Mei Mosi ya Singida ilivyodhihirisha uzoba wetu wapiga kura na wasimamia kura

Mei Mosi ya Singida ilivyodhihirisha uzoba wetu wapiga kura na wasimamia kura

NewPage

JF-Expert Member
Joined
Mar 22, 2021
Posts
1,380
Reaction score
2,236
Ilikuwa vichekesho sana yaaani. Yaani kwanza kwa kuhofia wananzengo kutojaa uwanjani basi ukatumika uwanja mdogo na ukaachwa ule mkubwa. Ili kuhakikisha wananzengo wanatamani kuingia uwanja huo unapambwa vema ile mbaya na viti vizuri vinawekwa. Inasemekana viti hivyo vingine vilitoka Makao Makuu ya Nchi. Ili kutufanya wananzengo tujae basi tukawekewa maji makubwa kwenye kila kiti na kwa kuwa uwanja wenyewe upo pembeni ya barabara ukipita wanaona basi wananzengo tukafuata yale maji na kukaa kwenye vile viti vizuri.

Njoo sasa kwenye sherehe zenyewe, viongozi wote walioongea hawakusema jambo la maana kuhusu maslahi ya wafanyakazi. TUCTA wana miaka zaidi ya miaka 10 walitoa mtazamo kuwa mshahara wa kima cha chini ni shilingi laki 6 lakini juzi ndiyo imefikishwa kuwa laki 5 na wakashangilia mno kuwa Mama kaupiga mwingi (sisi wa kima cha chini bomba sana na bado tunasubiri mihela yetu wakati wa kusimamia kura ambazo tutazitick wenyewe na kuziingiza kwenye kituo cha kupigia kura). Basi kila aliyesimama kuongea alishindwa kutamaka neno haki ambalo lilikuwepo kwenye kauli mbiu ya Mei Mosi na badala yake wakasisitiza mambo ya utu ambayo hayapo kwenye Kauli mbiu hiyo na yapo kwenye Kauli mbiu ya Uchaguzi, ambayo kusudio lake ni kutufanya tuendelee kuwa na utu hata pale utu wetu unapokuwa haujatambulika.

Tukio kubwa kuliko lote lililoshangiliwa sana ni la Mwanamuziki Diamond. Huyu alisimamisha uwanja wote mpaka baadhi ya wanameza kuu. Huyu bwana alivyosimama tu kuimba akaanza na wimbo ulimwita Mwenyekiti yaan Mama ndiyo zilikuwa nyingi mnoo. Katika wimbo wake huo hakukuwa kabisa na neno Mei Mosi au maslahi ya sisi wananzengo na badala yake ilikuwa ni mambo ya mitano tena - Kampeni kabla ya wakati.

CCM tumelewa madaraka, tumekula tumevimbiwa, hadi kuchoka na kumkufuru Mungu. Yaani TUCTA wamlipe Diamond halafu yeye hata neno TUCTA au Mei Mosi kwenye wimbo wake halikuwepo. Kazi kweli kweli!
 
95% ya watumishi wa umma ni wapumbavuawa hawajitambui wanadhani kufanya kazi serikalini ni hisani na siyo haki
Hiyo ni kama ccm waonavyo wana vyo imbq amani,ila haki na usawa haiwahusu.Japo ni kusahau ahadi za uwanachama wao,bimadamu wote nisawa,Sitatoa wala kupokea rushwa,rushwa ni adui wa haki,Nitawahudumia watu kwa usawa na bila upendeleo,ila hawa viumbe wamevuja ahadi zao wenyewe tena zote.Hata ile ya kuwa wazalendo.Halafu wanabambikia Wazalendo wa kweli kesi mchongo.Ccm wote wafaa washitakiwe kwa uhaini na ugaidi.
 
Tunapoteza pesa nyingi kufanya sherehe za ajabu kama hizi zinazoambatana na sifa na uchawa ambao hauna faida. Hivi kweli kiasi cha 500k kwa mwezi mtu unaishi vp?
 
Hiyo ni kama ccm waonavyo wana vyo imbq amani,ila haki na usawa haiwahusu.Japo ni kusahau ahadi za uwanachama wao,bimadamu wote nisawa,Sitatoa wala kupokea rushwa,rushwa ni adui wa haki,Nitawahudumia watu kwa usawa na bila upendeleo,ila hawa viumbe wamevuja ahadi zao wenyewe tena zote.Hata ile ya kuwa wazalendo.Halafu wanabambikia Wazalendo wa kweli kesi mchongo.Ccm wote wafaa washitakiwe kwa uhaini na ugaidi.
WEll said!
 
CCM ni genge la mashetani tupu
 
Back
Top Bottom