Mechi ya kesho Simba vs Singida inaenda kufunga midomo ya wanasimba wanaolalamika kuhujumiwa

Mechi ya kesho Simba vs Singida inaenda kufunga midomo ya wanasimba wanaolalamika kuhujumiwa

Kutoka kupanda ndege mpaka morocco wamerud kupanda mabasi mpaka kmc complex
 
Kutoka kupanda ndege mpaka morocco wamerud kupanda mabasi mpaka kmc complex
1000284294.jpg
 
Simba anashinda kuanzia goli 3 na kuendelea, subirini muone
 
Singida big stars ni Yanga B, Sasa mkakati ni mmoja tu, Simba mbovu isitoboe, Singida katikati waweke midfielders 5 Simba hawatapita watapeleka mipira pembeni, halafu huko pembeni namba 7 na 11 washuke mda wote kusaidia mabeki, kisha watumie counter attack. Singida wasiache uwanjani mchezaji atakaepata yellow card maana refa atampa red ya kulazimisha bila aibu, Singida wasicheze offside trick refa atawapa Simba goli la offside, singida wasicheze rafu ndani ya box Simba watapewa penati, singida wasicheze rafu kwa nyuma refa atawapa red cards, kipa wa singida asicheleweshe muda atapewa red card, singida wasimzonge refa anapowaonea watapewa red cards aongee captain tu.

Hapo ndipo mpira wetu ulipofikia, tff na Simba wana mkakati Simba ishinde kwa lazima mechi zote ili Yanga ilazimike kucheza derby ambayo hatutaki, singida tuokoeni please piga hao makolo, maana gepu likibaki point nne hatuchezi Simba wapewe magoli matatu na points tatu, Singida ni timu kubwa onesheni ukubwa wenu, Simba weupe tu ni debe tupu linavuma, chezeni kama Mashujaa au Kmc walifungwa kwa kuonewa. Simba ukiibana katikati kazi yao inabaki kupigiana pasi na kuzurura tu uwanjani hasa kwenye eneo lao.
 
Shida ya simba ni kutaka kubebwa kila sehemu. Wanafikiri Bodi ya Ligi ni CAF! Motsepe ni Karia! Halafu yule mwamuzi wa Mauritania ni Tatu Malogo/Japhet Smart/Kepha Kayombo/Shomary Lawi!
 
  • Red Card za mchongo
  • Penalty za kujidondosha
  • Magoli ya offside
  • dakika kuongezwa 15
  • Singida wakitaka kufunga ni offside
Penati tatu Singida wamenyimwa halafu shirikisho wanamlaumu refa, ukiwauliza yule refa aliwafanya nini hawakupi majibu.Unakuja kugundua wamezoea kubebwa na marefa.
 
Leo hakukukuwa na Mpira ila vitendo vya aibu katika mpira.
Mtaongea sana na mtasubiri sana Simba ianguke. Simba ni mpango wa Mungu. Vile ambavyo inapigwa vita na kutukanwa sana na kuandaliwa mazingira ya kufungwa, ndio hapo hapo Mungu anatupitisha kuelekea kwenye ubora na mafanikio...endeleeni kupiga makelele haya toka Sasa kwenye kibuyu Cha kichawi ulichokalia tangu saa 10 mpira ulivyoanza.
 
Penati tatu Singida wamenyimwa halafu shirikisho wanamlaumu refa, ukiwauliza yule refa aliwafanya nini hawakupi majibu.Unakuja kugundua wamezoea kubebwa na marefa.
Si mlisema penati katika mchezo huwa ni za mchongo? Sasa unataka penati ya nini tena? 🤣🤣🤣
 
Back
Top Bottom