Okwi alishawaduwaza Tunisia pia ,Kikosii kitapangwa hivi ..Golini Manula, Kapombe, ,Zimbwe,Kennedy,Onyango,Baka,Kanoute,Nyoni,Muzamiri,Kibu,Saidoo,Usiwe na shaka, Simba atalinda heshma yake Morocco. Utaiona Simba ambayo haujawahi kuiona kwa muda mrefu.
Niliwahi kwenda Misri juzi juzi na katika pita pita zangu mitaani nilikuwa najitambulisha kama mwanasimba. Wakawa wanafurahi wakikumbuka tulichowafanyia Zamalek miaka ile.
Shukrani sana mkuu, nimeipokea hiiUnatakiwa ujiandae tu kisaikolojia. Huna sababu ya kujinyima raha huku ukitambua fika kipigo cha mbwa mwizi hakikwepeki kwenye hiyo mechi yenu ya marudio.
Hivyo unachotakiwa kufanya siku hiyo ya mechi, ni kunywa tu maji mengi ili kupunguza presha ya mzunguko wa damu kwenye mwili. Hii ni kwa utaalamu wangu lakini.
Wale jamaa wana ufundi wa hali ya juu,, wana wachezaji wenye uwezo wa kufungua defense line ya wapinzani,, ukipaki basi unakuwa umeruhusu mashambulizi mfululizo matokeo yake mnapigwa 8Dawa ya kule n kuwa defensive tu...tunamuacha mbele Baleke tu [emoji1787][emoji1787]
Kupigwa hamsa sio matokeo?Raja ameshafuzu na tayari yuko na uhakika wa kuongoza kundi. Mechi yake dhidi ya Simba haitakua na umuhimu wowote.
Atapumzisha wachezaji wake muhimu, na hatakua na molari ya kupambana. Simba wakikaza, wanaweza kupata matokeo!
Unazijua rekodi wewe?Rekodi ya kufungwa magoli mengi kwenye mechi moja (6) inashikiliwa na Gongowazi. Walifungwa goli 6 na Raja. Ni lazima tuweke rekodi sawa.
Wakuu
Nimeshindwa kabisa kuwa na amani, hii mechi ya marudiano na Raja pale kwenye dimba la Mohammed V Morocco inaninyima kabisa usingizi.
Kila nikikumbuka zile thalatha walizotupiga tukiwa full house hapo lupaso pia nikikumbuka bado tuna mechi ya marudiano tena kwao nanyong'onyea mpaka miguu inaisha nguvu.
Kimahesabu tutakuwa tayari tumeshafuzu quarter finals maana Horoya hana pa kutokea lazima avute pumzi ya moto, lakini kuhusu Raja haya mambo mimi naona kama yana zungumzika.
Tunaweza kukaa chini tukayazungumza sio lazima mpaka tuaibishane kiasi hicho tusifike huko bhna.
Nguvu moja [emoji881]