Mechi ya pili tangu kuanza kwa ligi, lakini Mashabiki wa Yanga wanadhani zimebaki mechi mbili kumaliza

PakiJinja

JF-Expert Member
Joined
Jan 16, 2012
Posts
11,689
Reaction score
25,848
Kwa kiwango na mfumo wanaoenda nao Yanga tangu mechi za Majaribio msimu huu, hadi mechi za ushindani, ni ukweli ulio dhahiri kwamba Yanga ipo kwenye form nzuri sana.

Hali ikiendelea hivi kwa mechi tatu zijazo, basi walio chini itabidi wakaze buti tu na wamfuate hukohuko juu, kumsubiri chini itakua ni dua la kuku.

Pamoja na hayo, hali hii imeibua hamasa na furaha kwa mashabiki wa timu ya Yanga, kiasi cha wengi kujisahau na kudhani zimebaki mechi mbili ligi kuisha wakati ndiyo kwanza ni mechi ya pili.

Ni vyema sana kufurahia, ila ni vyema zaidi kuwa na akiba ya furaha na maneno, maana huu ni mchezo, wakati mwingine ushindi katika mchezo huu hautokani na ubora wa timu, bali makosa ya binaadam wote wanaohusika na mchezo, kuanzia wachezaji, waamuzi, viongozi wa timu, viongozi wa Chama Cha Mpira, viongozi wa kisiasa, afya, mashabiki n.k.

Alamsiki
 
Mzazi, huwa hangoji hadi afikishe mtoto wa 4 ndo afurahi. Anaanza kufurahia tangu mtoto wa kwanza, na kila anayefuata. Na kwenye kila namba, wakitokea mapacha (5G), furaha huongezeka..!!
 
Unaleta siasa, Mpira ni uwekezaji, kama hujaona uwekezaji uliofanywa na Yanga basi haya yanayotokea utadhani ni kubahatisha au yanakuja yenyewe.

Kumbuka Yanga imestruggle sana kipindi cha nyuma watu wapo uwanjani wanamtegemea Ditram Nchimbi na Molinga ndio wawape furaha huku benchi la ufundi mnategemea Mwinyi Zahera, tumeshatoka huko.
 
Mashabiki wa Uto ukimtoa Tate Mkuu , Kilimbatzz na LIKUD waliobaki awajielewi.

Frank Wanjiru kwisha Dr Matola PhD

πŸ‘† awa mashabiki wa Uto watata awaelewi somo hao.wazee wa kazi chafu.πŸ˜…πŸ˜‚
Huyu ni Popoma, siyo Mimi.

 
Pamoja na yote hayo,hatujawahi kuwa chini ya nafasi ya pili,hao wenzetu kuna mwaka almanusura washuke daraja tukawabeba.
 
Na tunakupelekea moto hukohuko mto msimbazszz
Utopolo ndio wanakaa kwenye mto unaofurika kila mwaka.
Simba ipo mjini kati Msimbazi street,ukitaka kwenda Airport ni karibu,ukitaka kwenda bandarini Dubai port pia ni karibu.πŸ‘πŸ‘πŸ˜‹πŸ˜
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…