Mechi ya Simba vs Yanga kupigwa Mei 10, 2025

Mechi ya Simba vs Yanga kupigwa Mei 10, 2025

Status
Not open for further replies.
Tungecheza tu na hiyo ya kmc kabisa maana tarehe 11 na 17 bado kuna kamuda na hapo bado mechi na utopolo nayo inahitaji maandalizi makubwa, japo kwa ratiba hiyo nawaza kama wachezaji bado watakuwa na energy ile ile au watakuwa washachoka sababu ya kucheza mfululizo, kocha angebadili kikosi kwenye zile mechi anazoona nyepesi maana hapo mechi ngumu zilizobaki ni za jkt, singida, na yanga tu hizo ndio za kupanga kikosi cha kwanza
Waombe tu hiyo ya KMC iahirishwe halafu za JKT na Pamba zisogezwe siku moja moja mbele. Kwa mtazamo wangu hiyo ndiyo itakuwa ratiba rafiki zaidi kwa Simba.
 
Nendeni muandamane kumpinga raisi wa team kwa kukubaliana na hili sasa kama mlivyokua mnaenda kushinda uwanja wa mpaka kupinga kikao. Mimi huwa siamini kama mnashaabikia kabumbu bila kuwa na mipaka hasa kwenye hizi timu zenu mbili kama mna akili timamu.
 
hakikisheni mnafanya maandalizi.

statment ya kitapeli hili tangazo ni uongo.
 
Ukiona mtu au Mchambuzi yoyote anakwambia Bodi ya ligi itapanga tarehe ya kuchezwa iyo mechi ujue uelewa wake ni finyu katika tasnia ya mpira wa miguu na mambo kwa ujumla.

Ilo jambo lipo katika ngazi ya Mahakama ya FIFA (CAS) hakuna mtu au mamlaka yoyote apa Nchini mwenye uwezo wa kuamua juu ya iyo mechi zaidi ya maelekezo kutoka CAS.
CAS ndio wata toa maamuzi baada ya kupitia shauri ilo na Bodi ya ligi ita takiwa itekeleze maamuzi ayo ya CAS.
 
I doubt sana kama hiyo ya KMC kama itachezwa maana kama Simba itaingia fainali nadhani itataka iwahi kidogo kwenda Morocco. Hakuna haja ya kuzikimbiza sana hizo mechi za ligi.

Simba ikichelewa kucheza mechi zake ni faida sana maana timu nyingi tayari zitakuwa zinajua nafasi zao kwenye ligi kwa hiyo labda wawe kauzu au vibaraka, wengi hawatakaza kihiiivyo.

Halafu hautaki kuingia kwenye risk ya kutoka sare au kufungwa na hatimaye kupoteza kabisa nafasi ya kuwa bingwa wa NBC kabla ya kwenda Morocco.
Sawa siyo mbaya maana nilidhani kupostpone haiwezekani, nilidhani simba italazimishwa icheze mechi zake hivyo hivyo ili kukimbizana na muda, ila kocha ajitahidi tu kubadili kikosi maana kikosi cha kwanza wengi wameshachoka
 
Ndio nafahamu hilo mkuu, tena umesahau na tarehe kumi na nne pia tuna mechi ya ligi na singida, nawaza tukifuzu fainali hivyo viporo sijui kama tutatoboa vyote na sijui tutavimaliza lini
Ni kweli binafsi mimi kama mwana SimbaSC napata hofu kwa namna vipori vinavyozidi. Kuna vitakavyochacha

SimbaSC NguvuMoja #UbayaUbwela
 
Sawa siyo mbaya maana nilidhani kupostpone haiwezekani, nilidhani simba italazimishwa icheze mechi zake hivyo hivyo ili kukimbizana na muda, ila kocha ajitahidi tu kubadili kikosi maana kikosi cha kwanza wengi wameshachoka
Jambo la kitaifa hili, TFF ni waelewa. Watu wanasahau kipindi kile Yanga ipo shirikisho ilikuwa inaahirishiwa mechi zake za Dar kwa wiki nzima wakati mechi inayofuata ya kimataifa nayo ipo Dar.

Hilo la kubadili kikosi ni muhimu. Uzuri Simba msimu huu ina upana wa kikosi.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom