Medali iliyopelekwa ikulu na Yanga SC inawatia Tumbo joto Simba SC

NALIA NGWENA

JF-Expert Member
Joined
Oct 6, 2016
Posts
11,297
Reaction score
14,588
Naaam! Medali ya fainali waliyoipata Yanga SC Baada ya Kucheza fainali kwenye michuano ya kimataifa (SHIRIKISHO) ni mzimu unaowatafuna Simba SC kwa kuwatia Hamasa, nguvu morali ya Kupambana ili kurejesha amani ya Mashabiki Wao Wenye ugwadu na uchu Wa kuona timu Yao imefika ama kuvuka hatua waliyoifika Yanga SC.

Timu inapopata medali ya kimataifa ni baraka kubwa sana na ni hatua kubwa kwa timu kubwa iliyoweka malengo Kabla msimu Kuanza.

Simba SC wanapresha kubwa sana kimataifa haswa Kila wanaposikia kelele za watani Wao Wa jadi (Yanga SC) wakiimba nyimbo ya "na Nyinyi mfike fainali kama tulivyofanya sisi"

Na ukiachana na presha ya kimataifa bado kuna presha ya Kuchukua kombe la Nbc, crdb, mbaya Zaidi Mpinzani wake Mkubwa (Yanga SC) Hana michuano ya kimataifa ana muda mwingi Wa kukabiliana na Simba SC kwenye mbio za ubingwa Wa NBCPL na Crdb.

Kwa Nini nasema Simba SC wanapresha na hawana kabisa furaha?!!

Kila nikitazama sura za Viongozi Wa Simba SC wakati Wa interview naona Kabisa zile mbwembwe na jinsi nilivyowazoea kwenye Hamasa zimekwisha kabisa yaani Kiufupi hawana amani.

Maoni Yangu: endapo Simba SC watatoka mapema kwenye michuano ya kimataifa pasi na kuingia hata nusu basi wakija kwenye michuano ya ndani wahakikishe wanachukua kombe na kumfunga mtani tofauti na hapo Mashabiki watagawana mbao pale MSIMBAZI.
 
Ikiwa unasema viongozi ndio hawana furaha,huenda ukawa sahihi,ila sisi mashabiki tutakuuliza kwa sasa Afrika Mashariki ( kama unazijua lakini nchi za Afrika mashariki) kuna timu gani ipo kimataifa?
Na kwa akili za vijana wa siku hizi walivyo vilaza hususan wa timu isiyojitambua huenda hata hujui kwamba ni Simba pekee ndiyo inawakilisha ukanda huu.
 
Tathmini mbovu inayotumia takwimu batili.

Kwanza, Yanga haina ubavu wa kumfunga Azam. Hilo tu linaonyesha ubingwa wa NBC bado hauna mwenyewe. Nataka derby ipangwe baada ya mechi ya Yanga vs Azam ndiyo itakuwa tamu zaidi.

Tumeamua tuwaonyeshe sura ya mbuzi ili msituelewe na kwa hii tathmini yako naona tunafanikiwa. Sisi bado tunajenga timu.
 
ENDELEA KUJIDANGNAYA
 
Mkuu naona umerudi na takwimu zako uchwara,
Medali gani za kuringia sasa kama ingekuwa kombe mmelibeba hapo sawa
 
Naaam! Medali ya fainali waliyoipata Yanga SC Baada ya Kucheza fainali kwenye michuano ya kimataifa (SHIRIKISHO) ni mzimu unaowatafuna Simba SC kwa kuwatia Hamasa, nguvu morali ya Kupambana ili kurejesha amani ya Mashabiki Wao Wenye ugwadu na uchu Wa kuona timu Yao imefika ama kuvuka hatua waliyoifika Yanga SC.

Timu inapopata medali ya kimataifa ni baraka kubwa sana na ni hatua kubwa kwa timu kubwa iliyoweka malengo Kabla msimu Kuanza.

Simba SC wanapresha kubwa sana kimataifa haswa Kila wanaposikia kelele za watani Wao Wa jadi (Yanga SC) wakiimba nyimbo ya "na Nyinyi mfike fainali kama tulivyofanya sisi"

Na ukiachana na presha ya kimataifa bado kuna presha ya Kuchukua kombe la Nbc, crdb, mbaya Zaidi Mpinzani wake Mkubwa (Yanga SC) Hana michuano ya kimataifa ana muda mwingi Wa kukabiliana na Simba SC kwenye mbio za ubingwa Wa NBCPL na Crdb.

Kwa Nini nasema Simba SC wanapresha na hawana kabisa furaha?!!

Kila nikitazama sura za Viongozi Wa Simba SC wakati Wa interview naona Kabisa zile mbwembwe na jinsi nilivyowazoea kwenye Hamasa zimekwisha kabisa yaani Kiufupi hawana amani.

Maoni Yangu: endapo Simba SC watatoka mapema kwenye michuano ya kimataifa pasi na kuingia hata nusu basi wakija kwenye michuano ya ndani wahakikishe wanachukua kombe na kumfunga mtani tofauti na hapo Mashabiki watagawana mbao pale MSIMBAZI.
IMG_20250330_155626.JPG

Kweli hamna akili.

Si mnasema kombe la Umiseta, luza na nini. Leo tena mnadai kutamaniwa na Simba na mnajivunia medali za kuwa luza katika kombe la luza.

Daah

Mnatuchosha bhana, tupumzisheni kidogo.
 
Kwenye mpira hakuna ushindi au ubingwa wa medali.
Kwenye mpira timu hujivunia mafanikio kwa kucheza robo, nusu, fainali na kuchukua kombe
Unaweza kuniambia Barcelena wanamedali ngapi?
Timu changa na mbovu duniani kuvaa medali kwao ni mafanikio makubwa sana
Medali kwenye mpira hazihesabiki ni kama kachumbari kwenye chakula kwahiyo huwezi kujivunia umekula pilau au ugali na kachumbari. Watu watakuona ni chizi
Hizo medali unaweza kumtambia Mamelodi? Watakuona ni tahira
Kama timu inaishia makundi lazima itambe imevaa medali.
Timu imefuzu kucheza robo fainal, msemaji wao akazimia. Ujue hivyo vitu ni vigeni kwao ndiyo maana ikaitwa utopolo fc
 
Back
Top Bottom