Media zetu zinavyofunga akili zetu kwa minyororo ya michezo ya kubashiri

Media zetu zinavyofunga akili zetu kwa minyororo ya michezo ya kubashiri

Redio zilianzishwa kwaajili ya watu maskini, kaa ndani msikilize anayelipwa mshahara, matangazoya biashara yapo kwa ajili yako, Ndo maana namkubali sana Chibude#Wasafibet.
 
  • Thanks
Reactions: Ok9
Hivi Mamlaka zinaregulate hii michezo au watu wanajiendeshea tu
 
Wiki nzima redio free wamtoa matangazo ya kutuweka attention leo tar 15 kumbe jambo lenyewe ni mchezo wa bahati nasibu wanaita PAKUA.

Eti ni fadhila kwa wasikilizaji kwa kuleta bahati nasibu. Kweli?
Wamechelewa sana
 
  • Thanks
Reactions: Ok9
Ningelikua na mamlaka fulani ya juu nchi hii [emoji847] ningelipiga marufuku michezo yote inayo husiha bahati na sibu, sijui kamari ikiwemo kubeti vile vi dude vya wachina wanavyo weka 200 ili kucheza n.k nguvu kazi ya taifa ina lemazwa.
 
huku ukitoa ajira.
Ningelikua na mamlaka fulani ya juu nchi hii [emoji847] ningelipiga marufuku michezo yote inayo husiha bahati na sibu, sijui kamari ikiwemo kubeti vile vi dude vya wachina wanavyo weka 200 ili kucheza n.k nguvu kazi ya taifa ina lemazwa.
 
Sio kila radio msikariri radio za dini hazitangazi hizo taarifa mkuu msijitoe ufahamu.
Radio za dini ndio takataka kabisa, hawa wanatumia mwamvul wa sadaka kuibia watu kinyenyekevu, mamichango yasiyo na tija, kama hilo liredio maria ndio hovyo kabisa vipind vya michango daily mpka mtu unajiulza wanaoendesha hizi radio station walkuwa na malengo gani ya kuanzisha? Kama hawakuwa na mitaji si wangeacha tu?

Kuna vipndi vingi vya kulazimsha watu wahudhulie kwenye makongamano bila kusahau sadaka na michango hovyo kbsa
 
Kwa kiasi kikubwa mambo tunayoyafahamu yanajengwa (Shaped) na yale tunayoyaona na kuyasikia na jinsi tunavyoona na kusikia zaidi ndivyo yanavyozidi kutukaa akilini na kuwa sehemu ya maisha yetu.

Nilikuwa likizo siku za karibuni hivyo mara nyingi nyumbani nikiwa nafanya kazi ndogondogo nimekuwa nikisiliza redio

Kikubwa kilichonishtua sana na kunileta humu kuandika haya ni kiasi kikubwa na nguvu kubwa inayowekwa katika matangazo ya michezo ya kubahatisha.

Kwa sasa inaonekana kila kituo cha redio kina mchezo wake ambao wengine hutoa washindi kwa dakika kadhaa, kwa saa kadhaa, kwa siku na kwa wiki.

Kuna wale wanajiita MCHONGO PESA kuna wengine CHOTA MIHELA yaani hakuna pa kujificha.

Nimegundua pia matangazo haya yanakwenda pia kwenye TV na hata kwenye mitandao ya Kijamii

Mbaya zaidi ni nguvu kubwa ya ushawishi inayotumika kwenye hilo.
Mshindi anapigiwa simu mubashara na kueleza anavyoshiriki na kushinda ili kuwapa moto na motisha wengine ili kuwanasa.

Nafasi ya ushindi kwenye michezo yoyote ya kubahatisha ni ndogo sana.
na haipo kwenye udhibiti wako, ukifanya hesabu za PROBABILIYT utanielewa katika hili.

Hoja yangu hapa ni namna MEDIA zetu zinavyotumia nguvu kubwa kupandikiza mawazo ya kuishi kwa kubahatisha, kuishi kwa kubashiri na namna ambavyo hakuna mamlaka zinaona au kuingilia kusimamia na ku-regulate hili.

Inaweza kuwa mimi nawaza tofauti na wengi na hakuna tatizo lolote juu ya kinachoendelea, vipi wadau vipi ninyi mmeliona hili? na kama jibu ni ndio nini mtazamo wenuView attachment 2297763
Mkuu unatakiwa kuelewa kuwa media zinatumia michezo ya kubashiri kutega waskilizaji kutokana na kuwa wasikilizaji wa redio wamepungua sana kutokana na mabadiliko ya kidijitali
 
Back
Top Bottom