Mechi ya Fainali Kombe la Dunia Qatar 2022 itakuwa kati ya Ufaransa na Argentina

Mechi ya Fainali Kombe la Dunia Qatar 2022 itakuwa kati ya Ufaransa na Argentina

Final France vs Portugal
Halafu France atabeba ndoo kwa mara nyingine
 
Mkuu

Umekosea Sana!

Argentina,uholanzi,England,ureno,croatia ni team za kawaida kama ilivyo morocco!

Timu za kiwango ni Brazil na ufaransa Hawa ndio wababe wa kweli!
Tutarudi hapa ijumaa na jumamosi, utaikimbia hii komenti yako.
 
ENGLAND NI HATARI HAKUNA CHA BRAZIL WALA NANI.. HAWA JAMAAA WANACHUKUA NDOO.. VIUNGO WAO NI WAVUNJA KUNI HASA HAWANA MAMBO MENGI... KIUFUPI ENLAMD ANACHEZA MPIRA KAZI KAZI NA SIO UREMBO UREMBO WA BRAZIL ARGENTINA FRANCE UHOLANZI
Ngojea nimfowadie mbappe hiki kichekesho.😂
 
Naisubiri kwa hamu sana semi final ya brazil vs argentina.. naoenda soka america kusini pale wanapokutana wapinzani wa jadi ufundi, kukamiana, ubabe n.k kikubwa tu iyo game refa asiwatishe wachezaji kwa kutoa kadi kizembe zembe watu tuone show ingawa karata yangu nampa brazil maana ile front 4 yao ujui umkabe nani umwache nani
Itakuwa bonge moja ya mechi, burudani ya kutosha. Wakimpa yule refa wa jana kati ya Morocco na Spain itakuwa poa maana hatoi kadi hovyo. Mimi nipo na Argentina maana hao wachezaji wa Brazil unaowataja walikuwepo uwanjani tulipochukua Copa America palepale kwao mwaka jana.
 
Fainali nazo tamani zitokee,

France VS Brazil

Argentina VS Portugal
( Messi Vs benched Ronaldo)

Argentina Vs England
 
Hakuna team zenye discipline kwenye kombe la dunia kama Netherlands na Morocco wanacheza kwa tahadhari sana huku silaha yao ikiwa ni counter attack hata jana kama yule striker wa MORROCO angekuwa makini mechi ilikuwa haifiki kwenye matuta na MORROCO wameruhusu goal moja tu toka june mpaka sasa na linyewe lilikuwa own goal ni kweli kwenye mpira lolote linawezekana ila Netherlands na Morocco wanavyocheza vile ndio huchezwa mechi za knockouts stage respect the opponent first and Morocco and Netherlands are better on defence let's wait and see what's coming.
 
Naona mnajifanya kama hamjaiona Morocco ilivowapelekea moto Spain
Morocco hajapeleka moto bali alipelekewa moto na kupaki basi. Wana nidhamu ya hali ya juu hivyo mchezo utakuwa mzuri. Ureno wanao viungo wanaofungua njia ndio maana ninaona Morocco watatolewa kirahisi.
 
ENGLAND NI HATARI HAKUNA CHA BRAZIL WALA NANI.. HAWA JAMAAA WANACHUKUA NDOO.. VIUNGO WAO NI WAVUNJA KUNI HASA HAWANA MAMBO MENGI... KIUFUPI ENLAMD ANACHEZA MPIRA KAZI KAZI NA SIO UREMBO UREMBO WA BRAZIL ARGENTINA FRANCE UHOLANZI
Hamna team pale Maguire aliwazawadia nafasi mbili GHANA wakashindwa kuzitumia mbape pale angewalaza na viatu ENGLAND kwa France hata laki naweka kwenye betting namuuwa ENGLAND.
 
Hakuna team zenye discipline kwenye kombe la dunia kama Netherlands na Morocco wanacheza kwa tahadhari sana huku silaha yao ikiwa ni counter attack hata jana kama yule striker wa MORROCO angekuwa makini mechi ilikuwa haifiki kwenye matuta na MORROCO wameruhusu goal moja tu toka june mpaka sasa na linyewe lilikuwa own goal ni kweli kwenye mpira lolote linawezekana ila Netherlands na Morocco wanavyocheza vile ndio huchezwa mechi za knockouts stage respect the opponent first and Morocco and Netherlands are better on defence let's wait and see what's coming.
Netherlands amefika hapo alipo kwasababu ya ubovu wa forward ya Marekani. Ile mechi yao wangeweza kupigwa hata 3 kipindi cha kwanza. Pia kaunta attacks zao zilikuwa nyepesi sana kwa timu compact kama Argentina hawataweza kuzipiga.

Morocco wakikutana na viungo wanaojua kupress na kufungua njia wanafungika kirahisi. Wakisharuhusu goli moja wataanza kucheza open game na hapo wataumia zaidi.
 
Argentina haiwezi cheza dakika 90[emoji23][emoji23][emoji23]mechi ya juzi na Australia ilikua ni utopolo sana
 
Back
Top Bottom