au zaidi akashindwa kuendelea na mchezo kwa maana wakapungua saba mchezo huo utamalizwa/utavunjwa.

Timu ambayo wachezaji wake wametimia uwanjani itapewa ushindi [alama tatu na magoli matatu] lakini kama ilikuwa imefunga magoli zaidi ya matatu, magoli yaliyofungwa yatasimama hivyohivyo.

Karim Boimanda, Ofisa Habari Bodi ya Ligi via Azam TV.
 
Back
Top Bottom