Meja Jenerali wa Kirusi auawa huko Ukraine

Meja Jenerali wa Kirusi auawa huko Ukraine

Lazima kuwepo na International order inayoongoza utendaji, kusomeka na kueleweka kwa mataifa. Vinginevyo kila mwehu akiamka na kusema hayo maneno yako dunia haitatawalika, itakuwa uwanja wa vurugu tupu.
Ni mRusi pekee ndiye anayejua usalama wake ulipo na tishio la kushughulikiwa kwa haraka ni lipi. Tusitafute ujuzi wa kumwamlia lipi afanye na lipi asifanye.
 
Ingetokea Urusi kamuweza Ukraine
Finland angevamiwa na Taiwan ingevamiwa
"Amuweze" vipi tena, si hadi sasa maeneo ya Ukraine yeshatangazwa kuwa ni sehemu ya Urusi? Kuna kuweza zaidi ya hapo?
Kama mpango mzima wa kuanza kuiingilia Urusi yenyewe umesambaratishwa, kuna zaidi ya hilo?
 
Lazima kuwepo na International order inayoongoza utendaji, kusomeka na kueleweka kwa mataifa. Vinginevyo kila mwehu akiamka na kusema hayo maneno yako dunia haitatawalika, itakuwa uwanja wa vurugu tupu.
Sawa kabisa.
Sasa usisahau kwamba hao rafiki zako ndio waliokuwa mstari wa mbele kuhimiza wanayoona ya kwao ndio "international order" ya kufuatwa kwa amri na mataifa mengine yote duniani.
Wao wanaziita "values" zao, ndio 'values' za dunia nzima na ni lazima zifuatwe!
 
Ingetokea Urusi kamuweza Ukraine
Finland angevamiwa na Taiwan ingevamiwa
Wengi hawaelewei jinsi gani uimara wa Ukraine na msimamo thabiti wa West dhidi ya Putin na uvamizi wake umevuruga kabisa ndoto zake za kulazimisha matakwa yake kwa majirani zake kwa nguvu, vitisho na vurugu za vita. Hii itasaidia kudumisha amani Ulaya kwa muda mrefu sana. Hakuna nchi nyingine itavamiwa na Urusi kirahisi kwa siku za karibuni.
 
Sawa kabisa.
Sasa usisahau kwamba hao rafiki zako ndio waliokuwa mstari wa mbele kuhimiza wanayoona ya kwao ndio "international order" ya kufuatwa kwa amri na mataifa mengine yote duniani.
Mfano yapi waliyolazimisha??
 
Wewe endelea kuamini hivyo hivyo, naona huyajui maswala ya dunia hii.

Wewe hapa kila siku unapigana vita ya kuondoka kwenye umaskini wa kutupwa, ulishasikia hao wajomba zako wakikumiminia misaada kama wanayoimwaga Ukraine, ili ushinde hiyo vita yako?
Sana sana wanachofanya ni kutoa vimisaada vya kuzima akili na kuzilaza fofofo, kama unavyoonyesha hapa.
Je kati ya Ukraine na Urusi nani aliyemvamia mwenzake nakuanzisha vita vya kichokozi?
 
Ngoja nikupe mfano mwepesi mwepesi, lakini kuna mazito zaidi ya hapo.

USHOGA.
Kwamba West wamewalazmisha Africa Kusini au Brazil ambao ni wanachama wa BRICS kuruhusu ndoa za ushoga kwenye nchi zao??
 
Ni mRusi pekee ndiye anayejua usalama wake ulipo na tishio la kushughulikiwa kwa haraka ni lipi. Tusitafute ujuzi wa kumwamlia lipi afanye na lipi asifanye.
Vipi na Iddi Amini alipoivamia Tanzania nakutaka kuichukua kagera kulikuwa nae na tishio kwa Uganda na alikuwa anatafuta usalama wa Uganda?
 
Je kati ya Ukraine na Urusi nani aliyemvamia mwenzake nakuanzisha vita vya kichokozi?
Ukikubali kuwa "chambo" na kutumika kumnasa samaki, ni lazima uwe tayari kwa matokeo yatakayokukuta, ikiwa ni pamoja na huko unakokuita wewe "kuvamiwa".
 
Ukikubali kuwa "chambo" na kutumika kumnasa samaki, ni lazima uwe tayari kwa matokeo yatakayokukuta, ikiwa ni pamoja na huko unakokuita wewe "kuvamiwa".
Unakuaje chambo kwa mfano? Ni jambo gani ukilifanya unahesabika umekubali kuwa chambo??
 
Kwamba West wamewalazmisha Africa Kusini au Brazil ambao ni wanachama wa BRICS kuruhusu ndoa za ushoga kwenye nchi zao??
hayo a Afrika Kusini au Brazil siyajui, lakini ninachojua ni kuwa hao jamaa zako ni 'snobbish' sana. Hawajasahau kuwa walikuwa na 'privilege' ya kuiendesha dunia yote watakavyo wao. Bado wanaamini kwamba dunia ni lazima iwe kama walivyo wao, vinginevyo hivyo viwango vingine vya maisha ya watu havikidhi viwango.
 
Vipi na Iddi Amini alipoivamia Tanzania nakutaka kuichukua kagera kulikuwa nae na tishio kwa Uganda na alikuwa anatafuta usalama wa Uganda?
Ukitaka mifano ya aina hiyo ipo mingi sana, kama Iraq na kwingineko.
Ndiyo maana nakueleza kwamba ufahamu wako wa haya mambo bado ni mdogo sana. Panua akili yako mkuu 'Paschal qamara'
 
NATO wana mandege? Wameyatoa wap,aise? Yaliwahi kutumika wapi kwa mfano 🤔
Kwamba NATO haina Mandege? Akili yako ina uwezo wa Kushangilia uuzwaji wa Bandari za Tanganyika? Hivi US na Mandege yake ilijitoa lini kwenye shirika la NATO?
 
Najua huyajui ndio maana najaribu kupanua ufahamu wako.

Back
Top Bottom