Mechi za mwisho VPL,Vita ya ubingwa na kushuka daraja

Mechi za mwisho VPL,Vita ya ubingwa na kushuka daraja

Yanga bingwa mzee. Msimu ujao mikakati ni kutangazwa mabingwa Kabla ya mechi3 ligi kumalizika.
 
Hatuna shida na ubingwa wa Africa..mara ya 27 mabingwa
 
Hatimae Rais wa TFF kupitia kamati yake amefanikisha alichokitaka ili Yanga ipate Ubingwa.Hongera sana Jamali Malinzi naamini utazishawishi hata kamati chama cha Soka cha Afrika kuipangia timu dhaifu ili itwae Ubingwa wa Afrika.
Mezani fc, malalamiko ka MTT wa kambo fc
 
Klabu ya Simba imegoma kuchukua zawadi ya mshindi wa pili mara baada ya mchezo wake wa mwisho wa ligi kuu Tanzania bara dhidi ya Mwadui FC.

Licha ya ushindi wa Simba wa magoli 2-1 na kufikisha alama 68 sawa na Yanga ambayo imepoteza mchezo wake wa mwisho kwa kufungwa 1-0 na Mbao FC, bado Simba imejikuta ikimaliza katika nafasi ya pili kutokana na tofauti ya wastani wa magoli.

Baada ya mchezo wa Simba vs Mwadui kumalizika kwenye uwabja wa taifa, MC alitangaza kwamba timu ya Simba itapewa zawadi kulingana na nafasi waliyomaliza (ya pili) huku Yanga wakiwa wametwaa ubingwa wa VPL 2016/17.

Jambo la kustaajabisha ni pale viongozi na wachezaji kuonekana kutojali zawadi hiyo, walielekea vyumba vya kubadilishia nguo mara baada ya mchezo.

Walisubiriwa kwa dakika kadhaa lakini hawakutokea, walipoulizwa baadhi ya viongozi walijibu kwamba wachezaji wanabadili jezi walizochezea na kuvaa nguo maalum kwa ajili ya kwenda kupokea zawadi hizo.

Kadiri muda ulivyozidi kuyoyoma bado Simba waliendelea kusalia kwenye vyumba vya kubadilishia nguo na mara kadhaa wachezaji na viongozi walitoka na kurudi tena vyumbani.

Waandishi wa habari waliokuwepo uwanjani kwa ajili ya kushuhudia tukio hilo walianza kuondoka mmoja baada ya mwingine na kuwaacha wachezaji wa Simba wakiwa bado hawajatoka ndani ya vyumba vya kubadilishia nguo.
Hii ni ripoti au taarifa?
 
Simba bado itabaki kua timu bora msimu huu kama ilivyo kwa yanga japo kiviwango yanga kashuka ikilinganishwa na misimu miwili ilopita
 
Mpira wa kibongo shida sana, Liver na Sevilla fainali ya mwaka juzi mabeki wa Sevilla walinawa mpira kama mara 4 na Liver walishindwa ile fainali.

Lakini hakuna sehemu waliyolalamika. Wazia pale ingekua ipo timu kutoka bongo, kwanza refa angepigwa ngumi mpaka angejiuliza kua katika kazi zote duniani kwanini aliamua kua refa, no fck that, angejiuliza kwanini duniani kuna mchezo wa mpira.
 
Mpira wa kibongo shida sana, Liver na Sevilla fainali ya mwaka juzi mabeki wa Sevilla walinawa mpira kama mara 4 na Liver walishindwa ile fainali.

Lakini hakuna sehemu waliyolalamika. Wazia pale ingekua ipo timu kutoka bongo, kwanza refa angepigwa ngumi mpaka angejiuliza kua katika kazi zote duniani kwanini aliamua kua refa, no fck that, angejiuliza kwanini duniani kuna mchezo wa mpira.
Asante kwa kutujulisha kuwa wewe ni shabiki wa liverpool
 
Simba aibu tupu
IMG_0250.JPG
 
Na hilo litawakosti endapo huko FIFA wakifeli basi sheria itawatafuna. Hizo point wangekomaa ndani ya dakika 90 haya mambo yasingekuwepo ila tatizo wanataka mezani
 
Back
Top Bottom