Meja wa Burundi auawa huko Kivu kusini

Meja wa Burundi auawa huko Kivu kusini

MBOKA NA NGAI

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2025
Posts
350
Reaction score
576
Meja Evariste Ndayizeye kutoka jeshi la Burundi, anaesadikika kuwa miongoni mwa wapiganaji mahili, ameuliwa na M23 huko Kivu kusini.

Ni katika mapambano ya M23 kuhakikisha inaudunga uwanja wa ndege wa Kavumu. Inasemekana kwamba mpaka sasa, wapiganaji wapo umbali wa Kilometa saba na wameshauzingira uwanja huo.

Huku jeshi la Burundi, likiwa na wanajeshi wapatao elfu nne kuulinda uwanja huo.

IMG_0027.jpeg
 
M23 wapo wangapi kama hadi jeshi la watu 4k wana jambishwa ,tena majeshi ya nchi mbalimbali
Hivi, unajua hata mwanajeshi kwa roho ya kawaida anaangalia na vigezo vya kupigana? Wenzao walishahukumiwa kufungwa maisha. Mwanajeshi mtutsi, usifikilie ni rahisi kupigana na M23. Wengine walishajiweka mikononi mwa Red-Tabara. Inayosubili tu njia ya kuungana na M23. Hivi ni vita vya watu wanaojuana wenyewe, haviko serious kivile. Unaweza ukakuta hao 4k nusu yake hawana mpango. Wanashitakiana usaliti. Unaanzaje sasa!!!
 
Warundi wanafia nini Kongo wakati asilimia kubwa ya Wananchi wao huwa wanalala na njaa.

Hizo fedha wanazotumia huko Kongo kununua risasi na Mabomu angalao wangekuwa wanawapa koo masikini za Burundi.
 
Kwanini hamumlaumu Kagame muda wote kuhangaika na mambo ya Congo?
Kuna strategic objectives lazima zilindwe!

Burundi ikiachia M23 wachukue kivu yote maana yake watakuwa wamezungukwa! Next target itakuwa Burundi yeneyewe kusimika utawala wa Kitutsi!

Kimsingi, M23 na Watutsi wanaweza kuteka maeneo leo lakini hawataweza kutawala maana wapo wachache! Another grand scale genocide is cooking!
 
Burundi ikiachia M23 wachukue kivu yote maana yake watakuwa wamezungukwa! Next target itakuwa Burundi yeneyew
Burundi pia ilikuwa ni himaya ya Wafalme wa Kitutsi, wamrudishe Mwami tu. Nchi itulie.
 
Nauona mwisho mbaya wa kagame. Atakufa vibaya kwa sababu ya tamaa yake. Japo kuna mataifa kama uganda yameungana nae mambo yakigeuka watapoteana na hasara kwake itakuwa kubwa maana mwisho wa ubaya ni aibu.

Jiulize kwa nini wanatoa ripoti ya hasara iliyotokea kwa jeshi la kongo lakini hawataji viongozi wa majeshi ya rwanda na uganda? Unadhani wao hawafi?
 
Warundi wanafia nini Kongo wakati asilimia kubwa ya Wananchi wao huwa wanalala na njaa.

Hizo fedha wanazotumia huko Kongo kununua risasi na Mabomu angalao wangekuwa wanawapa koo masikini za Burundi.
Vita ni biashara, nipe jeshi, nikupe dhahabu...baasi
 
Kimsingi, M23 na Watutsi wanaweza kuteka maeneo leo lakini hawataweza kutawala maana wapo wachache! Another grand scale genocide is cooking!
Kama tupo serious sasa, hili ndio la kulitazama kwa tahadhari ya kiwango cha juu
 
Warundi wanafia nini Kongo wakati asilimia kubwa ya Wananchi wao huwa wanalala na njaa.

Hizo fedha wanazotumia huko Kongo kununua risasi na Mabomu angalao wangekuwa wanawapa koo masikini za Burundi.
M23 Wakiteka bukavu basi ujue Burundi hali itakuwa tete kabisa vita vina mipango ya mbali sana hasa hv vya kikabila ni hatari sana
 
Meja Evariste Ndayizeye kutoka jeshi la Burundi, anaesadikika kuwa miongoni mwa wapiganaji mahili, ameuliwa na M23 huko Kivu kusini.

Ni katika mapambano ya M23 kuhakikisha inaudunga uwanja wa ndege wa Kavumu. Inasemekana kwamba mpaka sasa, wapiganaji wapo umbali wa Kilometa saba na wameshauzingira uwanja huo.

Huku jeshi la Burundi, likiwa na wanajeshi wapatao elfu nne kuulinda uwanja huo.

Burundi na Rwanda wanapambana ndani ya Drc.

Tresor Mandala
 
Back
Top Bottom