Mei Mosi: Wafanyakazi wa Tanzania Tutafakari Kama Tunayosababu ya Kusherehekea

Stuxnet

JF-Expert Member
Joined
Feb 12, 2011
Posts
18,875
Reaction score
29,427
Nakumbuka hata Rashid Kawawa alikuwa ni Secretary General wa Tanzania Federation of Labour wakati wa Ukoloni miaka ya mwisho mwisho kabla ya uhuru. Hata JK Nyerere alitumia platform ya Rashid Kawawa kwenye vyama vya wafanyakazi kuweza kuijenga TANU. Mkoloni alitambua haki za vyama vya wafanyakazi kwa kuvifanya kuwapo mahali pa kazi na kufanya shughuli zake ikiwa ni pamoja na MIGOMO.

Nimeshuhudia sherehe nyingi sana za Mei Mosi throughout awamu zote 5. Kwenye awamu ya 4 tutamkumbuka Nicholas Mgaya alivyokuwa anaipelekesha Serikali kwenye kudai haki za wafanyakazi na kuhamasisha MIGOMO. Munielewe MIGOMO kwa vyama vya wafanyakazi siyo jinai bali ni mchakato unaotambuliwa kwenye Sheria za vyama. Na tulishuhudia namna Serikali ilivyokuwa inatii nguvu ya TUCTA kwa marekebisho ya mshahara au kwa maboresho ya mazingira ya kufanyia kazi

Kwa miaka hii 5 yafuatayo yamefanywa dhidi ya wafanyakazi wa Tanzania na TUCTA iko kimya:-

1. Wamewaondoa wafanyakazi kwa kisingizio cha "vyeti feki" kinyume cha Sheria na TUCTA haija watetea. Zoezi la vyeti feki ni magumashi matupu wala msilitetee. Mbona halikupita JW na POLISI.

2. Serikali haija pandisha mshahara ya wafanyakazi kukidhi hali ya uchumi na uzalishaji kwa kisingizio cha kujenga miundombinu kwa miaka 5 sasa.

3. Serikali imewaondoa wafanyakazi wengi kwa kisingizio cha kutumbua bila kufuata Sheria za kazi na Utumishi.

4. Wafanyakazi wamekuwa wanahamishwa kwenda Dodoma bila kupewa posho stahiki.

5. Wafanyakazi hawajapandishwa madaraja wala kupewa posho ziendanazo na madaraja hayo.

TUCTA huendeshwa kwa michango ya wafanyakazi ambayo wanakatwa kila mwezi kama mchango. Lengo la kutoa michango kama mwanachama ni ili TUCTA kupitia vyama vyake ilivyovishirikisha itetee haki za mfanyakazi anapotendewa ndivyo sivyo na Mwajiri. Kwa UKIMYA ilionao TUCTA kwenye awamu hii ya 5 naiona iko sawa tu na Jumuiya zingine za CCM kama UWT au UVCCM.

Ukiniambia viongozi wanamuogopa Jiwe basi hawana sababu ya kuwa viongozi wa TUCTA. Karl Marx kwenye kitabu chake cha Communist Manifesto alisema nanukuu "“Workers of the World, Unite. You have nothing to lose but your chains!”

Nami nasema Wafanyakazi wa Tanzania tuungane tupate haki zetu zilizobanwa na Serikali ya Jiwe. Yafuatayo wanaweza kutendeka:
1. Tuwatose viongozi wa TUCTA kwa vile wamekuwa either Compromised na Serikali au wamekuwa THREATEANED. Kiasi kwamba TUCTA ya Tumaini Nyamuhokya imekuwa kama UVCCM

2. Tufungue kesi Mahakamani ya kutaka kusitishwa ukataji wa monthly deductions toka kwenye mshahara ya wanachama inayokatwa kama Trade Union fee mpaka Serikali itakapokubali kupandisha mishahara.
 
Mhanga mmojawapo. Nakushauri tu anzisha vuguvugu la chinichini mumpindue kiongozi wa chama chenu. Vinginevyo mtaendelea kupiga kelele na watu wako bize.
 
Mkuu serikali inaogopa trade unions pamoja kwamba ipo kisheria kama threat ya watawala wetu.Kisa wanaogopa migomo,lakini ukiwachunguza hofu yao ni kulipa wafanyakazi mshahara wenye mashiko.Na wao hawataki kabisa kuongeza mishahara kwa visingizio vya kujenga uchumi.
Lakini utasikia watawala wale wale wanataka Tanzania kukuwa kiuchumi na kufika kiwango cha middle class.
Sasa utakuwaje uchumi kiwango cha kati lakini wakati ule ule mnashindwa kuwalipa wafanyakazi mshahara wenye mashiko?
Yawezekana watawala hawajui watendalo.Ni vioja tu.
 
Umeongea point sana mkuu haiwezekani miaka 5 inapita tu hivi hivi hizi ni dharau sana kwa wafanyakazi tuungane tuwatoe viongozi wa tucta na vyama vyake mf tuico tughe nk

Sent using Jamii Forums mobile app
Nyie mchawi wenu hata sio TUCTA, na hivyo vyama vingine, vimepigwa ganzi na kung'olewa meno, mfuateni jiwe lilisotingishwa
 
Shida ya Watanzania ni elimu mbovu. Mtu akiambiwa mgomo au kuwatoa viongozi wa TUCTA anadhani atafukuwa kazi. Kumbe katiba ya JMT inatambua kwa vile imeridhia mikataba ya haki za wafanyakazi kwa mujibu wa ILO.

HOW DO YOU STAY 5 years solid without salary increment that reflects inflation and other economic adjustments between financial years?
 
Nyie mchawi wenu hata sio TUCTA, na hivyo vyama vingine, vimepigwa ganzi na kung'olewa meno, mfuateni jiwe lilisotingishwa
Jiwe lisilotikishika limejificha Chatto linaogopa ka kolona
 
Mkuu serikali inaogopa trade unions pamoja kuwepo kisheria kama threat ya watawala wetu.Kisa wanaogopa migomo,lakini ukiwachunguza hofu yao ni kulipa wafanyakazi mshahara wenye mashiko.Na wao hawataki kabisa kuongeza mishahara kwa visingizio vya kujenga uchumi.
Lakini utasikia watawala wale wale wanataka Tanzania kukuwa kiuchumi na kufika kiwango cha middle class.
Sasa utakuwaje uchumi kiwango cha kati lakini wakati ule ule mnashindwa kuwalipa wafanyakazi mshahara wenye mashiko?
Yawezekana watawala hawajui watendalo.Ni vioja tu.
Ndiyo maana napendekeza vuguvugu lianze kwa kuwapiga chini viongozi wa vyama vya wafanyakazi. Kwa nini tuwalipe mshahara wakati ofisi zimaweza kuendeshwa hata na Makatibu Muhtasi wao. Walipoomba ridhaa ya uongozi waliahidi kutetea masilahi, kama hawatetei tuwatoe
 
Mkuu hata wakichagua watu safi kwa sasa hasaidii,kwani nia na madhumuni ya hao wasiotaka maendeleo ya mfanyakazi ipo pale pale.
 
Me I am in!.. but How do we start this movements? ... something have to be done ,,tena mwaka huu ndo mzuri ,,corona itapita near uchaguzi tuwashe moto
 
How do we sytart this movement?? Kwa domo kaya hatuna mfano ila kimatendo hakuna. Tutabakia kubwabwaja humu JF tu mwisho; Nothing comes out in action. Tuwapige chini kivipi?? Kwa kuzivania ofisi zao usiku au kwa kuwapelekea vimelea?? Acheni kusema maneno mfu. Ka ni kupigika tumepigika kweli kweli. For 5 yrs
 
Me I am in!.. but How do we start this movements? ... something have to be done ,,tena mwaka huu ndo mzuri ,,corona itapita near uchaguzi tuwashe moto
Linaanza kwa kufungia milango viongozi wa TUCTA kwa sababu hawajitambui. Then inakuwa ni continuous mpaka tusimike viongozi wa mpito
 
Tuliyo yatarajia, ndiyo yaliyotokea kwenye Mei Mosi yake ya mwisho. Kiufupi tu hana faida yoyote ile kwa wafanyakazi wa nchi hii! Napata wakati mgumu kumfananisha na mtawala 'muongo' kwa wale anao watawala.

Ashukuru ana polisi wanao mpigania usiku na mchana, na tume mbovu ya uchaguzi. Kinyume na hapo, asingeamini matokeo yake kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka huu.
 
Nakumbuka hata Rashid Kawawa alikuwa ni Secretary General wa Tanzania Federation of Labour wakati wa Ukoloni miaka ya mwisho mwisho kabla ya uhuru. Hata JK Nyerere alitumia platform ya Rashid Kawawa kwenye vyama vya wafanyakazi kuweza kuijenga TANU. Mkoloni alitambua haki za vyama vya wafanyakazi kwa kuvifanya kuwapo mahali pa kazi na kufanya shughuli zake ikiwa ni pamoja na MIGOMO.

Nimeshuhudia sherehe nyingi sana za Mei Mosi throughout awamu zote 5. Kwenye awamu ya 4 tutamkumbuka Nicholas Mgaya alivyokuwa anaipelekesha Serikali kwenye kudai haki za wafanyakazi na kuhamasisha MIGOMO. Munielewe MIGOMO kwa vyama vya wafanyakazi siyo jinai bali ni mchakato unaotambuliwa kwenye Sheria za vyama. Na tulishuhudia namna Serikali ilivyokuwa inatii nguvu ya TUCTA kwa marekebisho ya mshahara au kwa maboresho ya mazingira ya kufanyia kazi

Kwa miaka hii 5 yafuatayo yamefanywa dhidi ya wafanyakazi wa Tanzania na TUCTA iko kimya:-

1. Wamewaondoa wafanyakazi kwa kisingizio cha "vyeti feki" kinyume cha Sheria na TUCTA haija watetea. Zoezi la vyeti feki ni magumashi matupu wala msilitetee. Mbona halikupita JW na POLISI.

2. Serikali haija pandisha mshahara ya wafanyakazi kukidhi hali ya uchumi na uzalishaji kwa kisingizio cha kujenga miundombinu kwa miaka 5 sasa.

3. Serikali imewaondoa wafanyakazi wengi kwa kisingizio cha kutumbua bila kufuata Sheria za kazi na Utumishi.

4. Wafanyakazi wamekuwa wanahamishwa kwenda Dodoma bila kupewa posho stahiki.

5. Wafanyakazi hawajapandishwa madaraja wala kupewa posho ziendanazo na madaraja hayo.

TUCTA huendeshwa kwa michango ya wafanyakazi ambayo wanakatwa kila mwezi kama mchango. Lengo la kutoa michango kama mwanachama ni ili TUCTA kupitia vyama vyake ilivyovishirikisha itetee haki za mfanyakazi anapotendewa ndivyo sivyo na Mwajiri. Kwa UKIMYA ilionao TUCTA kwenye awamu hii ya 5 naiona iko sawa tu na Jumuiya zingine za CCM kama UWT au UVCCM.

Ukiniambia viongozi wanamuogopa Jiwe basi hawana sababu ya kuwa viongozi wa TUCTA. Karl Marx kwenye kitabu chake cha Communist Manifesto alisema nanukuu "“Workers of the World, Unite. You have nothing to lose but your chains!”

Nami nasema Wafanyakazi wa Tanzania tuungane tupate haki zetu zilizobanwa na Serikali ya Jiwe. Yafuatayo wanaweza kutendeka:
1. Tuwatose viongozi wa TUCTA kwa vile wamekuwa either Compromised na Serikali au wamekuwa THREATEANED. Kiasi kwamba TUCTA ya Tumaini Nyamuhokya imekuwa kama UVCCM

2. Tufungue kesi Mahakamani ya kutaka kusitishwa ukataji wa monthly deductions toka kwenye mshahara ya wanachama inayokatwa kama Trade Union fee mpaka Serikali itakapokubali kupandisha mishahara.
naunga mkono hoja
 
naunga mkono hoja
Elimu ya vyama vya wafanyakazi na haki zao ni duni kwa Tanzania. Hii imedogoshwa na siasa za Ujamaa na Kujitegemea. Jaribu uangalie siasa za South Africa utakuta kitu kilikuwa kinaitwa SACTU (South African Congress of Trade Union). SACTU ilikuwa ina nguvu na in a way iliweza hadi kuinfluence ANC kwenye mapanbano dhidi ya sera za ubaguzi wa rangi. Hata Cyril Ramaphosa ni matunda ya SACTU kwa kuwa amewahi kuwa Secretary General wake.
 
Nakumbuka hata Rashid Kawawa alikuwa ni Secretary General wa Tanzania Federation of Labour wakati wa Ukoloni miaka ya mwisho mwisho kabla ya uhuru. Hata JK Nyerere alitumia platform ya Rashid Kawawa kwenye vyama vya wafanyakazi kuweza kuijenga TANU. Mkoloni alitambua haki za vyama vya wafanyakazi kwa kuvifanya kuwapo mahali pa kazi na kufanya shughuli zake ikiwa ni pamoja na MIGOMO.

Nimeshuhudia sherehe nyingi sana za Mei Mosi throughout awamu zote 5. Kwenye awamu ya 4 tutamkumbuka Nicholas Mgaya alivyokuwa anaipelekesha Serikali kwenye kudai haki za wafanyakazi na kuhamasisha MIGOMO. Munielewe MIGOMO kwa vyama vya wafanyakazi siyo jinai bali ni mchakato unaotambuliwa kwenye Sheria za vyama. Na tulishuhudia namna Serikali ilivyokuwa inatii nguvu ya TUCTA kwa marekebisho ya mshahara au kwa maboresho ya mazingira ya kufanyia kazi

Kwa miaka hii 5 yafuatayo yamefanywa dhidi ya wafanyakazi wa Tanzania na TUCTA iko kimya:-

1. Wamewaondoa wafanyakazi kwa kisingizio cha "vyeti feki" kinyume cha Sheria na TUCTA haija watetea. Zoezi la vyeti feki ni magumashi matupu wala msilitetee. Mbona halikupita JW na POLISI.

2. Serikali haija pandisha mshahara ya wafanyakazi kukidhi hali ya uchumi na uzalishaji kwa kisingizio cha kujenga miundombinu kwa miaka 5 sasa.

3. Serikali imewaondoa wafanyakazi wengi kwa kisingizio cha kutumbua bila kufuata Sheria za kazi na Utumishi.

4. Wafanyakazi wamekuwa wanahamishwa kwenda Dodoma bila kupewa posho stahiki.

5. Wafanyakazi hawajapandishwa madaraja wala kupewa posho ziendanazo na madaraja hayo.

TUCTA huendeshwa kwa michango ya wafanyakazi ambayo wanakatwa kila mwezi kama mchango. Lengo la kutoa michango kama mwanachama ni ili TUCTA kupitia vyama vyake ilivyovishirikisha itetee haki za mfanyakazi anapotendewa ndivyo sivyo na Mwajiri. Kwa UKIMYA ilionao TUCTA kwenye awamu hii ya 5 naiona iko sawa tu na Jumuiya zingine za CCM kama UWT au UVCCM.

Ukiniambia viongozi wanamuogopa Jiwe basi hawana sababu ya kuwa viongozi wa TUCTA. Karl Marx kwenye kitabu chake cha Communist Manifesto alisema nanukuu "“Workers of the World, Unite. You have nothing to lose but your chains!”

Nami nasema Wafanyakazi wa Tanzania tuungane tupate haki zetu zilizobanwa na Serikali ya Jiwe. Yafuatayo wanaweza kutendeka:
1. Tuwatose viongozi wa TUCTA kwa vile wamekuwa either Compromised na Serikali au wamekuwa THREATEANED. Kiasi kwamba TUCTA ya Tumaini Nyamuhokya imekuwa kama UVCCM

2. Tufungue kesi Mahakamani ya kutaka kusitishwa ukataji wa monthly deductions toka kwenye mshahara ya wanachama inayokatwa kama Trade Union fee mpaka Serikali itakapokubali kupandisha mishahara.
Kusema ukweli wafanyakazi tumenyanyasika awamu hii... Hakuna mahali dunia mfanyakazi wa umma amaweza kukaa miaka bila nyongeza, increment ya mshahara.... Jamaa amekaa kana kwamba hajui... Chapeni kazi???? Inauma sana.. TUCTA ni nafuu ya utopolo.... Yamekaa tu...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom