Mei Mosi: Dkt. Mpango asema Serikali imepokea hoja ya kuboresha kikokotoo kwakuwa wafanyakazi hawaridhishwi na kanuni zake

Mei Mosi: Dkt. Mpango asema Serikali imepokea hoja ya kuboresha kikokotoo kwakuwa wafanyakazi hawaridhishwi na kanuni zake

Sa100: Hata msipoichagua CCM, Bado itaunda Serikali.
 
Wameshindwa kuboresha usafiri wa mwendo Kasi kati ya kivuko hadi kimara na mbezi kwa miaka 4 aliyokaa,, hawezi vitu vingine vikibwa
Si afadhali ya Mama at least ameongeza mishahara na kuirudisha annual Increment kuliko lile shetani lenu la Chato lilikusanya kodi zetu likagoma kutupandisha mishahara na madaraja kwa miaka 6!
 
poleni sana watumishi kwa manyanyaso mnayopitia ila niwakumbishe hatma ya maiaha yenu na pesa zenu zipo mikononi mwenu inategemea umenielewaje
 
Anasubiria mwakani kwenye May Mosi kutoa rushwa ya uchaguzi na kufanya propaganda ya kura
 
Alishasema kupitia mpango au umekataa kukubali? Baada ya kazi Fanya shughuli zako kujiongezea kipato utakufa wewe
 
Fuatilia kinachojiri kwenye Maadhimisho ya siku ya Mei Mosi Kitaifa, Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Arusha, leo Mei 1, 2024


Maadhimisho haya yamehudhuriwa na Makamu wa Rais, Philip Mpango, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Spika wa Bunge Tulia Ackson, Mawaziri pamoja na viongozi wengine wa Serikali.

KATIBU MKUU TUCTA, HERI MKUNDA
Akizungumza kwenye Sherehe hizo, Katibu Mkuu TUCTA Heri Mkunda amesema maboresho ya mishahara iliyofanyika bado haijakidhi mahitaji ya wafanyakazi, hivyo vinapaswa kuboresha kwani gharama za maisha zimepanda sana.
View attachment 2978185
Amesema wanatambua uwepo wa nyongeza ya 23.3% ya kima cha chini cha mshahara iliyofanyika, lakini inafaa ongezeko hili lizingatie pia wafanyakazi wengine.

Aidha, wafanyakazi wanaolipwa kwa mapato ya ndani ya halmashauri wanalalamika kutokulipwa maslahi yao kwa wakati kwani uwezo wa halmashauri unatofautiana. TUCTA inapendekeza wafanyakazi wote wa halmashauri kulipwa kutoka Serikali kuu ili kuondoa ubaguzi.

Kuhusu kikokotoo, wafanyakazi hawaridhishwi na namna kinavyofanyika na kimeleta malalamiko mingi. TUCTA inashauri kanuni za ukokotoaji mafao ziboreshwe ili kuleta manufaa kwa wafanyakazi.

Mambo mengine aliyozungumza ni kuongezewa likio ya miezi 3 kwa wanawake waliojifungua watoto njiti pamoja na kupitishwa kwa kitita kipya cha bima ya NHIF bila kushirikisha wafanyakazi kupitia vyama vyao hivyo kuzua taharuki. TUCTA inapendekeza wafanyakazi washirikishwe kwenye maboresho haya ya kitita.

DKT. PHILIP MPANGO, MAKAMU WA RAIS
Dkt. Mpango amewapongeza wafanyakazi kwa kazi kubwa wanayofanya.

Changamoto za kitita cha NHIF imezungumziwa pia. Dkt. Mpango amesema hatua za uboreshaji bado zinaendelea na vyama wahusika wote watashirikishwa.

Aidha, Serikali inasisistiza kuwa likizo ya uzazi ni haki ya mfanyakazi hivyo inapaswa kuwa siku 84 kwa mtoto mmoja, siku 100 zaidi ya mtoto mmoja na iwapo mfanyakazi atajifungua mtoto njiti, kipindi cha uangalizi hospitalini hakitahesabiwa kama likizo, na likizo rasmi itahesabika pindi madaktari watakapoona mtoto amemaliza kipindi cha uangalizi maalumu.

Serikali imepokea ushauri wa kuboresha kanuni za uboreshaji wa kikokotoo, hivyo imepokea hoja ya kuboresha kikokotoo kwakuwa wafanyakazi hawaridhishwi na kanuni hizo. Uamuzi wa kubadili ni lazima utazingatia ushauri wa watakwimu bima na vyama vya wafanyakazi kama TUCTA.

Kuhusu nyongeza ya mishahara, Serikali imesema ikiwa hali ya uchumi itaendelea kuimarika kama ilivyo sasa itatoa neno la faraja kwa wafanyakazi muda si mrefu.

====

Pia soma:

Kwanini Rais Samia kakwepa Hoja za Wafanyakazi na kamtuma Makamu wa Rais wakati Rais wa zanzibar yeye amevunja ziara kwa ajili ya Mei Mosi?

Rais Samia hajaonekana kwenye Sherehe za Mei Mosi, yuko wapi?

Tabiri yatakayotokea Mei Mosi 2024 Arusha

Paul Makonda awatengea barabara moja wajasiriamali maalumu kwa ajili ya kufanyia biashara zao siku ya Mei Mosi

Rais Samia mgeni rasmi Mei Mosi mkoani Arusha, maandalizi yafana

Rais Samia naomba ukemee ubaguzi kwenye sherehe za Mei Mosi

Mei Mosi: Upo uhusiano kati ya maslahi Bora na mfanyakazi kuwa na kitambi?

Mei Mosi: Wafanyakazi Zanzibar kuongezewa Tsh. 50,000 kama posho ya nauli

Kitu kikubwa na cha msingi amezungumzia Yale mahesabu ya Pensheni yanayofanywa na wabobezi wa hesabu actuarial, lakini cha kushangaza wakurugenzi wa mifuko karibu yote ilikuwa inaongozwa na wakurugenzi ambao sio wabobezi wa hesabu za pesheni na mambo ya bima, matokeo yake vitega uchumi wa mashirika hayo haya kufuata hizo hesabu matokeo yake wafanyakazi ndio wanateseka na viongozi wa mashirika hayo kushangilia
 
Back
Top Bottom