Mechi ya marudiano na Raja AC inaninyima usingizi

Mechi ya marudiano na Raja AC inaninyima usingizi

Usiwe na shaka, Simba atalinda heshma yake Morocco. Utaiona Simba ambayo haujawahi kuiona kwa muda mrefu.

Niliwahi kwenda Misri juzi juzi na katika pita pita zangu mitaani nilikuwa najitambulisha kama mwanasimba. Wakawa wanafurahi wakikumbuka tulichowafanyia Zamalek miaka ile.
Okwi alishawaduwaza Tunisia pia ,Kikosii kitapangwa hivi ..Golini Manula, Kapombe, ,Zimbwe,Kennedy,Onyango,Baka,Kanoute,Nyoni,Muzamiri,Kibu,Saidoo,
Hapo Hawatoboi..Kanoute akitolewa Kwa Kadi nyekundu anaingua Phiri!😁
 
Unatakiwa ujiandae tu kisaikolojia. Huna sababu ya kujinyima raha huku ukitambua fika kipigo cha mbwa mwizi hakikwepeki kwenye hiyo mechi yenu ya marudio.

Hivyo unachotakiwa kufanya siku hiyo ya mechi, ni kunywa tu maji mengi ili kupunguza presha ya mzunguko wa damu kwenye mwili. Hii ni kwa utaalamu wangu lakini.
Shukrani sana mkuu, nimeipokea hii
 
Watatunza energy ya mechi ya robo fainali. Hakuna kocha anayependa aingie katika mechi muhimu akiwa na wachezaji wanaokosa mechi kwa yellow au red cards au kwa majeraha
Tuombe iwe hivyo
 
Dawa ya kule n kuwa defensive tu...tunamuacha mbele Baleke tu [emoji1787][emoji1787]
Wale jamaa wana ufundi wa hali ya juu,, wana wachezaji wenye uwezo wa kufungua defense line ya wapinzani,, ukipaki basi unakuwa umeruhusu mashambulizi mfululizo matokeo yake mnapigwa 8
 
Rekodi ya kufungwa magoli mengi kwenye mechi moja (6) inashikiliwa na Gongowazi. Walifungwa goli 6 na Raja. Ni lazima tuweke rekodi sawa.
 
Raja ameshafuzu na tayari yuko na uhakika wa kuongoza kundi. Mechi yake dhidi ya Simba haitakua na umuhimu wowote.

Atapumzisha wachezaji wake muhimu, na hatakua na molari ya kupambana. Simba wakikaza, wanaweza kupata matokeo!
Kupigwa hamsa sio matokeo?
 
Rekodi ya kufungwa magoli mengi kwenye mechi moja (6) inashikiliwa na Gongowazi. Walifungwa goli 6 na Raja. Ni lazima tuweke rekodi sawa.
Shukrani mkuu,, kuna watu walishaanza kujisahaulisha..
 
  • Thanks
Reactions: Tui
Mara ya mwisho Gongowazi kushiriki CAF Chmpions league walimaliza na pointi ngapi?Jikumbusheni ilikuwa mwaka 1998.Au wengine mlikuwa hamjazaliwa?
 
Draw inaweza kupatikana. Ni kwenda na line up ya kimkakati ya 5-4-1 kama ile ya Pablo mwaka jana dhidi ya Orlando Pirates.. 1) Manula 2) Kennedy Juma 3) M Husein 4) Inonga 5) Onyango 6) Mwenda 7) Kapombe 8) Nyoni 9) Kibu 10) Kanoute 11) Mzamiru
 
Unakosa usingizi kivipi sasa,ndo matokeo ya Mpira kushinda,kushindwa na sare.
Simba haiogopi changamoto
 
Rekodi ya kufungwa magoli mengi kwenye mechi moja (6) inashikiliwa na Gongowazi. Walifungwa goli 6 na Raja. Ni lazima tuweke rekodi sawa.
Unazijua rekodi wewe?
1651580803.jpg
 
Wakuu

Nimeshindwa kabisa kuwa na amani, hii mechi ya marudiano na Raja pale kwenye dimba la Mohammed V Morocco inaninyima kabisa usingizi.

Kila nikikumbuka zile thalatha walizotupiga tukiwa full house hapo lupaso pia nikikumbuka bado tuna mechi ya marudiano tena kwao nanyong'onyea mpaka miguu inaisha nguvu.

Kimahesabu tutakuwa tayari tumeshafuzu quarter finals maana Horoya hana pa kutokea lazima avute pumzi ya moto, lakini kuhusu Raja haya mambo mimi naona kama yana zungumzika.

Tunaweza kukaa chini tukayazungumza sio lazima mpaka tuaibishane kiasi hicho tusifike huko bhna.

Nguvu moja [emoji881]

Mnaenda Kupakuliwa [emoji1787]
 
Unaweza kuandika ujinga na uzushi lakini haifuti ukweli.
 
Back
Top Bottom