Mei Mosi 2020: Rais Magufuli atuma salamu za siku ya wafanyakazi, asisitiza waendelee kufanya kazi na kujiepusha na Corona

Uongezewe maslahi wakati katika hali ya namna hii kuna kupunguzwa kazi, kukatwa mishahara maeneo mbalimbali duniani?

Kama miaka minne iliyopita alishindwa kuwaongezea maslahi yenu, sahau hilo kwa sasa. Dunia inapigana vita ya kiuchumi, hakuna nchi itaongeza maslahi ya watu wake, sana sana muombe mifuko ya jamii iweke recovery package kwa ajili ya wafanyakazi kipindi hiki kigumu, walau 20% ya savings zenu.
 
Heading inasema...
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Content ni pongezi kwa wafanyakazi, pongezi kwa waajiri, wito wakuchapa kazi na tahadhali za Corona.

Hapa saivi nahangaika kuigeuza hiyo karatasi nisome ujumbe uliopo kwa nyuma, nataka kujua vyombo vya habari vimepewa taarifa gani.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huo ujumbe ukiuchunguza kwa makini utaelewa kuwa huo ulipaswa kuwa ujumbe wa siku ya afya na sio mei mosi maana hauna uhusiano hata kidogo na sikukuu ya wafanyakazi (mei mosi) ujumbe ulitakiwa kuzungumzia masrahi na changamoto za wafanyakazi na hatua ambazo serikali itazichukua

Sasa mie nashangaaa ujumbe umejaa Corona, Corona, Corona, Corona, Corona, Corona, covid 19 kuogopeshana tuu badala wafanyakazi wapewe hope unawajaza tena mi-stress

Kweli umeweza kutupiga chenga na watz naona wamehama badala wajadili mei mosi na wafanyakazi wanajadili covid 19 #tumekuelewa mkubwa, maana umezijua akili zetu zilivyo na umejitahidi kucheza nazo vizuri
#kama sio Corona sijui Leo ingekuwaje

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyo bingwa mtoro kazini mwambieni arudi kazini magogoni sheria ya divisheni ya kazi inasema ukiwa mtoro kazini kwa siku tano mfululizo na hujatoa taarifa kwa mwajiri wako huna kazi sasa sisi wananchi ambao ndo waajiri wake hajatuomba ruhusa Wala Nini hukohuko uliko huna kazi ww

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tumelimia meno hasa kwa miaka minne na usher,tumechapa kazi ila watawala wetu bado hawana cha kutupatia.Hata kupandishwa vyeo ni mbinde,ajira hakuna na mazingira magumu ya kazi ila hakuna maslahi.

Sawa jamaa wametimiza yote waliyoyapanga wamenunua ndege,wanajenga reli,wanajenga Stiegler dam,madaraja na vivuko vinaendelezwa kwa cash money na kununua wapinzani ila likija suala la maslahi ya watumishi/wananchi utasikia serikali haina fedha tuongeze uzalishaji.

Ukistaajabu ya Utawala huu unaweza kuugua mawazo.
 
Ni kweli lakini Mbona yeye achapi kazi bwana .arudi ikulu
 
Asente Rais Magufuli umekuwa nahodha bora kwa watumishi wa umma

Tukienda maofisini tunasikilizwa bila kutishiwa na vitambi
 
Huyo Ndio Rais tumpendaye ni nahodha bora

Nahodha bora hawezi kukizamisha chombo chake majini! Ajitokeze hadharani aje aongoze mapambano badala ya kujificha kijijini na kukiacha chombo kijiendee chenyewe. Hii Corona inasafiri kama umeme! Itamtafuta tu kokote kule alikokimbilia.

Labda atubu hadharani dhambi zake zote alizotutendea kwa miaka yote hii 5! Huenda atasamehewa.
 
JK umtuharibia nchi !!
Laana imeingia nchini.
Ulishindwaje kutupigania mpaka tumepata garasa?
Huyo JK mlimsema vibaya kuliko hata huyu na huyu akitoka mtamsema ajaye na kusema bora huyu...FANYA KAZI nchi yako bad changa
 
Asente Rais Magufuli umekuwa nahodha bora kwa watumishi wa umma

Tukienda maofisini tunasikilizwa bila kutishiwa na vitambi
Eti e
Ofisi gani umeenda karibuni na umefuatilia wangapi huenda huko na kuhudumiwa ipasavyo kama unavyodai??
Usiwasemee wengine sema kivyako

IF:X=WanaUFIPA+wanamaendeleo,Y=WanaLUMUMBA.
THUS:X=MABADILIKO
Y=WACHUMIA TUMBO!!
 
Maslah sahau

IF:X=WanaUFIPA+wanamaendeleo,Y=WanaLUMUMBA.
THUS:X=MABADILIKO
Y=WACHUMIA TUMBO!!
 
Nilifikiri atakuja na kauli juu ya wafanyakazi wa sekta binafsi wanaochishwa kazi kiholela na kuzuiwa malipo yao kipindi hiki,pia mpango madhubuti wa kumpa relief mfanyakazi katika kipindi hiki.
Huko kijijini kwake chato anafanya nini hataki kurudi ofisini?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
"Endeleeni kukaza mikanda"
Mi nafikiri maneno hayo tu yangetosha kwenye Salamu zako!!

IF:X=WanaUFIPA+wanamaendeleo,Y=WanaLUMUMBA.
THUS:X=MABADILIKO
Y=WACHUMIA TUMBO!!
 
Rikizo haijaisha atoke huko kyato aje mjini tuendelee kupambana Wote
"Endeleeni kukaza mikanda"
Mi nafikiri maneno hayo tu yangetosha kwenye Salamu zako!!

IF:X=WanaUFIPA+wanamaendeleo,Y=WanaLUMUMBA.
THUS:X=MABADILIKO
Y=WACHUMIA TUMBO!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…