Mei Mosi 2020: Rais Magufuli atuma salamu za siku ya wafanyakazi, asisitiza waendelee kufanya kazi na kujiepusha na Corona

Hakuna hata pole ya mdomo kwa wafanyakazi ! Hata kama kuna Corona lakini ikumbukwe kwamba hii sikukuu imo ndani ya kalenda ya dunia .

Tunatambua changamoto ya mikusanyiko , lakini je hata kusambaza waraka wa matumaini nayo imeshindikana ? Nawalilia wafanyakazi wa Tanzania .

Kama nimepitwa basi nisamehewe .
 
Rais Magufuli ameshatoa salamu za pongezi kwa niaba ya wananchi wote asubuhi ya leo!
 
Ila mishahara imeongezwa. At least tushukuru kwa hilo.
ikiongezwa kimyakimya nani atajua? kama ni hivyo ujue unaibiwa, mishahara inatakiwa kutangwa ili kila mmoja tujue! Maana mishahara yao ni kodi zetu!
 
ikiongezwa kimyakimya nani atajua? kama ni hivyo ujue unaibiwa, mishahara inatakiwa kutangwa ili kila mmoja tujue! Maana mishahara yao ni kodi zetu!
😂 nilikuwa natania. Jamaa wana hali ngumu, nasikia hata hela ya kulipa mishahara ni shughuli.
 
Ndivyo mlivyo mmejawa na unafiki saaana mnaumia mkiulizwa mnasema hapana tuko fit shenzy kabisaa
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Rais Magufuli timepokea salamu zako sisi wafanyakazi wako.
Tumependa zaidi pale uliposema huu ugonjwa wa COVID 19 ambao unaitikisa dunia usiwe sababu ya kutokuchapa kazi vizuri.
Tutachapa kazi, ila nasisi tunasema kuwa Ugonjwa huu wa corona usiwe sababu ya kutokutupandishia mshahara kwa miaka 5 mfululizo.
Asante
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…