Mfano sasa ndiyo nimekuwa His Exellency Mr. President
Tate Mkuu , Ningejenga vyuo vya ufundi stadi kila kata nchi nzima ili kuwapa vijana wengi elimu ya ujitegemea. Hii mambo ya shule za kata ni kuwapotezea tu muda watoto wa kitanzania. Mtoto anateswka miaka 4 shuleni, halafu anaishia tu kupata divisheni 0.
Ningehakikisha naboresha maisha ya wafanyakazi kwa kuwapa stahiki zao kwa wakati. Mfano kupanda madaraja, nk. Ili wafanye kazi kwa moyo na morali kubwa.
Kuboresha kilimo kutoka cha jembe la mkono mpaka kilimo cha kisasa cha umwagiliaji! Haiwezekani nchi imezungukwa na mito, maziwa, bahari, mabwawa! Halafu kilimo kinategemea mvua zisizo tabirika.
Na ningekuja na sera moja iliyoenda shule ya kuhamasisha sekta binafsi kujenga viwanda vya kutosha vya kuongeza thamani bidhaa zote zitokanazo na kilimo!
Kwenye sekta ya viwanda ndiyo usiseme! Ningeingia mikataba yenye maslahi kwa nchi na Mabeberu ya kujenga viwanda mbalimbali vikiwemo vya nguo, kua assemble mashine mbalimbali, nk.
Kwa wafanyabiashara ningehakikisha nawatoza kodi ndogo na rafiki ili wazalishe kwa wingi, wapate faida kubwa na pia kulipa kodi kwa hiyari na pasipo kutumia kile kikosi kazi!
Kwenye demokrasia ndiyo usiseme! Ningefungua milango ya demokrasia ya kweli na uhuru wa habari ili kukomesha vitendo vya rushwa, ufisadi na uhujumu uchumi!
Ningejenga mfumo imara wa utawala huru na unao jitegemea! Katiba mpya na tume huru ya uchaguzi ingekuwa ndiyo msingi wa uongozi wangu makini!!
Kuhusu miundombinu, ningejenga kutegemeana na bajeti iliyopo! Ni upuuzi kuwaumiza wananchi eti wajibane kwa kisingizio cha kujenga miundombinu huku wewe mwenyewe ukiishi peponi.
Niendelee?