Mechi ya marudiano na Raja AC inaninyima usingizi

XII Tz

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2020
Posts
4,345
Reaction score
7,076
Wakuu

Nimeshindwa kabisa kuwa na amani, hii mechi ya marudiano na Raja pale kwenye dimba la Mohammed V Morocco inaninyima kabisa usingizi.

Kila nikikumbuka zile thalatha walizotupiga tukiwa full house hapo lupaso pia nikikumbuka bado tuna mechi ya marudiano tena kwao nanyong'onyea mpaka miguu inaisha nguvu.

Kimahesabu tutakuwa tayari tumeshafuzu quarter finals maana Horoya hana pa kutokea lazima avute pumzi ya moto, lakini kuhusu Raja haya mambo mimi naona kama yana zungumzika.

Tunaweza kukaa chini tukayazungumza sio lazima mpaka tuaibishane kiasi hicho tusifike huko bhna.

Nguvu moja [emoji881]
 
Usiwe na shaka, Simba atalinda heshma yake Morocco. Utaiona Simba ambayo haujawahi kuiona kwa muda mrefu.

Niliwahi kwenda Misri juzi juzi na katika pita pita zangu mitaani nilikuwa najitambulisha kama mwanasimba. Wakawa wanafurahi wakikumbuka tulichowafanyia Zamalek miaka ile.
 
Raja ameshafuzu na tayari yuko na uhakika wa kuongoza kundi. Mechi yake dhidi ya Simba haitakua na umuhimu wowote.

Atapumzisha wachezaji wake muhimu, na hatakua na molari ya kupambana. Simba wakikaza, wanaweza kupata matokeo!
 
Hoyo mechi wala haitakuwa ngumu,hawawezi kuweka wachezaji wa maana coz washafuzu roboechi haina umuhimu kwao hiyo
 
Kama nitakua tayari nime-mpiga Horoya hapa kwa Mkapa, it means tayari nimepita. No worries

Ila kama matokeo yatakua tofauti na hayo, basi 2-4 zinatuhusu. Confidence itapotea kabisa, pressure itakua kubwa kwa wachezaji, Viongozi, mashabiki.

Believe me or not, kama tutakua tayari tumepita, basi tutashuhudia mechi moja safi sana(Raja Vs Simba). No Pressure, Just Football. No Vayolence, Just Football.
 
Usiwe na shaka, Simba atalinda heshma yake Morocco. Utaiona Simba ambayo haujawahi kuiona kwa muda mrefu.

Niliwahi kwenda Misri juzi juzi na katika pita pita zangu mitaani nilikuwa najitambulisha kama mwanasimba. Wakawa wanafurahi wakikumbuka tulichowafanyia Zamalek miaka ile.
Mkuu hawa ni Raja wanaotaka sifa, na sipati picha kama wale mashabiki wao wata ruhusiwa uwanjani full house
 
Raja ameshafuzu na tayari yuko na uhakika wa kuongoza kundi. Mechi yake dhidi ya Simba haitakua na umuhimu wowote.

Atapumzisha wachezaji wake muhimu, na hatakua na molari ya kupambana. Simba wakikaza, wanaweza kupata matokeo!
Tunaomba iwe hivyo mkuu, ila hawa jamaa kwenye lile dimba lao, wakikukosa sana 5
 
Hoyo mechi wala haitakuwa ngumu,hawawezi kuweka wachezaji wa maana coz washafuzu roboechi haina umuhimu kwao hiyo
Mkuu wale jamaa huwajui kwa kutaka sifa, huwa wanapenda kumaliza makundi na alama 18 na magoli ya kutosha hivyo usishangae aka kupangia full mkoko na kukupiga Hamsa plus
 
Wakuu

Nimeshindwa kabisa kuwa na amani, hii mechi ya marudiano na Raja pale kwenye dimba la Mohammed V Morocco inaninyima kabisa usingizi.

Kila nikikumbuka zile thalatha walizotupiga tukiwa full house hapo lupaso pia nikikumbuka bado tuna mechi ya marudiano tena kwao nanyong'onyea mpaka miguu inaisha nguvu.

Kimahesabu tutakuwa tayari tumeshafuzu quarter finals maana Horoya hana pa kutokea lazima avute pumzi ya moto, lakini kuhusu Raja haya mambo mimi naona kama yana zungumzika.

Tunaweza kukaa chini tukayazungumza sio lazima mpaka tuaibishane kiasi hicho tusifike huko bhna.

Nguvu moja [emoji881]
Unatakiwa ujiandae tu kisaikolojia. Huna sababu ya kujinyima raha huku ukitambua fika kipigo cha mbwa mwizi hakikwepeki kwenye hiyo mechi yenu ya marudio.

Hivyo unachotakiwa kufanya siku hiyo ya mechi, ni kunywa tu maji mengi ili kupunguza presha ya mzunguko wa damu kwenye mwili. Hii ni kwa utaalamu wangu lakini.
 
Mkuu hawa ni Raja wanaotaka sifa, na sipati picha kama wale mashabiki wao wata ruhusiwa uwanjani full house
Watatunza energy ya mechi ya robo fainali. Hakuna kocha anayependa aingie katika mechi muhimu akiwa na wachezaji wanaokosa mechi kwa yellow au red cards au kwa majeraha
 
Dawa ya kule n kuwa defensive tu...tunamuacha mbele Baleke tu [emoji1787][emoji1787]
 
Raja ameshafuzu na tayari yuko na uhakika wa kuongoza kundi. Mechi yake dhidi ya Simba haitakua na umuhimu wowote.

Atapumzisha wachezaji wake muhimu, na hatakua na molari ya kupambana. Simba wakikaza, wanaweza kupata matokeo!
Raja ata akiweka timu B...Tano ziko pale pale[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16]
 
Back
Top Bottom