Meeting with Mr. President

Meeting with Mr. President

Sasa kama waandish wa habari wanapangwa kwenye groups za wanne wanne je hiyo ni press conference au kitu gani? Je waandishi wa habari wenyewe ni wangapi? Maana wakiwa let say 32 na kila group likachukuwa 1/2 hour then rais itabidi atumie masaa 4 kuwaeleza wandishi alichowaitia na itabidi arudie hiyo taarifa yake mara 8. What a waste of time!!! Kweli USANII sasa umefikia mahali pake!!!!
 
He, sijui kama THISDAY na Mwanahalisi wapo, maana Mwanahalisi leo hata mitaani halipo....

Halisi, nitashangaa sana kama hujui kwamba THISDAY na Mwanahalisi hawajaalikwa. Angalia source zako kaka
 
kwaherini nijiandae kwenda "kunywa chai na kuangalia makochi ya ikulu." maana hizi foleni za bongo haziaminiki
 
He, sijui kama THISDAY na Mwanahalisi wapo, maana Mwanahalisi leo hata mitaani halipo....

hat mimi sijaliona,Kuna mtu an infomation what went wrong?Kiranja kama ni kweli mkuu wa kaya kafanya hivyo basi hii nikashfa nzito,Ukipewa pesa tafadhali njoo utuambie.
Mie niko tayrai kuwalipa Waandishi wote walio na shida ya pesa ila waandike ukweli.
 
Naona mnazozana kama watoto wadogo.Kikubwa ni hiyo hotuba ya JK.Kama itakuwa ya kunywa chaina kuangalia fenicha,tufanye subira ili tusikilize nini atakalosema.
 
Jamani, nilikua huko, kimefanyika kituko, Ikulu wamegawa makundi mya watu wanne wanne, sisi tumerudishiwa getini tumepangiwa muda mwingine (sitaji muda watanijua)... kwa hiyo hiyo ndio hali halisi, kwamba leo kutwa nzima Rais atakua na kazi ya kuzungumza na waandishi wa habari

Labda kuna zawadi za Christmas toka US, Naona this time walengwa ni waandishi.
 
Kuhusu kutokuwepo kwa MwanaHalisi mtaani leo ni kuwa nilikuwa naongea na news dealers pale lilipo jengo la ILO karibu na Raha Towers,akaniambia kuwa MwanaHalisi wameamua kuachia siku ya Jumatano kwa Raia Mwema kwani imefika mahali wasomaji wanachanganyikiwa ifikapo jumatano wanunue gazeti lipi,ila kuanzia kesho Alhamisi litakuwa mtaani katika siku hiyo kila wiki.My take ni kuwa soon we'll bid farewell to our erstwhile critical weekly newspaper RAI...hizo ndizo habari nilizozipata asubuhi na mchana huu...
 
Jamani, nilikua huko, kimefanyika kituko, Ikulu wamegawa makundi mya watu wanne wanne, sisi tumerudishiwa getini tumepangiwa muda mwingine (sitaji muda watanijua)... kwa hiyo hiyo ndio hali halisi, kwamba leo kutwa nzima Rais atakua na kazi ya kuzungumza na waandishi wa habari

Dah,

kiranja nadhani sasa utakuwa umeniona! Mi ni mmojawapo wa waliopigwa stop. Imenisikitisha lakini si mbaya sana; that's the way it is. Kama umefanikiwa kuingia tafadhali keep other folks informed. Nimeondoka eneo husika na sikupenda kuandika nikiwa maeneo hayo.

Invisible
 
duh, Au wameshakugundua unatoka Jambo forums?sooo..ngoja tusikie litakalojiri,labda Hasara atatupa yatakayojiri
 
Vituko na maajabu ya Mussa, huyu ndiye rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania. Anaona aibu hata kuongea na waandishi wote wa habari kwa mara moja kwani hoja ikipamba moto hataki wengine wakoleze. Hiyo ndio style mpya ya kugawa bahasha, courtesy ya EL na RA na bado mwaka huu tutaona mengi.

Maji yakimwagika hayazoleki.

Hiyo ni 'strategy' yenye maana yake. Pengine ni kutaka kuwafahamu na kuwa'identify' wahusika kutokana na 'feed-back' ya kiaina fulani. Sijui kama mbinu hiyo inamaana yoyote kwa nyakati hizi.
 
Halisi, nitashangaa sana kama hujui kwamba THISDAY na Mwanahalisi hawajaalikwa. Angalia source zako kaka

Basi, inapofikia hapo, ndio ujue mambo yanaanza kuwa magumu. Ina maana Watu wanaanza kukimbia vivuli. Uwazi na takataka zote tupilia mbali, nje ya dirisha. Si ajabu hata biashara ya matangazo ya serikali hao hawapewi. Nao waanze kudai haki yao kama ni walipa kodi. Wasibaguliwe.
 
Hivi hiyo Press confrence inachukua muda gani? Maana sasa tunachoka kusubiria!!!
 
Hivi hiyo Press confrence inachukua muda gani? Maana sasa tunachoka kusubiria!!!

Waaalikwa wameshikwa na bumbuazi kwani brown envelope zimekuwa kubwa kiasi cha kutisha, lazima ufahamu unapouza nchi bahasha zinakuja kwa namna yake ati!
 
Ilikua kazi kweli kweli, maana tulipofika kundi letu lilikua la nne, ama la mwisho, lakini baada ya makundi mawili kuingia, wakiongozwa na TUT (TVT na RTD) na wale watu wa ma-TV... baadaye sasa baada ya makundi mawili ya kwanza kumaliza, muda ulikua umekwisha ikaamuliwa sasa nakundi mawili ya mwisho yaingie pamoja.

Lakini kwa sababu za kitaaluma, tumeambiwa kwamba kilichojadiliwa humo kitaruhusiwa kurushwa hewani ama kuchapishwa Ijumaa ya Desemba 21, na si kabla ya hapo kwa hiyo tunaskikitika kwamba inabidi tusubiri. THISDAY si kama hawajaalikwa, nadhani ni tatizo la "MAWASILIANO" kati yao na wenzao wa "The Guardian Limited" kule Mikocheni ambako "mwaliko" ulipelekwa. Hata hivyo swali ambalo halina jibu ni kwamba je, press release zote huwa zinapelekwa Mikocheni ziliko ofisi za The Guardian ama huwa zinapelekwa Posta Mpya zilipo ofisi za THISDAY? ALAMSIKI
 
Mama yangu,

Yaani rais anaitisha press conference halafu anatoa mkwala habari zisichapishwe mpaka siku fulani? Anawafanya waandishi kama wanae, hata hao mababa wanoko siku hizi inabidi kuieleza kwa watoto zao.

By the time this "news" will be out it will be stale.Hii inaonyesha hamna cha maana kilichosemwa, huwezi kuwa na habari muhimu ukawapa waandishi halafu ukawaambia wasubiri siku kadhaa.

Utumbo mtupu!
 
loooooo,kweli hapa ni kiboko,wenzeni walialikuwa kula chrismas na mheshimiwa wametoka vitumbo dididi,kweli shibe ni mwanamalegeza
 
Mama yangu,

Yaani rais anaitisha press conference halafu anatoa mkwala habari zisichapishwe mpaka siku fulani? Anawafanya waandishi kama wanae, hata hao mababa wanoko siku hizi inabidi kuieleza kwa watoto zao.

By the time this "news" will be out it will be stale.Hii inaonyesha hamna cha maana kilichosemwa, huwezi kuwa na habari muhimu ukawapa waandishi halafu ukawaambia wasubiri siku kadhaa.

Utumbo mtupu!

Kitaaluma hiyo inaruhusiwa. Si kosa hata kidogo na ndio maana waandishi wanaielewa. Lakini haikua na maana kwani wangeweza kufanya mahojiano na kuandika kwa siku waitakayo. Pia taarifa inayozuiwa mara nyingi huwa si Press Conference bali taarifa, hotuba ama habari na hiyo ni kwa ajili ya kulenga malengo mahsusi mfano unapewa hotuba ya Rais ya mwaka mpya siku tatu kabla, na unasubiri hadi aisome na wewe kuilinganisha na ile uliyopewa kabla na anapomaliza tu, na wewe unairuhusu ama itoke katika gazeti ama website yako ama radio/TV ambayo haikua ikirusha live na kadhalika.
 
Mzee hii inaruhusiwa na ni kawaida kwetu tu. In fact kwa wenzetu mambo ambayo kiongozi anaongea huwa wanakuwa wanayo na yanatoka kwenye vyombo vya habari (in key issues) hata kabla ya hiyo press conference yenyewe. Utasikia wanasema kwa mfano kuwa "Rais atasema hivi na vile. Sasa kama na nyie waandishi wa habari mnakubali kutoa habari siku ambayo wanasiasa wanataka ujue tunashida kuliko tunavyoweza kufikiri na kueleza!
 
Sasa kama hiyo habari ilitakiwa iwe ya Ijumaa angeitoa Ijumaa! Sasa kwa vile sisi wengine hatufungwi na masharti hayo tukiidokeza hadharani itakuwaje?
 
Back
Top Bottom