Mehmet Ali Agca ni nani?

Mehmet Ali Agca ni nani?

bryan2

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2016
Posts
3,323
Reaction score
4,679
Mehmet Ali Agca ni Raia mwenye Asili ya Uturuki Aliyefanya Jaribio la Kutaka Kumua Mtakatiku PAPA JOHN PAUL II tarehe 13/5/1981.

Katika Jaribio hilo Mehmet alifyatua Risasi nne kutoka kwenye Pastola yake pale Pope John Paul II alipokua akisamilia waumini katika kanisa la Mt Petro Vatican Italy na mbili kumpata Kwenye Utumbo wake na nyingine kumjeruhi mkono wa kulia na kushoto na kusababisha Papa Kupoteza damu kwa sana

Pope aliwahishwa hospitali na kutolewa Risasi kwenye utumbo wake na kupata nafuu na baadaye kupona Kabisa

Mehmet alikamatwa na kuhukumiwa kifungo cha Maisha na Mahakama ya Italia na alipokua mahabusu Papa John Paul II alimtembelea na kufanya Maongezi na Mehmet

Papa alitangaza kumsamehe Mehmet na kuandika Barua kwa Raisi wa Italy kumwombea msamaha ambapo ombi lake lilifanikiwa na Mehmet kusamehewa na kurudi kwao Uturuki

Isitoshe Papa John Paul II aliitembelea familia ya Mehmet na Kuongea na Mama na Kaka zake.

Pia Mwaka 2005 baada ya Pope John Paul wa II kuugua Mehmet alimwandikia barua Akimtakia Papa aweze kupona Haraka.

Kwa kifupi sana huyo ndo Mehmet Ali Agca.

Tafakari ni Wangapi wameweza kuwasamehe wenzao ambao wamewakosea kwa Namna Moja au Nyingine?

Muwe na Jumapili Njema Ndugu Zangu.
 
HUYU HAPA
upload_2016-11-6_17-4-43.jpeg
 
Hapa nimejifunza aliemfunga Papy Kocha amsamehe buuuuuure
 
Back
Top Bottom