benzemah
JF-Expert Member
- Nov 19, 2014
- 1,533
- 3,187
Kwa kiasi kikubwa mambo tunayoyafahamu yanajengwa (Shaped) na yale tunayoyaona na kuyasikia na jinsi tunavyoona na kusikia zaidi ndivyo yanavyozidi kutukaa akilini na kuwa sehemu ya maisha yetu.
Nilikuwa likizo siku za karibuni hivyo mara nyingi nyumbani nikiwa nafanya kazi ndogondogo nimekuwa nikisiliza redio
Kikubwa kilichonishtua sana na kunileta humu kuandika haya ni kiasi kikubwa na nguvu kubwa inayowekwa katika matangazo ya michezo ya kubahatisha.
Kwa sasa inaonekana kila kituo cha redio kina mchezo wake ambao wengine hutoa washindi kwa dakika kadhaa, kwa saa kadhaa, kwa siku na kwa wiki.
Kuna wale wanajiita MCHONGO PESA kuna wengine CHOTA MIHELA yaani hakuna pa kujificha.
Nimegundua pia matangazo haya yanakwenda pia kwenye TV na hata kwenye mitandao ya Kijamii
Mbaya zaidi ni nguvu kubwa ya ushawishi inayotumika kwenye hilo.
Mshindi anapigiwa simu mubashara na kueleza anavyoshiriki na kushinda ili kuwapa moto na motisha wengine ili kuwanasa.
Nafasi ya ushindi kwenye michezo yoyote ya kubahatisha ni ndogo sana.
na haipo kwenye udhibiti wako, ukifanya hesabu za PROBABILIYT utanielewa katika hili.
Hoja yangu hapa ni namna MEDIA zetu zinavyotumia nguvu kubwa kupandikiza mawazo ya kuishi kwa kubahatisha, kuishi kwa kubashiri na namna ambavyo hakuna mamlaka zinaona au kuingilia kusimamia na ku-regulate hili.
Inaweza kuwa mimi nawaza tofauti na wengi na hakuna tatizo lolote juu ya kinachoendelea, vipi wadau vipi ninyi mmeliona hili? na kama jibu ni ndio nini mtazamo wenu