Kuna watu wanapenda ushabiki wa kiporojo porojo Ila wengine zinatushinda tunakaa kimya tu.
Mkuu hivi ni kweli hukuona yale matukio ya faulo ndani ya box ambayo kimsingi zilikuwa ni penati ambazo refa hakuziamua?
Angalia hii clip hapo mwishoni mchezaji wa Medeama aliwekewa mguu kwa mbele katikati ya box.
Ilikuwa ni faulo ila refa hakuiona
Angalia na hii faulo ya Aucho dhidi ya wachezaji wawili wa Medeama
Aucho alimsukuma mchezaji wa Medeama ili ku win mpira ambao ulipitiliza na kwenda jirani ya mchezaji mwingine wa Medeama ambapo Aucho akafanya faulo nyingine
Lakini refa kutokana na makosa ya kibinadamu hakuweza kutafsiri vyema tukio hilo
Njoo kwenye hii faulo ya wazi ya Baccka ambayo haikuamuliwa kwa adhabu yeyote na refa akaiacha ipite like nothing happened
Hapo bado sijaongelea ile incident ya Pacome kufanya faulo wakati anaenda kufunga bao la kusawazisha.
Sasa nyinyi watu ambao mnajinasibu kuwa hamna upande ndio tulitegemea muwe mbele kuongea moments kama hizi.
Lakini katika hali ya kustaajabisha tunaona unawadhihaki watu wanaozungumza matukio ambayo yalitokea kweli kwa kwa kuita porojo.
Ni ngumu sana kuwa neutral hii tuliijua na ndio maana hata wachambuzi wetu inawapa shida sana hii ishu.